Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,914
- Thread starter
- #201
MkuuLakini kitu cha kustaajabisha sana ni kuwa wameweza kueleza kwa ufasaha sana vitu vinavyoishi ndani ya hiyo kuiper belt, hadi kufikia ku-categorize aina ya hao aliens na tabia zao hadi mission zao na jinsi wanavyotuchukulia sisi.
kila aina na mipango iliyonayo kuhusu binadamu, as if kama hao wataalamu walikaa meza moja na hao aliens na kupia story.
Sasa inakua vigumu kidogo mtu kuelewa kwa kweli maana kama huo ukanda tu bado hawaujui kwa asilimia mia unawezaje kujua kilichopo ndani yake na kukielezea kwa ufasaha namna hiyo.
kwa mafano mtu ameona nyumba kwa mbali na kwa sababu ya umbali hawezi kujua rangi ya bati la hiyo nyumba kuwa ni blue au kijani, lakini hapo hapo anakuelezea kwa ufasaha kuhusu mazingira ya ndani ya nyumba jinsi yalivyo.
inakua na ukakasi sana kuelewa
Nafurahi sana kusikia kuwa unasoma maandiko yangu kwa makini lakini pia ninafurahi kujua kuwa umesoma na baadaye umeuliza pale ambapo umeshindwa kuelewa....
Iko namna hii..
Uwepo wa Aliens upo kabla hata ya ugunduzi wa Kuiper Belt hivyo basi ya uwepo wa Aliens siyo Kuiper Belt isipokuwa tu baada ya kugunduliwa kwa mkanda huu kuna wataalam wamefanya utafiti na kujua kuwa huko ndiko makao ya hawa Aliens jambo ambalo linaweza kuwa siyo kweli...
Kwa taarifa nilizozipata siku chache zilizopita ni kwamba Aliens wanafanya kukutana huko kwenye Kuiper Belt kwaajili ya kuandaa mpango wao wa kuja duniani ramsi na inadaiwa kuwa siyo mbali sana tukio hili litatokea hivyo tunaambiwa tukae tayari tayari....
Pamoja na hayo yote ni kwamba uwepo wa Aliens na mission zao kutuhusu pamoja na aina ya hao Aliens haijajulikana baada ya kujulikana kwa Kuiper Belt bali kabla ya hapo kwasababu Aliens wamekuwa wakishirikiana na binadamu kwa mambo mengi sana na wamekuwa wakieleza mengi kuwahusu....
Kitu ambacho wengi wanapaswa wakielewe ni kwamba,haijajulikana haswa hawa Aliens wanapanga nini au lengo lao ni nini kwa hakika kwasababu inawezekana hao Alines hawatoi taarifa sahihi kwa binadamu au wanaweza kuwa wanatoa taarifa sahihi...
Pia inawezekana wanaotueleza hawatuelezi taarifa sahihi kuwahusu kwa faida yao wao wenyewe hivyo sisi watu wa kawaida tupo njia panda kuhusu jambo hili lakini ukweli ni kwamba hawa viumbe wapo....