Mkuu
Eiyer kwanza lazima nikuambie ukweli, mimi ni mmoja kati ya watu ninao kuheshimu sana, na kuheshimu mawazo yako, huwa ninapoona bandiko lako popote lazima nilisome kwa umakini maana najua lazima kutakua na nondo. Salute mkuu.
sasa tuje kwenye mada.
nimesoma hili bandiko lako kwa umakini, ila kuna vitu vinaonekana vinapingana vyenyewe au laba mimi kuna mahali unaniacha.
kwanza wakati unaelezea hiyo kuiper belt, kwa maelezo yako ni kwamba ni "vimawe ambavyo ni kama barafu au vinauwezekano wa kuwa na barafu" kwa jinsi unavyosema ni kitu ambavyo hata hao wataalamu hawana ukakika navyo, hawajui kama ni barafu kabisa au vina hali ya ubarafu kwa asilimia fulani. na pia wanahisi/wanadhani kuwa kuna uwezekano wa kuwa na uhai. Hawana uhakika sana labda pengine hawajawahi kufika au kukaribia eneo hilo.
Lakini kitu cha kustaajabisha sana ni kuwa wameweza kueleza kwa ufasaha sana vitu vinavyoishi ndani ya hiyo kuiper belt, hadi kufikia ku-categorize aina ya hao aliens na tabia zao hadi mission zao na jinsi wanavyotuchukulia sisi.
kila aina na mipango iliyonayo kuhusu binadamu, as if kama hao wataalamu walikaa meza moja na hao aliens na kupia story.
Sasa inakua vigumu kidogo mtu kuelewa kwa kweli maana kama huo ukanda tu bado hawaujui kwa asilimia mia unawezaje kujua kilichopo ndani yake na kukielezea kwa ufasaha namna hiyo.
kwa mafano mtu ameona nyumba kwa mbali na kwa sababu ya umbali hawezi kujua rangi ya bati la hiyo nyumba kuwa ni blue au kijani, lakini hapo hapo anakuelezea kwa ufasaha kuhusu mazingira ya ndani ya nyumba jinsi yalivyo.
inakua na ukakasi sana kuelewa