Wewe umesoma hujanielewa kumbe.
Sijasema watu waache utafiti, utafiti upo, ulikuwepo toka hujazaliwa na utaendelea kuwepo hata baada ya sisi kufariki, sema usije na specifications zako za aliens wakati unajua fika ni za uongo, kama ni za uongo kwa nini umeziweka?
Unasema wataalamu wa mambo ya anga, nitajie mtaalamu moja unayemjua ambaye alishawahi kusema kaona alien, story za watu ambazo hazina backing yoyote ile ndiyo unataka tuziamini? Haya basi na mimi niliona mnyama mwenye mwili wa simba na pembe za ng'ombe, umeamini kua ni kweli?
Unaweza jitetea ila ukweli unabaki kua uliamini hizo story hadi kuzileta hapa na picha kibao, kama ungekua huamini usingezileta maana kiukweli unajua ni za uongo, hizo random images zimetengenezwa tu, nyingine for films, nyingine 3d artists, nyingine watu ka mimi tu tunaedit kwa kujifurahisha.
Ungekuja na reasoning mfano the universe is too big, sayari nyingi zinazidi kupatikana ambazo zipo kwenye habitable zone kwenye star system zao, hiyo yaweza kua moja ya vitu vikasababisha uwepo wa viumbe wengine, ila siyo reasoning yako kua chizi moja kasema alipaa akaondoka na alien sijui wapi, hehehe!
Sorry man ila hujaja na hoja za kisomi, umekuja na conspiracy kujaribu kuback up your claim, so nitakupa 5% for trying.