Dunia haieleweki, maisha hayaeleweki

Dunia haieleweki, maisha hayaeleweki

Jeremiah Stephin

Senior Member
Joined
Feb 6, 2014
Posts
129
Reaction score
166
1. Maisha ya kwenye Ndoto ukiwa umesinzia si halisi,ila utagundua si halisi pale utakapo zinduka kutoka usingizini.Ndoto ni Illusional..unadanganywa.

2. Video games kama zile za FIFA,GTA n.k wahusika wa kwenye zile games mfano unacheza PS5 kuna muda wachezaji wanalalamika,wanaumia,wanahuzunika na Kushangilia ila hawajui kwamba kila wanachokifanya ni Program,wao ni program ya computer inayo chezeshwa na binadamu.

3. Kwa Kuzingatia 1 na 2 hapo juu nashawishika kwamba hata sisi binadamu na viumbe wengine kwenye huu ulimwengu Tunaishi maisha yasiyo na uhalisia..tunaishi maisha danganyifu kama wale wachezaji wa kwenye PS au yale maisha ya ndoto.

4. Kila tunachokiona sio halisi(illusional) na maisha yote ni kama simulation za games..Sisi tupo kwenye Program inayoendeshwa na aliyeiunda.Maisha yetu ni program ndio maana hayaeleweki.

5. Tunazaliwa Then Tunakufa bila kujua hata lengo la kuwepo duniani ni lipi(achana na falsafa za dini).Magonjwa,Vita na kila uharibifu unaofanyika ni sehemu ya simulation za mcheza game..

6. Mwisho wa haya maisha ni pale anayetuchezesha Game Akiacha kucheza au akashindwa kuendesha program yake vizuri. #Ongeza na wewe
7.
8.
 
Ukitumia hoja yake ya 1 na 2 kama kueleleza kielelezo cha maisha yetu ndugu itakuwa umepotea sana!, vipo vitu vingi sana tunatofautiana na huo ulimwengu unaojaribu kuulezea!. ni ulimwengu usiokuwa na hisia na si halisia!. maisha yetu halisi yamegubikwa na kanuni zake ambazo ukizivunja utavunjika ama zitakudhuru moja kwa moja!.. mfano katuni kwenye game hawezi kula na wala sio shida zake na wala hapambanii kuishi!!.
Kiufupi niseme umetumia mfano mbaya sana katika kuangalia uhalisia wetu!.

Kutoyaelewa maisha haimanishi ya kwamba tupo program vilevile kuyaelewa maisha haimanishi tuwe au tusiwe kwenye program!.
yani kuwa program ama kutokuwa yote yanawezekana!, sema bado hatuna majibu ndio tunaweza kuchagua jibu lolote ila sio kwamba jibu halipo ni vile hatujalivumbua tu!.

Nadharia yako ya kuwa tunachezeshwa unaweza kuithibitisha ama unafuata hisia zako ktk kuwaza tu..?
 
Wewe umepata uwezo wa kufikiria kuhusu maisha yako. You mean hata zile cartoons kwenye games na zenyewe sometimes zinakaa chini na kuwaza kama unavowaza wewe?

Basi huyochezesha game wetu kiboko yaani hapumziki. Maana hizo play station unacheza mwisho unaacha unaendelea wakati mwingine.
 
Human beings are trapped in illusional World
Everything we experience through the senses appears real… yet it ...
 
hakuna illusionary (udanganyifu), kila kitu ni halisi katika mtazamo wa kitu chenyewe. hakuna anaetuchezesha ila ni ufahamu wenyewe unaojichezesha. kwa macho ya kawaida inaonekana kua sisi tupo, ila kiuhalisia hatupo na hata ulimwengu wenyewe haupo ila ni ufahamu unaojionyesha katika miili tofauti na hii ni kwa sababu kitu pekee ambacho kinaweza kua, ni ufahamu tu
 
hakuna illusionary (udanganyifu), kila kitu ni halisi katika mtazamo wa kitu chenyewe. hakuna anaetuchezesha ila ni ufahamu wenyewe unaojichezesha. kwa macho ya kawaida inaonekana kua sisi tupo, ila kiuhalisia hatupo na hata ulimwengu wenyewe haupo ila ni ufahamu unaojionyesha katika miili tofauti na hii ni kwa sababu kitu pekee ambacho kinaweza kua, ni ufaham

hakuna illusionary (udanganyifu), kila kitu ni halisi katika mtazamo wa kitu chenyewe. hakuna anaetuchezesha ila ni ufahamu wenyewe unaojichezesha. kwa macho ya kawaida inaonekana kua sisi tupo, ila kiuhalisia hatupo na hata ulimwengu wenyewe haupo ila ni ufahamu unaojionyesha katika miili tofauti na hii ni kwa sababu kitu pekee ambacho kinaweza kua, ni ufahamu tu
Mkuu ulicho andikq hakina tofauti sana na nilicho maanisha mimi ha
 
Udhibitisho wa huu mchezo ni kuwepo kwa coincidence na synchronicity events.

Mfano 1.
umesafiri safari ya mbali, mji uliofikia unakutana na rafiki yako wa zamani sana wote mnabaki mnashangaa imekuaje! Kilichotokea ni mwenye mchezo kawakutanisha aone reaction yenu au kuna kitu anataka mfanye pamoja.

Mfano 2.
Mzunguko wa Mwezi kuendana na mzunguko wa hedhi, au ukubwa wa Mwezi na umbali kutoka lilipo Jua kuwa katika kiwango kinacholeta kupwatwa kwa jua! Kubwa zaidi tupo wenyewe kwenye ulimwengu mzima!

Na endapo kama hatupo kwenye Matrix basi hii sehemu tuliopo ndio Kuzimu kwenyewe kwani hakuna jambo unaweza fanya ukaridhika. Mfano ukila baadae utataka tena, ukijamiana badae tena, ata ukisali Leo kesho utataka tena kuomba.
 
Haya tunayoita "mafanikio" ni pale mtu anapokuwa na vitu dhidi ya wengine ,hapo anajiona amefanikiwa..Mtu akifaulu sana kuzidi wengine kwenye mtihani basi anaitwa amefanikiwa ,akiwa na pesa kuliko wengine vivyo hivyo...Ikitikea mashindani ,mtu akishinda anjiona ana mafanikio.

Kiufupi ,hakuna uhalisia mafanikio yanategemea na wengine kuanguka au kuwa chini yetu...Ebu tujiulize ,mawazo ya mgonjwa aliyekuwa mahututi ni yapi ? Anafikiria zaidi mafanikio ya duniani kama yale anayofuatilia kila siku au anafikiria zaidi kuhusu hatma ya afya yake?

Kuna muda ,utaona mambo ya duniani hayana uhalisia ila tulipanga sisi tuishi vipi.
 
Maisha ni magumu kwakuwa kila mtu anatoka katika nyumba na makuzi tofauti.

Laiti kama wote tungekuwa tunaishi nyumba moja kuubwa hali ingekuwa tofauti.

Ukiondoa hiyo tofauti bado unaweza enjoy maisha ukitaka.
 
Haya tunayoita "mafanikio" ni pale mtu anapokuwa na vitu dhidi ya wengine ,hapo anajiona amefanikiwa..Mtu akifaulu sana kuzidi wengine kwenye mtihani basi anaitwa amefanikiwa ,akiwa na pesa kuliko wengine vivyo hivyo...Ikitikea mashindani ,mtu akishinda anjiona ana mafanikio.

Kiufupi ,hakuna uhalisia mafanikio yanategemea na wengine kuanguka au kuwa chini yetu...Ebu tujiulize ,mawazo ya mgonjwa aliyekuwa mahututi ni yapi ? Anafikiria zaidi mafanikio ya duniani kama yale anayofuatilia kila siku au anafikiria zaidi kuhusu hatma ya afya yake?

Kuna muda ,utaona mambo ya duniani hayana uhalisia ila tulipanga sisi tuishi vipi.
Fact sana
 
Back
Top Bottom