Yale maandishi ya Mwakyembe yalikuwa ni miongoni mwa simulizi tamu tu hakuna lolote la maana! Kama sikosei, taarifa iliwataja Mwakyembe, Sitta, Membe, Mengi, Mwandosya, Slaa na Mama Malecela.Haya nisaidie wewe; tuseme zile zilikuwa ni njama za serikali ya JK kutaka kuwanyamazisha wanaoisakama serikali. Au, karibu na hilo, tuseme zilikuwa ni njama za RA! Sasa je, hapo Membe na Mwandosya waliingia vp kwenye hiyo list?! Ni lini Membe au Mwandosya wamewahi kuishutumu serikali au RA hadharani?! Ni lini JK au RA wamepata kuwa adui wa Membe kiasi cha kutaka kumtumia Al Shabab?! Au tangu lini Al Shabab wakatumiwa kuua watu?! Al Shabab ni kundi la kigaidi na wala sio snipers wa kukodiwa!! Lakini Mwakyembe alifanya makusudi kuwaweka Al Shabab ili ionekane kinachotaka kufanyika hapo ni udini; waislamu against wakristo!!!!Ile taarifa aliitunga Mwakyembe ili kumuharibia Membe na kumfagilia njia mnyakyusa mwenzake Mwandosya! Ndani ya CCM kuna wapuuzi wengi tu wanaoongelea ukanda huku wengi wao wakionekana kutoridhishwa na urais kwenda kanda ya pwani misimu yote mitatu mfululizo. Alichotaka kukifanya Mwakyembe ni kuonesha kwamba waislamu wa CCM/waislamu wa serikali ya JK wanatumia Al Shabab(waislamu wenzao) kutaka kuua viongozi wakristo wanaotarajiwa kugombea urais wa nchi hii. Sumu hii endapo ingefanikiwa, ingeleta mgongano wa kimaslahi kati ya wana CCM wakristo na wale waislamu ambao wengi wao wapo pwani/mashariki ya tz. Kv waislamu wengi wanatoka east TZ, wakristo wa bara wangeacha kutofautisha kati ya mkristo na mtu wa pwani kwa kuona ili mradi wapo pwani, basi ni walewale tu! Bila shaka, hii ingewafanya wakristo wengi wa bara kumpigia Mwandosya baada ya kukosa imani na wakristo wenzao wa pwani, ambao angekuwa ni Membe! Likewise, simulizi ile ililenga kumfanya Membe asimwani JK na akishakosa kumwamini basi bila shaka angejitenga nae. Kujitenga huko kungemaanisha Membe kujitenga vilevile na uungwaji mkono toka kwa wapambe wa JK.....hilo lingefanikiwa, nalo lingeendelea kumweka Mwandoysa close na wapiga kura wa CCM! Kama kuna mtu hodari wa kucheza na akili za watu ni mwakyembe, hivyo kuwaweka akina Mengi, Anna Kilango na wengine ilikuwa ni danganya toto tu ya kuficha nia yake! Unfortunately, wenye akili zao wakashitukia kwani michezo kama hiyo ni mambo ya kawaida sana katika masuala ya ujasusi!!! Hushangai, Mwakyembe ni mwanasheria aliyebobea; na ukisoma riwaya ile utakuta mshikaji alikuwa na ushahidi wote wa kuwafikisha korokoroni wahusika!! Kwanini basi asingefungua jalada mahakamani?! guys, acheni kuchezewa akili na hawa manipulating politicians!!