Kujengea makaburi ya Waliotutangulia - Kuna umuhimu wowote?

Kujengea makaburi ya Waliotutangulia - Kuna umuhimu wowote?

Wadau mbona mna maneno makali sana... Nazungumzia nakshi jamani yaan inafika mahali watu wanapamba makaburi as if aliyekufa anashuhudia au kutoa shukrani kwa kilichofanyika!

Kuweka kumbukumbu sio issue issue ni kunakshi mpaka inakuwa kufuru. Kwanini ile pesa isitumike kuyaenzi mazuri aliyoyaacha au kusaidia watoto au jamaa zake????

Sidhanikm tiles ni kufuru...maana box ni elfu 8 tuuu
 
Nakshi sio mbaya ni poa tuu kana pesa inaruhu unafanya tuu,,,,,
hiyo ni sawa na uki bar unakunywa bia unashushia na nyama choma/mchemsho/supu
au
unatafuna supu na chapati pembeni
au
unapiga wine/konyagi bila kusahau mgegedo utapata
au
unaoga baada ya hapo kuna bodyspray au lotion pembeni
au
unatoka out bila kusahau mkoba/ kwapani/mkonon au wallate mfukoni
mengne utaongeza lkn kimantiki ni hivyo unajengea kama pesa ina ruhusu unamalizia nakshi,japo sii lazima.na ndoo maana wengine wana weka nakshi wengne hawaweki hii naamini ni kutokana na uwezo wa kifedha,manaake wengne baada ya ujenzi utaskia 'tutakuja kufanyia finishing,mambo yakiwa mazuri'
 
Ni kawaida tu, maana kuna mambo mengi ya dizaini: km vile mtu alikuwa anapendwa sana lakini akifa anachomwa moto, au ishu ya kujali au kutojali mgonjwa ni sawa na ukiwa na jamaa anakupeleka bar anakununuli bia hata za elfu 30 lakini ukimuomba shilingi mia tano hakupi!
 
Tunajengea ili lisipotee kama kumbukumbu kwa wapendwa wetu, njoo uone makaburini ya Kinondoni ambayo hayajengewa yanavyo potea.

Binadamu wengi hawapendi kukubali kifo kama ni mwisho na aliyefariki hata tungempenda vipi hatoonekana tena kwenye uso wa dunia. kujenga makaburi ya kifahari ni woga, hofu na ubatili
 
Mkuu unajua kujengea hakuna shida ila kuweka nakshi, mara marumaru, mara kuweka kivuli ndio shida! kwani ukijenga kawaida kumbukumbu haibaki???

Hizo ni mbwembwe tu kama wewe unavyo jiremba hakukubadili usiitwe mwanadamu.
 
Binadamu wengi hawapendi kukubali kifo kama ni mwisho na aliyefariki hata tungempenda vipi hatoonekana tena kwenye uso wa dunia. kujenga makaburi ya kifahari ni woga, hofu na ubatili

Ni ishara ya upendo wa dhati kwa marehemu.
 
charminglady Je siku ukifa watoto zako wasijengee kaburi lako?
Si litapotea kabisa, kule moshi utasikia hapo kwenye sale alizikwa
mzee fulani siku hizi wanajengea, huku mjini wasipojengea ndo
kabisa utakuta siku moja mtu mwingine amezikwa juu yako.

Hizo nakshi ni matanuzi tu, kama pesa ipo nao wanataka wajitanue hivyo.

Kuhusu kumjali mgonjwa hilo nalo ni neno kwa kuwa huwa tunajisahau sana
wakati mwingine.

Mie hata wakinitupa bila kuzika it up to wao.. Wakati huo sitakuwa charminglady bali marehemu. Uzuri hakuna jalala la binadamu najua tu watanichimbia shimo waniweke....

Tena nitapenda hata mwili wangu ufanyiwe "practical" Ngoja nitafute ni jinsi gani naweza fanya hivi. Sitaki kumbukumbu yangu iwekwe katika kaburi langu!!! Nawish nipoteelee mavumbini tu!!
 
Last edited by a moderator:
kujengea kaburi si tatizo maana kunalifanya lidumu usipojenga linapotea na kufutika kabisaa..tatizo kuweka nakshi za thamani sioni maana yeyote

Kwani likipotea kuna tatizo gani?
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Binadamu wengi hawapendi kukubali kifo kama ni mwisho na aliyefariki hata tungempenda vipi hatoonekana tena kwenye uso wa dunia. kujenga makaburi ya kifahari ni woga, hofu na ubatili

Well said mkuu, tena hakubadili chochote katika marehemu huyo... Bora fedha hizo zitumiwe hata wakati wa matanga kuliko kugharamika kujenga kaburi la kifahari!!!!!!!!
 
Habari za asubuhi ya leo wapendwa wana Jamvi....

Kwanza niombe radhi kwa nitakaowakwaza kwa namna moja ama nyingine.

Kuna suala hili huwa linanitatiza naomba kuelewesha.

Kumezuka tabia ya kujengea makaburi kwa marumaru ya samani za aina tofauti tofauti tena zenye gharama kubwa, Utakuta mtu alikuwa anaumwa kwa muda mrefu lakini watu hawakujitokeza kumhudumia lakini baada ya mtu huyo kufariki dunia wanajitokeza ndugu, jamaa na marafiki wanapanga mipango ya kujengea kaburi lake na kuweka nakshi ya kila aina.

Je watu hawa walikuwa wapi wakati wa ugonjwa??

Je kujengea kaburi hilo kutamsaidia nini yule marehemu??

Kuna watu wanafariki ghafla aidha kwa ajali ama kifo cha aina yoyote ila kwa ghafla... Kuna ulazima gani wa kulinakshi kaburi???

Tena kuna wengine wamekwenda mbali wakaanza kutafuta makaburi haya ya mababu zao na kuanza kuyajengea na kuyaweka katika hali ya unadhifu kana kwamba kilichomo ndani yake kina thamani... Tena na kufanya sherehe sijui ya kujengea makaburi... Ni nini maana yake???

Kwa mtazamo wangu ujenzi huu wa kuweka nakshi ni kugharamika kusiko na faida...

N.B. Ni mtazamo tu naomba nisipondwe mawe....
Ile ni huduma kwa waliohai kujifariji kwamba hata wao wakifa mambo yatawekwa sawa na wataburudika; ni aina fulani ya kutibu hofu zetu za kufa na kupunguza stress za maisha. Kwa maneno mengine ni tiba kwa waliohai kwani wanadamu wote ni wagonjwa akilini kwa namna moja au nyingine.
 
Mkuu unajua kujengea hakuna shida ila kuweka nakshi, mara marumaru, mara kuweka kivuli ndio shida! kwani ukijenga kawaida kumbukumbu haibaki???

Suala la marumaru yaweza kuonekana anasa kwako ila kwa wengine ni kawaida kutokana na ukwasi.......,labda kwako CL ikoje kwa makaburi ya wapendwa wako (hasa hasa kama ni wazazi wako-samahani kama wapo hai )
 
Mie hata wakinitupa bila kuzika it up to wao.. Wakati huo sitakuwa charminglady bali marehemu. Uzuri hakuna jalala la binadamu najua tu watanichimbia shimo waniweke....

Tena nitapenda hata mwili wangu ufanyiwe "practical" Ngoja nitafute ni jinsi gani naweza fanya hivi. Sitaki kumbukumbu yangu iwekwe katika kaburi langu!!! Nawish nipoteelee mavumbini tu!!

Aliwazalo mjinga ndilo litakalo mtokea,Asemacho mtu ndicho anacho maanisha,
NOTE;simaanishi kuwa wewe ni mjinga nope ila naheshimu tamko lako.
 
Last edited by a moderator:
ww kama huna hela za kujengea kaa kimya. mama yangu amefariki tumetumia uwezo wetu wote lkn Mungu hakupends apone. Kaburi tumejengea na kulinaksh kwa tulikopa kwako au kwa mtu yeyote? kaa kimya bwana

Daaah, alishaomba radhi kwa atakaowakwaza! shambulia hoja na usimbshambulie yeye! TUMEUMBWA TOFAUTI NA TUNATENDA TOFAUTI!
 
Aliwazalo mjinga ndilo litakalo mtokea,Asemacho mtu ndicho anacho maanisha,
NOTE;simaanishi kuwa wewe ni mjinga nope ila naheshimu tamko lako.

Wewe ndin mjinga kabisa! Bila watu kutoa maiti zao zikafanyiwe majaribio na kujifunza hiyo technogy inayotumika kukutibu wewe ingeshushwa kutoka mbinguni? Hiyo CT-scan watu wangeoteshwa na malaika Ng'wana Mashiku?

Mimi pia nafuta mwanasheria wa kunisaidia ili nikifa mwili wapeleke maabara wanafunzi wajifunzie!
 
Ngoja nikuitie Mtambuzi inaonyesha una tatizo la kisaikolojia.
Mie hata wakinitupa bila kuzika it up to wao.. Wakati huo sitakuwa charminglady bali marehemu. Uzuri hakuna jalala la binadamu najua tu watanichimbia shimo waniweke....

Tena nitapenda hata mwili wangu ufanyiwe "practical" Ngoja nitafute ni jinsi gani naweza fanya hivi. Sitaki kumbukumbu yangu iwekwe katika kaburi langu!!! Nawish nipoteelee mavumbini tu!!
 
Last edited by a moderator:
Aliwazalo mjinga ndilo litakalo mtokea,Asemacho mtu ndicho anacho maanisha,
NOTE;simaanishi kuwa wewe ni mjinga nope ila naheshimu tamko lako.

Kama mimi ni mjinga basi walioamuru wakifa miili yao itumike katika Practical watakuwa wajinga square..

Bila hizo practical watu wangetibiwaje??

BTW.. Huwezi kuniita mimi mjinga make hunifahamu na wala hutokaa unifahamu!
 
Uko sahihi dada yangu hakuna ulazima wa kujengea makaburi...unachoweza kufanya ni kuweka kisaruji upande wa kichwani na ukaandika jina lake, siku alozaliwa na kuzikwa...Kinachomfaa maiti baada ya kufa ni mambo ma3 tu:

1. Sadaka yenye kuendelea kama aliacha kitu cha kuwasaidia watu....Kisima, Hospitali, Public toilet au hata miti kama aliipanda. Watu,wanyama,ndege au hata wadudu wakiwa wanaendelea kunufaika.
2. Elimu yenye kuwafaa watu...Alimfundisha mtu kuchonga vitanda,uhasibu, au taaluma yoyote ile ya halali...yeye ataendelea kupata malipo ya elimu ile kwa kila ataenufaika na elimu ile...hata wakisomeshwa watu wengine...madhali yeye ndo chanzo basi yeye atapata malipo.
3.Mtoto mwema/au Jamaa wema ambao wanaendelea kumuombe dua.

Kwa hio kujengea makaburi ni kupoteza muda na kujidanganya kwa roho zetu...wadudu chini hawana habari na Tazi zetu.

Tujiandae na safari sisi...ni msosi wa wadudu tu!
issue ni kujengea au kujenga kwa gharama! kwa sababu hataukiweka mchanga wa kawaida tu umejengea,ukiweka tiles umejengea ...ukifunika kwa tanzanite napo umejengea!,amabaye anaweza kujenga hoja hapa ni wale wanaotupa maiti ndio wangeuliza kwanini mnajengea ! akama hali inaruhusu jenga ,pamba kaburi la marehemu...! Mimi alipolazwa baba yangu nikama chumbani kwake ,nikifika nyumbani lazima nikatoe heshima pale na kuweka maua ,hata watoto wangu nimewafundisha hivyo ,baba yabgu kwangu alikuwa MTAKATIFU kama wale wa Roma au Uganda,au alikuwa kama AYATOLAH KHOMEIN WA IRAN watu walipokanyagana kugusa jeneza lake!
 
Wamisri walikuwa wanajenga pyramids! Itakuwa hivi vikaburi vya mita tatu kwa mita mbili?
 
Kutoa maiti yangu ikafanyiwe Practical ni tatizo la kisaikolojia??

Ngoja nikusaidie kuwaita hapa...

Mzee Mtambuzi na kaka Pasco tunaomba msaada wenu hapa!
Dear CL, kuna issues 3 hapa zihusuzo kujengea makaburi!.

  1. Kuweka Alama- Hii ndio sababu kuu ya kujengea makaburi, ili tuu kuweka mark, nani alizikwa hapa, kaburi lisipotee. Ujenzi wa kuweka alama ni simple na wala hautumii gharama kubwa!.
  2. Kumplease Marehemu!. Watu wanajengea makaburi kwa gharama kubwa ili kujifariji nafsi zao kuwa ndio namna bora ya kumuenzi marehemu!, kwa kadri familia ilivyo na uwezo, ndivyo kaburi la thamani linavyojengwa hadi mengine kuwa kama minara, hivyo kuonyesha jeuri ya pesa.
  3. Kujengea makaburi kama sehemu ya kuabudia!. Hizi ni ibada za wafu!. Kuna makaburi yanajengwa kama shrines kwa watu wa ukoo ule kwenda hapo, kufanya misa, ibada, kumbukumbu hata kutoa makafara ya kiukoo!, hawa ndio wale utasikia hata akifia wapi, lazima akazikwe kwao ili wakafanye mambo yao!.
My take:
Mwili wa binadamu una sehemu kuu mbili, mwili na roho!. Mwili unakufa na kugeuka mavumbi, roho haifi, inadumu milele!. Mwili ukiishakufu, its nothing!, hata wafanyao ibada za wafu kwa kuombea dua miili, kupeleka nyumba za ibada, kusali misa za kumbukumbu za marehemu, kwenda kusali makaburini, kujengea makaburi, au anything to do with a dead body ni ubatili tuu, kwa watu kujifariji na kujifurahisha nafsi zao, a dead body is a dead body!.

Wako wengi wanaofanya ibada za wafu!, hawajijui kuwa hizo ni ibada za mashetani!. Bwana Wetu Yesu Kristu, alituasa
"Waacheni wafu wawazike wafu wao!".

Watu enlightened, wanakuwa wamefunuliwa kuijua kweli, ndio maana wengi wakifa, wanachomwa au kufanyiwa creamation kwa sababu the deadbody or lifeless body is nothing at all!. Kenda kusali makaburini ni ibada za kishetani kwa kujua au kutojua!.

Mtu anayetoa mwili wake kufanywa cadaver is better of kuliko ule mwili, uliovishwa vito vya dhahabu na almasi, ukazikwa kwenye jeneza la kioo, alminium au la mbao lilitengenezwa vizuri na kupabwa sana hadi maua!, kisha kaburi likajengwa na marumaru, granite, tiles, etc ili lipendeze machoni, what befals that body huko ulimo, its the same!.

Pasco
 
Back
Top Bottom