Kiongozi twende taratibu sasa,naona unaelekea kunielewa.Nimekwambia urejee misingi ya sayansi ili ujue ni yapi mapungufu ya sayansi na usiendelee kujadili matokeo ya sayansi sababu mafikio yako yatakuwa ni kubebeshwa uongo ulio mwepesi na kushindwa kuujua uongo huo.Misingi ndio asasi ya kujua hatima ya jambo husika,misingi imara huleta natija madhubuti.Sayansi siikubali hasa sayansi ya mambo ya anga kutokana na misingi yake.Natilia mkazo urejeetena na tena kwenye misingi ya sayansi ili ujue uozo wa sayansi.
Nilikuuliza kwamba,kwako wewe sayansi ni uongo yote au kuna mambo inasema kweli?
Sijaona mahali umejibu hili swali....
Maelezo yangu kamwe hayapingani na ukiona yanapingana basi tambua kuna mambo mawili juu yako.
1.Kwanza ituhumu akili ya kuwa imeshindwa kuyadiriki mawazo na kuyaelewa ndio maana ukafikia hitimisho la kusema ya kuwa yana kinzana.Hapa naweza kukupa mfano juu ya kauli kwayo kwa uelewa mdogo utaweza kusema ya kuwa kauli hizi zina kinzana.Tazama kwa makini kauli hizi.
a) Nilijifunza shari niijue ili nisifanye shari na
b) Haifai mtu kujifunza kufanya mambo maovu.
Mwenye uchache wa kufikiri na kung'amua mambo hapo lazima atasema kauli hizi mbili zinakinzana.Swali la msingi litakuja ni wapi zinakinzana kauli hizo.Tusipende mteremko lazima tuzishughulishe kauli zetu.
1;Siyo kweli kuwa napaswa kuituhumu akili yangu kwasababu tu ya kutoyaelewa maelezo yako nitakueleza hili nikiwa najibu maelezo yako hapa chini....
2;Mfano wako pia siyo sahihi na hili linaendelea kuonesha shida kwenye tafakari yako..
Kujifunza jambo ili ulielewe siyo sawa na kujifunza ili ulifanye.Kinachotofautisha hayo mawili ni dhumuni la kujifunza na sentensi yako ya pili inakataza dhumuni la kujifunza jambo ili ulifanye na siyo kwamba unakatazwa kujifunza jambo kwa ujumla wakeHii ndiyo tofauti iliyoko kwenye mfano wako...
Wewe ulichokisema ni tofauti na hiki.Nakubali kwamba ukikagua msingi wa kitu unaweza kujia tatizo la kitu hicho lakini hili linategemea na muundo wa hoja na muktadha mzima wa jambo lenyewe...
Kama jambo ni uongo kwa ujumla wake itakuiwa sahihi kurejea misingi yake lakini kama siyo uongo lote misingi haiwezi kukusaidia chochote,hapa rejea swali langu kwako kama unaamini [sijatumia neno amini kwa bahati mbaya] sayansi yote ni uongo au inadanganya kwenye baadhi ya maeneo tu....
2.Pili kuona kwako kauli zangu kama zinakinzana,lazima uituhumu elimu yako kuwa haina uwezo kung'amua mawazo yangu au hoja nilizo zihudhurisha hapo juu.
Hapana,jambo kutokueleweka linakuwa na mambo mawili...
1;Mtoa maelezo kuhusu jambo haeleweki
2;Anayesikiliza maelezo hana uwezo wa kuelewa
Hapa ninachokiona mimi ni tatizo la kwanza na linaongezewa nguvu na kauli yako ya kudhani moja kwa moja kuwa mimi ndiye mqwenye tatizo na siyo wewe.Nasema hivi kwasababu mtu yoyote mwenye tafakari hawezi kujihesabia haki kwanza isipokuwa anaweka nafasi ya kukosolewa [room of doubt] kwasababu anajua uwezekano wa yeye kutokuwa sahihi upo....
Wewe hujafanya hivi,unanirushia tu tuhuma japokuwa nakuonesha mara nyingi tu namna unavyokosea kwenye maelezo yako bila wewe kuonesha ni namna ipi hukosei....
Jaribu kuangalia upya kiongozi...