Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NYAGI DRY, Oct 10, 2011.

 1. N

  NYAGI DRY JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Tuhuma za kuuawa kwa Mwakyembe na wenzake kwa IGP na Mwandishi wetu FEBRUARI 8, mwaka huu, Dk. Mwakyembe alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

  Baada ya maelezo hayo, polisi walimtaka aweke madai yake kwenye maandishi na siku moja baadaye Dk. Mwakyembe aliwasilisha taarifa yake ya maandishi.

  Dk. Mwakyembe amesema kwenye barua hiyo, "Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.

  Maelezo ya Barua ya Mwakyembe "Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

  "Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea Januari 22, 2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa Januari 21, 2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 68… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 68…).

  Gari hiyo iliwateremsha "abiria" hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T7…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea. "Majina ya baadhi ya watu hao saba ni Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a "Master"; Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na mtu mwingine (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.

  "Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya (kaitaja) akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina (linahifadhiwa). Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda "kulogwa" safari hii.

  Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Willibrod), Anne Kilango - Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe. "Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyika, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.

  "Usiku wa Jumamosi Januari 22, 2011 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo, (kwa gari aina ya Defender STK 26…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga' …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve With Impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni' hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa'. Walirejea Songea Januari 29, 2011 na kesho yake Januari 30, 2011 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

  "Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T7… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo).

  Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T8… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro. "Kufuatana na ‘mganga' mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza "waliohukumiwa kifo" (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

  "Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu' hao walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: Februari 5, 2011, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili: moja ya polisi (PT 02…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

  Ushiriki wa Al Shabaab "Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al- Mujahideen (kwa kifupi Al- Shabaab). "Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini.

  Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati' wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini la Uislamu kutishiwa.

  Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu. "Niliweza vilevile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao.

  Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. "Utabiri" huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo. "Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari).

  Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu' yamefanywa: "(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi Februari 5, 2011 kwa "maandalizi" hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile ‘portion' ya mganga ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni); "(b) Kesho yake (Jumapili) Februari 6, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T3… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).

  "Waliomo kwenye kikosi hicho ni Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a "Master" na kijana mmoja ambaye Januari 19, 2011 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T6…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.

  "Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji. "Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili.

  Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi: "Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T8… AQS) Januari 8, 2011 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa polisi Morogoro. "Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life.

  Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli ya….(jina la hoteli na mmiliki tunalo). "Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T8… AQS, VX Land Cruiser STK 1…, Mercedes Benz (Station Wagon) T8… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T2… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T6… APF, Nissan Patrol T8… ADH."

  "Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata vyanzo vyangu vya habari ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.

  "Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani iko siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake wasitake, hakika ni suala la muda tu. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa taifa letu, taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.

  "Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

  "Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi' niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia Kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji."
   
 2. N

  NYAGI DRY JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  nafkir manifestation ndo hii au?
   
 3. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Fanya editing kidogo ya habari yako, uweke na paragraphs, hii inakuwa ngumu sana kuisoma mpakaa mwisho.
   
 4. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  alamsiki kaka, kilichokufanya ukaficha madudu ya serikali wakati unailipua richmond ndo matokeo yake haya kumbuka wenzio walisema 'hatukukutana barabarani' we kaa na uzalendo wako wa kinafki na huo ndio mshahara wake, alamsiki mkuu.
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi ulivyotumimia habari nyeti kiasi hiki na bila hata kupata wasaa wa kuweza kuweka sawa hili na lile kwenye taarifa yenyewe, mkuu nadhani unafanya kazi sehemu nyeti sana vile vile.

  Tunasubiri habari zaidi please ukipata tena ka-kipenyo kama huu hapa.

   
 6. D

  Derimto JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kila nafsi itaonja mauti hata akifa mwakyembe watazaliwa wengine na mwisho wenu utafika tu na kwa hili tayari linanifanya nianze kuamini ugonjwa wake siyo wa kawaida.
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ooooh,,,,halafu hii barua uchunguz wake umeshaisha au??????
   
 8. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2011
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Duh.... Tanzania hii hii...
   
 9. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  hii habari sio mpya. Nilishawahi kuisoma ktk gazeti la Mwanahalisi. Hapa ameficha baadhi ya mambo, kama namba za magari na jina la shekhe.
   
 10. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Unafiki wake unampönza. Mungu ameshaanza kumhukumu hapahapa duniani.

  Hakuna sumu wala nini, ni madhara ya unafiki wake.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwakyembe ni Mnafiki na malaya wa kisiasa, hana tofauti na Samwel Sita!
   
 12. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Eeee Mungu, Uliokoe taifa la Tanzania. Ushirikina huu na mauaji haya yatalifikisha wapi taifa letu?
   
 13. m

  mfngalo Member

  #13
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Maskini Mwakyembe 2nakuombea
  Watashindwa wote kwa jina la yesu
  Dr Slaa wasahau walijaribu wakashindwa hatataweza tena,makanisa yote yako mbele yake wamalizen wakristo ndo muende kwa x padri we2
  Hv unajua cheo cha padri na mafunzo wanayopata co hvyo iz ufikirivo
  HATUTISHIKI
  MUNGU YU MBELE YA DR SLAA,MWAKYEMBE,MEMBE,MWANDOSYA,NA KILANGO AFU ZEY A OL CHRISTIAN
  DAMU YA YESU ILIYOMWAGIKA MSALABAN ITAWAONGOZA
  Na pepo la kuwaua litashinda kwa jina la Yesu
  Glory b 2ze father,n 2ze son n 2ze holy spirity
  B blecd.
   
 14. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii habari si mpya ilishawahi kutolewa hapa jamvin lakin hata hivyo tunashukuru kwa kutukumbusha naamini ugonjwa wake hautofautiani na habari hii, hii inamaana jeshi la polisi halikufanyia kazi tuhuma hizi na wala halikumpa ulinzi unaostahili na ndo maana hali hii imemkuta. Kwa ugonjwa unaotajwa kwa kawaida mtu angalau huwa anakuwa na historia ya kupata allergy ya mtindo huo, coz source zote zinaonyesha ana exfolative dermititis kulingana na visababishi toka utotoni hadi sasa lazima angesema anahx ya allergy kama imemkuja ghafla basi yawezekana kabisa inauhusiano na hii scenario. Lakin hakuna siri chini ya jua tutajua tu. Mungu umjalie afya njema Dr Mwakyembe na Prof. Mwandosya wapone haraka waje tulijenge Taifa.
   
 15. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kama alificha baadhi ya ukweli kuhusu richmond, hastahili adhabu ya kifo hiki cha umafia.
  Tunatangaza ole kwa kifo chake.

  Ole Ole Ole.

  Ole kwa kumuua huyu. Ole kwa kumuua Dr. Slaa.
  Ole kwa kumuua MWANDOSYA. Nchi haitakalika hii.
  Mafisadi wanaleta ya Rwanda. Hapa itakuwa matajiri vs masikini
   
 16. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Kazi ipo, bado Dr.Slaa,Kilango,mengi mh..siyo mchezo.
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  TURUFU YA KUDUMU KATI YA MAFISADI NA WAPAMBANAJI NCHINI TUNAO SISI VIJANA NA KUTUMIKA KUNAKO HAJA STAHIKI - DUA NJEMA DR MWAKYEMBE!!!

  Dr Mwakyembe, ugua pole Mungu kipenda tutawaona tena hapa nyumbani pamoja na kaka yako Prof Mwandosya huku mkiwa buheri wa afya na mkipokelewa na yule ndugu yenu Prof Mwakyusa, Daktari Bingwa wa Mwlimu Nyerere enzi hizo, ambaye naye kwa mtaji wa uhuru wa mawazo yake leo hii umemfanya kusugua benchi kwa kipindi kisichojulikana kwenye serikali hii ya awamu ya nne.

  Ni kweli tunao habari kwamba wana-CCM wanaotumikia vifungo vya nje kama vile Dr Lamwai, wako wengi mno kuliko idadi ya watuhumiwa wote Keko wakiwekwa kwa pamoja. Nasema Dr Mwakyembe kwa mtaji wa kauli hizi ulizozitoa hapo chini kwe kijipande chako cha maneno kwenye barua yako kwa IGP na ukimya uliofuatia mpaka hivi leo kelele za JF ndio zikakurukisha ndege kwenda India, naamini sana kwa umeondoka na mambo mtatu mazito:

  1. Maombi binafsi kati yako wewe na Mungu wako hizo sumu zisije zikawa zimeharibu baadhi ya viungo,

  2. Siri nzito moyoni kuhusu Ma-Fisadi wa DOWANS na kona gani wanatuweka kama taifa hivi sasa,

  3. Uchungu juu ya Mafisadi kuendelea kutamalaki na kuenziwa kama Wafalme na Mashujaa nchini.

  Dr Mwakyembe, Dr Slaa, Prof Mwandosya, Mzee wetu Mpendwa Ole Sendeka, Mzee Reginald Mengi, Mama Anna Kilango, na wengine wengi mliotajwa kwenye taarifa hiyo chafu hapo juu - tunawawekeeni katika maomba bila kuchoka; na wala hamtokufa kutokana na lolote kabla ya wabaya wenu ambao pia ni wabaya wa taifa letu kutangulia kwanza.

  Tofauti hizo zoooote huko juu, TURUFU yake yote tunayo sisi vijana wenu huku Uswahilini; lakini kwa sasa ni maombi tu mjaliwe salama salmini, Amen!!!!!!!


  ..................... "Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata vyanzo vyangu vya habari ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.

  "Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani iko siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake wasitake, hakika ni suala la muda tu. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa taifa letu, taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.

  "Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

  "Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi' niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia Kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji." ................


   
 18. d

  demokrasia Member

  #18
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe ndio malaya ndio maana huna lugha yenye staha. Nafikiri umepotea njia. Hutufaikwenye jukwaa hili la wastaarabu.
   
 19. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  kuwa mkristo sio hoja..hao kwenye red ni wanafiki tu...waboreshe hospitali za kwao mbeya sio kukimbilia india
   
 20. N

  NYAGI DRY JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Acha uvivu! Niki edit haitakua poa
   
Loading...