Kuiper Belt: Behind the certain

Kuiper Belt: Behind the certain

Anzisha uzi wako wa namna gani mnatengeneza haya mambo kupotosha watu acha huu uzi ujitegemee.
 
Mkuu nakuomba tafadhali, acha kupoteza watanzania.
Acha waliopo ambao hawajui huu ujinga wakae wafanye mambo mengine ya msingi. Ulichondika ni uongo mtupu na huna evidence hata moja zaidi ya vipicha ulivyoleta kutoka kwenye blog ambazo hata miminilishiriki kuziandika miaka ya zamani kusambaza uongo maana zilikua zinalipa, kutengeneza $150 kwa siku ilikua ni kugusa tu. Ila nimeelimika nikaona negative side of it nikaacha nikaanza kufanya mambo mengine ya halali ya maana. Nilikua natumia hata photoshop kukaa na kutengeneza picha fake za aliens kua wameonekana maeneo mbalimbali kama evidence na watu wanaamini, I'm super good at photoshop huwezi ona picha ukasema its fake. Picha zote ulizoleta hapo ni fake, I am 100% sure.

Aliens labda wapo, ila hatujadetect hata moja, the closest thing ambacho tumedetect tukajichanganya kusema ni aliens ni Pulsars, hizi ni neutron stars zinakua zinaemit huge amounts of radiations katika interval moja nzuri sana kiasi kwamba the first time inakua detected miaka ya 1960s wanasayansi walidhani ni message kutoka kwa aliens imekua decoded, later on wakaja kugundua ni just stars. Nimeattend meetings nyingi sana za astronomy, nilikua napenda sana astronomy wakati nipo chuoni, nimekaa nawasikiliza watu wengine very popular duniani in science live, ukipeleka huu ujinga mbele yao watakucheka.

Huwajui NASA, wala any space agency wanavyo-operate, wala hujui wanaohusika na space research, ila ungekua umezunguka au umesumbua hata kichwa kidogo ungetambua kua ni watu ka wewe na mimi tu na they are smart enough kutokukaa wanafuatilia huu ujinga, ukiwa bongo kila kitu unaaminishwa unabeba, kikiwa tu kwenye blog watu mnameza, hizo blog tunaandika sisi sio malaika, advertising is a serious business. Ngoja nikwambie how it will happen, siku ikitokea tumedetect aliens, dunia nzima itajua, na utasikia kwenye reputable sources zote dunia nzima, wala haitofichwa, na kama extraterrestrial beings wapo hadi sasa na hatujawatambua basi ni obvious they are smarter than us, wanafikiria kwa uwezo zaidi kuliko wa kwetu, au wapo kwenye a completely different life form sio tuliyozoea, if thats the case probability ya sisi kuwatambua ni next to zero.

TLDR Tafadhali usipotoshe watanzania.
Anzisha uzi wako kuonesha namna gani umeshiriki uache uzi huu ujitegemee Tuendelee kuunganisha dots
 
Graph ,habari yako?

Kwanza kabisa naona kuna makosa kadhaa umeyafanya wakati unasoma japokuwa inawezekana hata hujasoma nilichoandika....

1;Mimi nimesema Aliens wapo.Hoja yangu hii ina base yake na base hiyo siyo NASA bali tafiti ambazo zimefanywa na wanaanga mbali mbali waliokuja na dhana zao kuhusu hawa viumbe lakini kikubwa aidi ni shuhuda za mashuhuda waliowahi kuona hawa viumbe na wengine kukabiliana nao katika namna tofauti tofauti kwenye maisha yao,hivyo wewe kudhani kuwa base yangu ni NASA ni makosa ya kiuelewa uliyonayo kwenye makala hii...

2;Mwanzo umeanza kunirushia shutuma kwamba ninapoteza Watanzania kwa sababu ninaandika habari za uzushi lakini hapo hapo unasema "inawezekana Aliens wapo".Mkuu kumbe inawezekana nilichoandika kiko sahihi,sasa ni kwanini unaniambia napotosha?Kama unaona kuna huo uwezekano wa hawa viumbe kuwepo,ni kwanini usisisitize watu waendelee kutafiti zaidi na badala yake unawaambia kuwa waache? Kwanini unataka watu waache kutafiti kitu ambacho kwa maelezo yako inawezekana kipo?

Hapo juu nimeonesha uwezekano wa kuwepo kwa malengo hasi ya hawa viumbe kwa uwepo wa binadamu hapa duniani kitu ambacho ni hatari kwetu na sisi kujua uwepo wao kutatufanya tuwe katika mazingira mazuri angalau ya kukabiliana nao kuliko kukaa tu na kuamini hawapo halafu ukute wapo halafu kesho watumalize kizuzu.unapotuambia tuachane nao unataka tuje tuangamie kijinga tu? [kama wapo]

3;Hkuna aliyesema wanasayansi ni malaika au watu fulani special sana kiasi kwamba tuwachukulie kwa namna tofauti.Ninajua ni wanadamu,lakini kwao kuwa wanadamu haimaanishi tudharau kila wanachotuambia.Tupo hapa leo kutokana na tafiti mbali mbali za watu hawa hivyo ni wa muhimu sana kwetu.Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni kwamba kuna watu wanajiona wao wanaelewa sana mambo kwasababu tu wamekutana na uzoefu fulani fulani maeneo mbali mbali duniani na kujiona wamemaliza....

Brother/Sister JF inakusanya watu wa aina tofauti tofauti sana,humu hatujuani hivyo hujui hata mimi ni nani na ninajishughulisha na nini,kuanza kudhani tu kuwa ninaamini kila kinachoandikwa mtandaoni ni kuona kama sifikirii kabisa kitu ambacho siyo sahihi kabisa.Wewe kuwahi kuandika uzushi kuhusu Aliens hakufanyi Aliens wasiwepo au kuwepo.Unachodhani sikijui hujui kama sikijui na unachodhani sijawahi kukifanya hujui kama sijawahi kukifanya hivyo kuwa makini unapokuwa unajibu jambo lolote hapa JF kwakuwa hujui unajibizana na nani....

Acha majigambo yasiyokuwa na maana weka hoja mezani.Kama wewe ushawahi kuandika kuhusu uongo wa Aliens haimaanishi kuwa unaelewa sana kuhusu haya mambo.Mimi kuandika kuhusu Aliens hapa JF haimaanishi kuwa ninaelewa sana kuliko watu wengine bali tunajaribu kubadilishana tu uzoefu hapa kwa kuheshimiana...

La mwisho..
Naona hata hujasoma thread yote ndiyo maana umekuja na hoja ya kuwa picha nilizoweka ni fake.Ninajua kuwa nimeweka picha ambazo siyo halisi na nimelisema hilo kwenye post zangu kadhaa kwenye uzi huu hivyo ninakushangaa tu unapokuja kwa speed ya mwanga kuanza kutaka kuonesha kuwa unaelewa sana juu ya hizo picha.nimeweka hizo picha kusaidia tu watu kuelewa nimeandika kitu gani na kinahusu nini na siyo zaidi ya hapo....

Wakati mwingine jitahidi kujadili hoja na siyo viroja...
 
Kituko

Kwema mkuu?

Ishu ya mapiramidi ina mengi sana mkuu na historia yake ni ndefu sana na iko siku tutajitahidi kuja kuyachambua hapa hapa JF,tuombe uzima tu....

Ukweli mchungu sana ni kwamba wengi,kama siyo wote tumeaminishwa kwamba binadamu wa leo ndiye mwenye maendeleo makubwa ya kisayansi kuliko binadamu wa nyakati yoyote kitu ambacho kwa wale wafuatiliaji wa mambo wanaona siyo kweli kabisa....

Hizo Nazca lines na mengine mengi ni moja kati ya mambo mengi ambayo yanaonesha kuna mahali tumedanganywa kabisa.Huwezi kutengeneza kitu ambacho unapata view nzuri na maana nzuri ya mchoro ukiwa umbali mrefu angani kama huwezi kufika umbali huo...

Kama ulivyojiuliza ni kwamba haiwezekani kabisa.Hawa watu walikuwa na uwezo wa kwenda umbali huo angani na ndiyo maana wameweza kutengeneza hiyo michoro....

Annunaki

Hawa ni viumbe waliowahi kufika hapa duniani miaka mingi iliyopita na watafiti mbali mbali wanatofautiana juu ya viumbe hawa kuhusu kilichowaleta na walipo leo.Mtu kama Zachariah Thitchin ana theory yake.Mtu kama Tom Horn ana dhana yake na wengine wengi lakini kimsingi ni kwamba hii nayo ni ishu nyingine na siku moja tutaijadili pia....

hao wageni wanaosemwa na hilo kabila la Dogon ni hao hao Annunaki,siku tukiwajadili kwa kina tutaelezea pia hayo yote mkuu....
 
Anzisha uzi wako kuonesha namna gani umeshiriki uache uzi huu ujitegemee Tuendelee kuunganisha dots
Kabisa mkuu...

Siyo kila kitu ni kubishana tu tena ubishani usiokuwa na msingi kabisa....
 
Mkuu Eiyer kun wakati uliahidi kuleta mtiririko wa jinsi hivi vyama vya siri vilivyoanza na mlengo yao, ndhani ndio wakati huu sasa na ningeomba kama hautajali ile mwanzo sura ya 3 na 6 maelezo yke kidogo.
 
Anzisha uzi wako kuonesha namna gani umeshiriki uache uzi huu ujitegemee Tuendelee kuunganisha dots
Haina haja, watu wanapenda kuambiwa wanachotaka kusikia, ukiwaaambia tofauti hata kama ni facts hawataki kuamini kwa kua wanapenda kuwa kwenye bubble yao waliyoizoea, kutoka nje ni kazi sana.
 
Graph ,habari yako?

Kwanza kabisa naona kuna makosa kadhaa umeyafanya wakati unasoma japokuwa inawezekana hata hujasoma nilichoandika....

1;Mimi nimesema Aliens wapo.Hoja yangu hii ina base yake na base hiyo siyo NASA bali tafiti ambazo zimefanywa na wanaanga mbali mbali waliokuja na dhana zao kuhusu hawa viumbe lakini kikubwa aidi ni shuhuda za mashuhuda waliowahi kuona hawa viumbe na wengine kukabiliana nao katika namna tofauti tofauti kwenye maisha yao,hivyo wewe kudhani kuwa base yangu ni NASA ni makosa ya kiuelewa uliyonayo kwenye makala hii...

2;Mwanzo umeanza kunirushia shutuma kwamba ninapoteza Watanzania kwa sababu ninaandika habari za uzushi lakini hapo hapo unasema "inawezekana Aliens wapo".Mkuu kumbe inawezekana nilichoandika kiko sahihi,sasa ni kwanini unaniambia napotosha?Kama unaona kuna huo uwezekano wa hawa viumbe kuwepo,ni kwanini usisisitize watu waendelee kutafiti zaidi na badala yake unawaambia kuwa waache? Kwanini unataka watu waache kutafiti kitu ambacho kwa maelezo yako inawezekana kipo?

Hapo juu nimeonesha uwezekano wa kuwepo kwa malengo hasi ya hawa viumbe kwa uwepo wa binadamu hapa duniani kitu ambacho ni hatari kwetu na sisi kujua uwepo wao kutatufanya tuwe katika mazingira mazuri angalau ya kukabiliana nao kuliko kukaa tu na kuamini hawapo halafu ukute wapo halafu kesho watumalize kizuzu.unapotuambia tuachane nao unataka tuje tuangamie kijinga tu? [kama wapo]

3;Hkuna aliyesema wanasayansi ni malaika au watu fulani special sana kiasi kwamba tuwachukulie kwa namna tofauti.Ninajua ni wanadamu,lakini kwao kuwa wanadamu haimaanishi tudharau kila wanachotuambia.Tupo hapa leo kutokana na tafiti mbali mbali za watu hawa hivyo ni wa muhimu sana kwetu.Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni kwamba kuna watu wanajiona wao wanaelewa sana mambo kwasababu tu wamekutana na uzoefu fulani fulani maeneo mbali mbali duniani na kujiona wamemaliza....

Brother/Sister JF inakusanya watu wa aina tofauti tofauti sana,humu hatujuani hivyo hujui hata mimi ni nani na ninajishughulisha na nini,kuanza kudhani tu kuwa ninaamini kila kinachoandikwa mtandaoni ni kuona kama sifikirii kabisa kitu ambacho siyo sahihi kabisa.Wewe kuwahi kuandika uzushi kuhusu Aliens hakufanyi Aliens wasiwepo au kuwepo.Unachodhani sikijui hujui kama sikijui na unachodhani sijawahi kukifanya hujui kama sijawahi kukifanya hivyo kuwa makini unapokuwa unajibu jambo lolote hapa JF kwakuwa hujui unajibizana na nani....

Acha majigambo yasiyokuwa na maana weka hoja mezani.Kama wewe ushawahi kuandika kuhusu uongo wa Aliens haimaanishi kuwa unaelewa sana kuhusu haya mambo.Mimi kuandika kuhusu Aliens hapa JF haimaanishi kuwa ninaelewa sana kuliko watu wengine bali tunajaribu kubadilishana tu uzoefu hapa kwa kuheshimiana...

La mwisho..
Naona hata hujasoma thread yote ndiyo maana umekuja na hoja ya kuwa picha nilizoweka ni fake.Ninajua kuwa nimeweka picha ambazo siyo halisi na nimelisema hilo kwenye post zangu kadhaa kwenye uzi huu hivyo ninakushangaa tu unapokuja kwa speed ya mwanga kuanza kutaka kuonesha kuwa unaelewa sana juu ya hizo picha.nimeweka hizo picha kusaidia tu watu kuelewa nimeandika kitu gani na kinahusu nini na siyo zaidi ya hapo....

Wakati mwingine jitahidi kujadili hoja na siyo viroja...

Wewe umesoma hujanielewa kumbe.
Sijasema watu waache utafiti, utafiti upo, ulikuwepo toka hujazaliwa na utaendelea kuwepo hata baada ya sisi kufariki, sema usije na specifications zako za aliens wakati unajua fika ni za uongo, kama ni za uongo kwa nini umeziweka?

Unasema wataalamu wa mambo ya anga, nitajie mtaalamu moja unayemjua ambaye alishawahi kusema kaona alien, story za watu ambazo hazina backing yoyote ile ndiyo unataka tuziamini? Haya basi na mimi niliona mnyama mwenye mwili wa simba na pembe za ng'ombe, umeamini kua ni kweli?

Unaweza jitetea ila ukweli unabaki kua uliamini hizo story hadi kuzileta hapa na picha kibao, kama ungekua huamini usingezileta maana kiukweli unajua ni za uongo, hizo random images zimetengenezwa tu, nyingine for films, nyingine 3d artists, nyingine watu ka mimi tu tunaedit kwa kujifurahisha.

Ungekuja na reasoning mfano the universe is too big, sayari nyingi zinazidi kupatikana ambazo zipo kwenye habitable zone kwenye star system zao, hiyo yaweza kua moja ya vitu vikasababisha uwepo wa viumbe wengine, ila siyo reasoning yako kua chizi moja kasema alipaa akaondoka na alien sijui wapi, hehehe!
Sorry man ila hujaja na hoja za kisomi, umekuja na conspiracy kujaribu kuback up your claim, so nitakupa 5% for trying.
 
Eiyer shukrani Kwa kuleta kitu fikirishi Kwa bongo zetu. Kabla sijaanza kuchangia naomba majibu ya maswali haya
1,umesema hao alliance baadhi yao wanafanana na binadamu,how about kufa je nao wanakufa kama binadamu?
2:kama wana akili na utashi vipi kuhusu imani/Mungu wanaamini uwepo wake?
3;kwa kuwa kila kitu kina chanzo/nature,vipi kuhusu asili yao?3
3;Kama hao viumbe wanaakili more than human je mataifa makubwa ambayo yanatishana kila siku hawawezi kuwatumia hawa viumbe katika kushambuliana badala kuunda silaha za nuclear? Nikipata majibu nitajua kwa kuanzia.Asante
 
Kabla ya kusoma / kuandika kuhusu Aliens ningewashauri watu wajiulize maswali haya

What is Alien...?

What is life....?

What is interagency..?

What's are necessary conditions for life to exist....?

Which are credible source to study about Aliens...?

Otherwise tutalishana "Hoax+conspiracy + wishful thoughts +believes "
 
ndio hivyo mkuu Graph wengi wape, mada kama hizi tumetoka nazo mbali na zinatupa tafakari fulan hivi kuhusu ulimwengu ulivyo. hata km ni uongo haidhuru kwani napungukiwa nini? siasa mapenzi michezo na umbea vinafaida gani kwani? bora uongo huu!.
 
Haina haja, watu wanapenda kuambiwa wanachotaka kusikia, ukiwaaambia tofauti hata kama ni facts hawataki kuamini kwa kua wanapenda kuwa kwenye bubble yao waliyoizoea, kutoka nje ni kazi sana.
Hicho wanachotaka kusikia kinatengenezwa kwa hoja zenye mashiko ziwe za uongo au za ukweli kama huna uwezo huo unapata wapi mandate ya kukataa alichoandika mwenzio bila hoja mbadala? Jitathimini. Uje na uzi wako wenye hoja mbadala tutacoment, hoja hujibiwa kwa hoja mbadala sio vioja
 
Nikija na hoja huwezi elewa, hoja ni scientific, kama ungekua na scientific mind hata kidogo ungejua kabisa alichoandika hapa sicho. Zipo post nyingine hapa hapa JF zinazoongelea same thing ila zimebase kwenye science na sio story za uongo. Kama jamaa alivyosema hapo juu wengi wape, society yetu siku hizi watu mnajali sana feelings zenu kuliko facts, sasa ngoja nikuache, endelea kumeza huu ujinga, hata hivyo haisaidii chochote, usijejaza tu watoto wako upuuzi ukawa unaendeleza generation za wanaoamini maduduwasha, tunahitaji wanasayansi wanaojielewa sio imbeciles.
 
Wewe umesoma hujanielewa kumbe.
Sijasema watu waache utafiti, utafiti upo, ulikuwepo toka hujazaliwa na utaendelea kuwepo hata baada ya sisi kufariki, sema usije na specifications zako za aliens wakati unajua fika ni za uongo, kama ni za uongo kwa nini umeziweka?
Naona sasa umebadilika tena unadai ni uongo,basi sawa mkuu ni uongo...
Unasema wataalamu wa mambo ya anga, nitajie mtaalamu moja unayemjua ambaye alishawahi kusema kaona alien, story za watu ambazo hazina backing yoyote ile ndiyo unataka tuziamini? Haya basi na mimi niliona mnyama mwenye mwili wa simba na pembe za ng'ombe, umeamini kua ni kweli?
Kuna mahali nimesema unachodai hapa? Hivi unaelewa ninayoandika kweli mkuu au umeamua tu kuja hapa kujaza sever za JF bila sababu ya msingi?

Kama unahitaji kujifunza,kwenye makala yangu nimetaja mambo mengi sana,kama unahitaji jina nenda kasome upya....
Unaweza jitetea ila ukweli unabaki kua uliamini hizo story hadi kuzileta hapa na picha kibao, kama ungekua huamini usingezileta maana kiukweli unajua ni za uongo, hizo random images zimetengenezwa tu, nyingine for films, nyingine 3d artists, nyingine watu ka mimi tu tunaedit kwa kujifurahisha.
Nimeshasema lengo la mimi kuweka picha na litabaki kuwa ni hilo hilo,haya mengine na maneno yako yasiyokuwa na mshiko nitakuachia wewe mwenyewe mkuu...

Naona una tatizo la kuelewa au unataka tu kubishana hata kwenye mambo yasiyokuwa na msingi.Kama nimesema lengo la kuleta picha halafu wewe unag'ang'a nia habari za kuamini picha si kupotezeana wakati huko mkuu?
Ungekuja na reasoning mfano the universe is too big, sayari nyingi zinazidi kupatikana ambazo zipo kwenye habitable zone kwenye star system zao, hiyo yaweza kua moja ya vitu vikasababisha uwepo wa viumbe wengine, ila siyo reasoning yako kua chizi moja kasema alipaa akaondoka na alien sijui wapi, hehehe!
Sorry man ila hujaja na hoja za kisomi, umekuja na conspiracy kujaribu kuback up your claim, so nitakupa 5% for trying.
Msingi wa nilichoandika hujakielewa,naona unataka ubishe tu labda unataka uonekane na wewe unaelewa haya mambo lakini ulichokiandika hapa hata hiyo reasoning hakina,sasa sijui ni reasoning gani unayoisema mkuu....

Nikutakie kila la kheri mkuu....
 
Asante kwa Uzi hawa viumbe wanaeasiliana na binadamu kwa Njia IPI na kwa lugha IPI?
 
Mkuu Eiyer kun wakati uliahidi kuleta mtiririko wa jinsi hivi vyama vya siri vilivyoanza na mlengo yao, ndhani ndio wakati huu sasa na ningeomba kama hautajali ile mwanzo sura ya 3 na 6 maelezo yke kidogo.
Mkuu,hii ni mada inayojitegemea na itakuwa na nengi kuhusu masuala haya....

Tuombeane uzima tu mkuu ili tuweze kupata afya njema na wakati wa kuandika haya mambo vyema....
 
Nikija na hoja huwezi elewa, hoja ni scientific, kama ungekua na scientific mind hata kidogo ungejua kabisa alichoandika hapa sicho. Zipo post nyingine hapa hapa JF zinazoongelea same thing ila zimebase kwenye science na sio story za uongo. Kama jamaa alivyosema hapo juu wengi wape, society yetu siku hizi watu mnajali sana feelings zenu kuliko facts, sasa ngoja nikuache, endelea kumeza huu ujinga, hata hivyo haisaidii chochote, usijejaza tu watoto wako upuuzi ukawa unaendeleza generation za wanaoamini maduduwasha, tunahitaji wanasayansi wanaojielewa sio imbeciles.
Unashindwa nini kuweka hizo scientific arguments ili zioneshe utofauti wa hizi personal feelings na sisi tu comment, anzisha uzi ndugu kuuelewa na kutouelewa itabaki kwangu otherwise achana na huu uzi kama hutuwekei hizo scientific arguments ziache hizi personal feelings ziendelee kutamalaki hapa Jf.
 
Eiyer shukrani Kwa kuleta kitu fikirishi Kwa bongo zetu. Kabla sijaanza kuchangia naomba majibu ya maswali haya
1,umesema hao alliance baadhi yao wanafanana na binadamu,how about kufa je nao wanakufa kama binadamu?
Niliwahi kuangalia documentary moja kulikuwa na mtaalam mmoja wa masuala ya anga na miamba anasema kwamba hawa Aliens wanaweza kuishi miaka zaidi ya 2000.Sikumbuki haswa ilikuwa ni documentary ipi lakini nikiikumbuka nitaiangalia upya na kucherki upya juu ya hili kisha tutashea.Nimeshaangalia na kusoma mengi sana mkuu hadi mengine niyatafute...
2:kama wana akili na utashi vipi kuhusu imani/Mungu wanaamini uwepo wake?
Hawa viumbe sijawahi kusikia kuhusu wao kuwa na imani mkuu wangu...
3;kwa kuwa kila kitu kina chanzo/nature,vipi kuhusu asili yao?3
Chanzo chao hakijulikani mkuu,watafiti wote hawajaweka jambo hili wazi isipokuwa kuna nadharia nyingi sana kuhusu chanzo chao...
3;Kama hao viumbe wanaakili more than human je mataifa makubwa ambayo yanatishana kila siku hawawezi kuwatumia hawa viumbe katika kushambuliana badala kuunda silaha za nuclear? Nikipata majibu nitajua kwa kuanzia.Asante
Kama umesoma makala hapo juu nimesema kwamba hawa viumbe wanashirikiana na serikali karibia zote kubwa hapa duniani.Nikuambie tu kuwa pia kwenye hayo matishano na majigambo baina ya hizi serikali za dunia kune mengi wengi wasiyoyajua....

Kwangu mimi sioni kama kuna ugomvi wowote ule mkuu.Nikitaka kuanza kuelezea hili nitaanza kutoka nje ya mada na nitaelezea mambo mengine ambayo siyo wakati wake huu,lakini ukweli ninaouona ni huo mkuu kuwa hakuna cha ugomviwowote baina ya nchi kubwa duniani bali ni kuwahadaa watu tu....
 
Back
Top Bottom