Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,261
Kwanini tukuamini jason?...bado hujanikomvisi...
u are one in a million. U add or change notin'
Kwanini tukuamini jason?...bado hujanikomvisi...
Nawashukuru sana wapiganaji wenzangu muhimu wa jf kwa kuukubali uchunguzi wangu japo kutofautia kifkra ndilo jambo jema ktk dunia hii!
Una akili sana wewehii itachomolewa ghafla humu na mods baada ya mkwara mzito! Subirini muone,nikifika hm naisave kabisaaa!
Hekaya za Abunuwasi, hivi Mwandosya ana usafi gani? hakuna wa kumuua ila dhambi zake za kutafuna pesa za miradi ya maji vijijini na kuwaacha akina mama wa same wakiendelea kuchota maji kwa ndoo na kutembea umbali mrefu ndoo zikiwa kichwani. Haihitaji huruma huyu, adhabu aipatayo inamtosha. Mkuu uliyefanya uchunguzi, pitia upya vielelezo vyako, wengine humo wanachomekwa tu!
Sasa kama rais JK ameamua ''kuwapumzisha'' watanzania wenzake kwa sababu ya kuwa na mitazamo tofauti kwanini aliwateua kuwa mawaziri?
Sasa wakishauawa ndo inakuwaje? Hajui kwamba wataibuka wengine? Hii tabia ni mbaya sana, si ajabu akahamia JF akishawamaliza walioko kwenye list yake ya sasahivi.
kwa kifupi ni kwamba hujui unachokiongea...hujui LTK ni nini...hujui LTK wana mafungamanao gani na IKULU+ TISS, huwajui KGB...na pia hujui uwezo wa TISS...
wadau nijibuni swali langu kuhusu huyo mtu hapo kwenye red.mkuu samahani huyu jamaa-Exaveri H.Limo naona umem-rank kama jasus mashuhuri nchini.umeshuhuri wake ulitokana oparation gani alizofanikisha kwa maslahi ya taifa?hata mataifa mengine yana mashujaa wake wa kijasus na michango yao inaheshimiwa.
We unahitaji msaada, sasa ukianza kuamini kwa kuangalia signature hata hiyo ripoti hutaisoma maana muandishi ni Jason Bourne si ni picha hiyo? Ni hivi mi najaribu kusema kulingana na kilichowasilishwa kwenye ripoti. "Mtunzi" ameonesha kama LTK ni kundi na lina kiongozi wake, wakati sio kweli hao labda ni majambazi tu...LTK kwa level ya nchi yetu inatoka kwa Rais pekee kisheria ndo maana hata adhabu ya kifo lazima ipate GO AHEAD yake. Na sio kama alivyoweka yeye maana hao wahusika hawapo katika list ya watu hatari katika nchi hii sasa iweje wawekewe notisi ya kifo? Mbona yule Jasusi Kombe aliuwawa kiubua tu, klichofanyika ni kuiomba radhi familia yake mchezo ukaisha, huyo Mwakyembe kawa Jasusi lini hadi akwepe mitego ya akili 16? So unreal kwa kweli.
Sisemi kama ripoti ni sahihi au sio sahihi, isipokuwa:
1. Unajuaje kama LTK haijapewa go ahead na rais? Yaani unaona hili linashindikana? Wewe unafikiri rais wako ana uchungu na nchi labda kama alivyokuwa George Bush au Obama kwa Marekani? Yaani kama mtu anaweza kukutengenezea scandal na kukusokomeza jela kwa sababu mnagombania mwanamke atashindwa kufanya hili? Swali ni kwamba wewe umemwona huyo rais wako kuwa yuko makini kiasi cha kushindwa kufanya haya yaliyoandikwa?
2. Unaposema wahusika hawako katika list ya watu hatari katika nchi una maana gani? Kwa sababu hao watu ndio wanaoumbua magamba na serikali yake, uhatari wao ni kuhatarisha maslahi ya mafisadi, sasa hapo unashindwa kuelewa nini? Ni mara ngapi wahusika wenyewe wamedai kwamba wanataka kuuawa? Sasa kwa taarifa yako ni kwamba serikali hii ya Tz ya kifisadi adui zake ni watu wanaoumbua ufisadi au kuikosoa sana serikali au wakionekana wako kinyume na mtizamo wa serikali, kiujumla wanapopingana na maslahi ya mafisadi na ndio wenye uchungu na nchi. Rejea nyuma Sokoine aliuawa kwa nn? Na akina nani walipanga? Kwa nini Kolimba alikufa? Vifo vya utata vya akina chifupa? Viongozi wangapi Tz wanaopingana na ufisadi wametegwa ajali? Hujui? Akina Mrema walidai kufuatiliwa kutaka kuuawa! Hukusikia?
3. Unasema Kombe aliuawa kiubua, sasa huyo si walikuwa na sababu kwamba alivujisha siri za ndani za nchi? Kwa hiyo unataka wamuue Mwakyembe hadharani kama huyo halafua wakuambie tumemuua kwa sababu anapingana/anaumbua ufisadi?
4. Kama wewe unaona serikali yetu haiwezi kufanya huo upupu ingekuwa safi basi? Lakini mbona imejaa wezi, walaghai na wauaji! Wasingekuwa hivyo kungekuwa na kashfa zote hizi mpaka nyingine za waziwazi?
5. Jenerali alisema kama kuna dhambi ambayo haiwakilishwi ndani ya CCM hiyo dhambi bado haijashuka! Mara ngapi Tz umesikia mke au mme anamuua mwenzi wake kwa makosa madogo tu sana? Sasa kama mauaji yanawezekana kwa watu ambao tunadhani wanapendana, yaani wewe unaona serikali ya Magamba inashindwa kuua mtu yeyote anayezuia au kupinga maslahi yake ya kifisadi?
6. Hii serikali haina aibu! Mie nikuhabarishe, inafuata watu wengine tena ni wadogo sana, mpaka unajiuliza sasa kwa nini itumie nguvu nyingi kupambana na mtu kama huyu? Labda wakikusimlia ndio utaelewa! Nani amekuambia hii ni serikali ya haki? Kumbuka wale wachimba madini wa Moro ambao hawakuwa wanapingana na ufisadi wowote lakinia walikuwa busy na shughuli zao, walipigwa risasi kwa kisingizio kuwa ni majambazi na watu ambao walitakiwa wawalinde! Wakachukua zao hela wakatoweka. Nina mengi ya kuongea lakini sina muda.