Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

mbona mnamuhoji sana mkuu??.Kesha wambia baada ya kushauliwa ikabidi kuna mambo ayapunguze.Kwanza nazan hatumfaham huyu aliyeandaa ripot hii anahusikaje au anauhusiano gan na wahusika xaxa nyie mlitaka ataje ofisi kilipofanyikia kikao ili iweje??.
Hum hum siajab hao wahusika nao wamo na mi namashaka xana na nyie mnaouliza uliza maswali ya rejareja ili muweze kujua msariti wen nan. Hiii ndiyo jf bana zaidi ya fbi.

Point unayo angalau.
Ila lugha za ki-facebook hapa sio mahali pake,
Ma-Great Thinkers hua hawaongeagi hivyo
 
Nafikir kuna conflict of nterests hapa yaani walioileta ni wao wana uweizo wa kuzuia uchunguzi na kuhonga mahakama, so labda kelele za wananchi na mabalozi na wa wanafamilia wa waathirika ndiyo utaamua hili nafikiri wakifa prominent pipo wa3 hivi katika miaka 2 au mi3 itakua ni shida
 
Kama haya ni kweli. Mwisho wa Dunia huoooo..........
Lakin yote hay kusingiziwa kua adui wa uisilam ni kwa sababu tu ya tamaa za uongozi. Yan mtu upo radhi upoteze uhai wa mtu ili uwe kiongozi.
Waasisi wa mpango huo ndo haohao wanaopanda majukwaani kusema nchi yetu ni ya aman, umoja, nk

Kama tumefikia hapa nackitika saana

Natumain Rais anajua mpango wote pengine kwa kupewa taarifa. Leo hii kwa Mwakyembe na wenzake kesho kwake aangalie nasana.


Kumbuka asiyesikia kilio cha Mwenzake ipo cku na yeye atalia na hakuna mtu atakayemsikiliza
 
Hahahaha

Kumbe Chadema na wafuasi wao wana imani kubwa sana kwenye mambo ya uganga na ushirikina teh teh teh

Huyu aliyeleta hizi habari za magazeti ya udaku aende akaiuze kwenye magazeti ya vikatuni watu wanaweza kufurahia kule.

Eti mwakyembe,mwandosya,kilango, Membe adui wa uislam???? whaaat??

Hebu acheni kuleta habari za uchonganishi hapa!
 
Ni jambo la kushangaza sana hapa JF tunaendesha kampeni za kizushi ambazo hazina manufaa kwa nchi yetu,swala la mwakyembe kuumwa ni jambo la kawaida sana,maradhi yanayomsumbua ni siri kati ya yeye na daktari wake na familia yake,tumebaki kuwa kama ndo wasemaji wake,ni kweli baadhi ya viongozi afya zao ni mbovu ila kama akipata wasaa atatuambia maradhi yanayomsumbua ila kwa sasa tusiwe wasemaji wa familia za watu....tuache unafiki na maneno ya kuokota mitaani ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kutosha...
 
He is a hypocrite who professes what he does not believe; not he who does not practice all he wishes or approves.

Unafiki wake unampönza. Mungu ameshaanza kumhukumu hapahapa duniani.

Hakuna sumu wala nini, ni madhara ya unafiki wake.
 
Kama nilivyosema unahitaji ELIMU tena kubwa tu:

1. Hakuna kundi la kijajusi la kijajusi lenye jina LTK, hili ni neno la kisheria linalotumika kumpa mtu au maofisa wa ngazi fulani kinga wanapotekeleza operation/mission ya kinchi iwe ndani au nje ya nchi. Na kwa nchi yetu kinga hii hutolewa na Rais pekee. Sasa ni kuongopeana mtu akisema mkuu wa LTK akatoa oda ya kumuua mtu bahati mbaya mwandishi hakuonyesha kama huyo mkuu alimaanisha Rais. Hivyo nimepingana nae kwa hoja hii.

2. Mwakyembe anaweza kuwa na maadui lakini si kwa nchi yetu, definition yako ya hatari kwa mafisadi ingefaa kama ripoti ingeweka wazi kuwa waliotumika hapo ni kikundi cha kimafia na hawana affiliation na serikali....again ningehoji mafia na ujanja wao wote kamwe hawana uhusiano na Usalama wa taifa katika nchi yoyote je hawa waliowaleta KGB mafia gani? Labda hujui ngoja nikwambie hakuna ndege inaweza kuingia nchini bila jeshi kujua. Sasa kama hawa walikuja na kutua private haiingii akilini kwa kweli.

3. Hao uliowataja hawana ulinzi zaidi ya madereva wao, kama watu hao wamediriki kuwawekea sumu kwa kuwafuata maeneo husika walishindwa nini kuwa tumia majambazi au hata njia zingine kuliko hizo zilizotajwa? Wamekunywa sumu kibao bado wanadunda jamani hata sumu ya panya lazima itakufikisha hospitali vipi wenzetu wadunde tu kwa misumu ya kutisha? So fiction kwa kweli

4. Suala la Rais kuwatumia majasusi kumfanyia mtu mwingine ni la kudhania sana, upo huo uwezekano lakini si kwa hili, kwanza nahisi unahitaji elimu ya mfumo wa usalama wa taifa ila nitasamehe mi sio mahiri eneo hilo. Kifupi Rais sio mtu mmoja ni taasisi hakuna anachokifanya bila watu wengine ndani ya taasisi yake kufahamu. Na pia akiamua fulani afe wala hana haja ya kuitikisha kikao Movenpick au kuagiza sumu urusi na Bulgaria. Walipona makomandoo waliotaka kupindua nchi ndo wawe hawa.

Sitakulazimisha ufuate maoni yangu maana wapo watu wataikubali ripoti hii kwa utashi wao wa kisiasa na wengine kama sie tutaikaa kwa weledi wetu maana ripoti za aina hii ni rahisi kuona mapungufu ukiwa NEUTRAL kuliko ukilalia upande wa kushoto. kwahiyo naelewa kuwa mjadala huu unategemea sana na unaelemea upande gani, kama ule wa vidole viwili utajulikana, kama wa Nyundo na Jembe pia utajuliakana na bahati mbaya wengine tusio na upande tutawekwa huu wa Nyundo.....sitajali ila kikubwa nina asilimia MIA MOJA kuwa THIS IS NOT EVEN CLOSE TO THE TRUTH.

fiksiman unapojibu mtu soma vizuri na kuelewa halafu tumia akili.

1. Sijasema LTK ni kundi la kijasusi, Kwa mjibu wako "hili ni neno la kisheria linalotumika kumpa mtu au maofisa wa ngazi fulani kinga wanapotekeleza operation/mission ya kinchi iwe ndani au nje ya nchi", LTK ni kifupi "acronym" ya "License To Kill", kwa mujibu wa mwandishi ametumia neno LTK kama kundi lilopewa ruhusu ya kuua, na mahali pengine ametumia hilo neno akimaanisha mtu aliyepewa ruhusa ya kuua alipoandika kwa mfano LTK/DBK (huu ni mfano tu). Na mwandishi ameandika vizuri na yuko sahihi na anaeleweka licha ya maana yako ya kukariri. Nikisema unajuaje kama LTK haijapewa go-ahead na rais? Naweza kumaanisha unajuaje kama rais hajatoa ruhusu/idhini ya kuua? kwa mjibu wa maana yako ya LTK, au unajuaje kama rais hajaliruhusu hilo kundi kuua? Kwa mjibu wa mwandishi. Hata mwandishi katika maelezo yake mengine amemaanisha "license". Na narudia tena katika maelezo yako mengi umeonesha kwamba rais wako hawezi kufanya mambo fulani, sio hapa Tz labda kama unamaanisha rais wa nchi nyingine! Nina uhakika hapa Tz kwa jinsi siasa zilivyo rais anaweza kufanya jambo lolote hata kama linamshangaza mtoto wa chekechea!

2. "Mwakyembe anaweza kuwa na maadui lakini si kwa nchi yetu",

Hii kauli yako umetumia nini kuiandika? Yaani Mwakyembe hawezi kuwa na maadui Tz? Au unamaanisha nchi gani? Na wale mafisadi wa Richmond aliowaumbua sio maadui zake kweli? Yaani kama mtu wa kawaida tu ambaye sio mwanasiasa anaweza kuwa na maadui, unadai kwa Mwakyembe haiwezekani?
Unaniuliza " je hawa waliowaleta KGB mafia gani?" Katika maelezo yangu sijaongelea KGB.

3. Unawapangia wauaji njia gani watumie kuua watu! Wao ndio wanaojua ipi inafaa na kwa nini? Ni sawa na mtu ameuawa kwa kupigwa risasi halafu wewe unadai kwa nini wasingemuua kwa kumpiga rungu?

4. "Suala la Rais kuwatumia majasusi kumfanyia mtu mwingine ni la kudhania sana, upo huo uwezekano lakini si kwa hili, kwanza nahisi unahitaji elimu ya mfumo wa usalama wa taifa ila nitasamehe mi sio mahiri eneo hilo...."

Kwa nini unakuwa hauko makini kihivyo? Angalia juu kabisa kwenye habari yangu, msitari wa kwanza, nimeandika hivi "Sisemi kama ripoti ni sahihi au sio sahihi, isipokuwa:" Sikusema kama ripoti ni sahihi au sio sahihi, ila nimeonesha mambo ambayo kwa nchi yetu yanawezekana yenye uhusiano wa karibu na hii ripoti.

5. Wewe umeonesha kuwa ripoti sio sahihi, pinga basi kwa "logic", toa "concrete reasons", onyesha ushahidi inapowezekana ili kuwashawishi watu unachokiamini, kama mimi nilivyoandika kwamba ndani ya Tz kuna mambo mengi maovu yanawezekana, kwa kuwataja wahusika na baadhi ya matukio yaliyowakumba au waliyoyasababisha. Sio unaandika oh sidhani, haiwezekani, kwa nini wasingefanya hivi, najua n.k?

6. "Kama nilivyosema unahitaji ELIMU tena kubwa tu".

Elimu gani unataka kunipa? Unadhani kati ya mimi na wewe yupi anahitaji elimu?
 
Hii habari inataka kufanana na ile niliyoisikia hivi karibuni kwamba Al- Shabaab wamenunua maeneo kibao ukanda wa pwani ya kunduchi (si Ununio ndo hukohuko?) Lengo lao no kuwapa tafu maharamia wanapofanya uhalifu huko baharini wapate maficho na support ya uhakika. Hivi viongozi wa nch hii wamelala wapi jamani? Au ndo wamepewa cha juu walifumbie macho? mbona tumekwiiiiiiiiiiiiiiiisha. Hatuna viongozi bali wafanyabiashara mafisadi wameshauza kila kitu hata uhai wa raia wake umewekwa rehani. Eee Mwenyezi Mungu tuhurumie waja wako
 
Ndugu yangu machozi kweli yamenilenga lenga. Bora mwl. yeye alikuwa anatuweka kizuizini huko vijijini mwetu. Lakini huyu rais wa kutuuwa! mh! Gadafi. "Watakula vya kufisha nao hawatakufa!"
Kufa kwa watz hao na kuambatane na vifo vya familia zenu na damu zao zisizohatia na ziwe juu ya nyumba ya kila anayehusika na njama hizi mbovu.

Wote hapa duniani tutakufa
Wanayoua wenzau maisha Yao yanaweza kuwa mabaya zaidi
Mungu anapanga yote lakini mauwaji ni shetani
Mungu atusaidie na hao wabaya
 
Tz kila kitu kinawezekana,hata hao wakiuwawa leo hamna chochote kitakachotokea zaidi ya kusononeka na kulaumu,watz kama vile tumelaaniwa.Kuna mambo mengi ya kuufanya tu riot lakini tupo tv tunatumbua macho,uoga kibao...Jitu kama katiba mpya hakikuwa ni kitu cha kuhachia govt ipumue,na huo ni mfano mdogo.Watz ni wepesi kughilibika,nirahi7i ukawatoa kwenye jambo lolote la msingi kwa kitu ambacho hakina hata mashiko na wote wakaelekea huko,hii viongozi wetu wanajua kuitumia.Hebu tuwe serious japo kidogo.Vinginevyo hatuna chetu bongo hii.
Hili neno mkuu umeongea, kuna muda mambo wanayofanya viongozi wetu huwa inatakiwa kbs kama wananchi tuliowapa dhamana tuwahukumu,lkn wapi, kimyaaa.
Mfano halisi umeutoa wa katiba wananchi hata habari hatuna kama kuna shinikizo hilo tupo kimyaa,mwisho 2015 uchaguzi mwingine utafanyika pasipo katiba kubadilishwa,wa TZ sijui tuna matatizo gani??? sijui ujamaa umetuharibu,yaani ni watu tusiojali lolote,tena muda huo ambao hatujali sio kuwa hatujui tunaumia, tunajua sana tu,lkn watu wa kulalamika chini chini tu,mwishowe watu wanasahau,maisha yanaendelea na walio juu kuendeleza yao kwa kufanya watakavyo kwa kujua hakuna watachofanywa.
Kuna muda huwa natamani kulia kwa jinsi tunavyofanyiwa na viongozi wetu,pasipo sisi kama wananchi tuliowapa dhamana ya kutuongoza kuchukua hatua yoyote.
Hata sijui tulilogwa na nani.
 
Hekaya za Abunuwasi, hivi Mwandosya ana usafi gani? hakuna wa kumuua ila dhambi zake za kutafuna pesa za miradi ya maji vijijini na kuwaacha akina mama wa same wakiendelea kuchota maji kwa ndoo na kutembea umbali mrefu ndoo zikiwa kichwani. Haihitaji huruma huyu, adhabu aipatayo inamtosha. Mkuu uliyefanya uchunguzi, pitia upya vielelezo vyako, wengine humo wanachomekwa tu!
Jamani Musiwe mnaropoka hovyo kwa mambo ambayo hamuyajui. Leta ushahidi kwamba Mwandosya alikula hela ya miradi.
Unamtakia kufa unaweza kutangulia
 
Kibona aliwaaga marafiki pale salender B club mapema kabisa akielekea nyumbani, ajabu gari lake lilikutwa asubuhi limeegemea ukuta wa jengo la ubalozi wa burudi na ikatangazwa kuwa amepata ajali mbaya na kufariki hapohapo- ukuta haukubomoka na gari halikubonyea sana. Hii taarifa ya Mwakyembe ni ya ku-read bth the lines, ina lengo zaidi ya kuomba msaada wa ulinzi.
Check facts zako. Kibona alifia Ulaya, ni Mwaikambo ndio aliyefia Upanga
 
nimeikuta facebook nikaona niwaondoshee wadau kama ilivyo copy and paste... JE KUNA UKWELI HAPA??????

Beatrice John
RIPOTI YA UCHUNGUZI BINAFSI JUU YA UGONJWA WA DR HARISON MWAKYEMBE 12/10/ 2011
JASON BOURNE
TEL:*********
ID************

Hatua ya kwanza:
Niliamua kujua kama ni kweli kalishwa sumu au laa. Na watu nilio wahusisha katika kujua huko ni TISS.
Katika uchunguzi niliweza kuzungumza na LTK wapatao kumi na tano.
1. Maboharia wawili
2. Wapanga mikakati wawili
3. Mkuu wa LTK
4. Vijana wa kazi kumi
Wote maelezo yao yalifanana kwa maana ya (walishiriki kupanga na kutekeleza kumlisha sumu Dr Harison Mwakyembe)

Hatua walizopitia:
Kwa mujibu wa maelezo ya LTK/D00/B1 mkuu wa kitengo hicho ambae kwa kweli niliongea nae kama rafiki yangu wa karibu ndie aliyenipa mwangaza wakufanikisha kazi yangu.
Katika misheni hii watu wengi wanatakiwa KUFA, nitawataja wale muhimu tu:
1. Wilblod Slaa
2. Samweli Sitta
3. Harison Mwakyembe
4. Said Kubenea
5. Mark Mwandosya
Mnamo ijumaa ya tarehe 01/10/2010 saa 4:25, kikao kikuu cha mikakati kilikalika Moven Pick kikihudhuriwa na watu sita,
1. TISS/A001 XXX
2. TISS/B1
3. TISSB32
4. TISS/B5
5. TISS/A6
6. TISS/F5
Baada ya mjadala wa saa moja uliogusa magumu inayokumbana serikali na watu walio waona wao ni vikwazo na waliosababisha magumu hayo, ndipo wakaibuka na listi ya wanaotakiwa kusalimisha uhai wao:

Bada ya hapo kesho yake TISS/B1 alikutana na LTK/D00/B1 na kumpa amri ya misheni hiyo na orodha kamili ya watuhumiwa bila kumwambia sababu za mauaji hayo, zaidi alisema “nahitaji ripoti ya utekelezaji”. Baada ya amri kuwa chini ya LTK, mikakati ya aina ya kifo kwa kila mtuhumiwa ilipangwa ambapo walipamgwa katika makundi matatu,
1 Samweli Sitta
2 Harison Mwakyembe
3 Mark Mwandosya
Hawa wamepangiwa vifo vya aina mbili kwanza ajali na ikishindikana watalishwa sumu.
1 Said Kubenea
Kumwagiwa tindikali, baada ya kufeli ile ya kwanza imeagizwa nyingine toka Bulgaria yenye kuua baada ya masaa kumi na mbili tu!
1.Wilblod Slaa
Huyu anatakiwa kufa kwa shabaha ya risasi (snipers) ndio wanao andaliwa tu kwa sasa.
Waliopewa kipaumbele kufa ni Samweli Sita, Mark Mwandosya na Harison Mwakyembe ambapo LTK/D00/B10, LTK/D00/B14, LTK/D00/B17 na LTK/D00/B21 walipewa kazi hiyo.
Kikwazo kikuu walichokumbana nacho vijana wa kazi, ni kuwa, Sita, Mwandosya na Mwakyembe wote ni majasusi na kwapamoja walifanikiwa kufumbua njama hizo chafu za mauaji kwa siri.
Mitego ya ajari 16 kwa Mwakyembe yote imemkosa, 12 kwa Sita nayo ikamkosa,7 kwa Mwandosya nae kakoswa.
Walipoona mbinu zote za vifo vya ajali zimefeli wakahamia kwenye aina ya pili ya vifo vya kulishwa sumu:
Katika aina hii ya mauaji kwa muujibu wa vijana wa kazi wanashangaa uimara wa Samweli Sita na Mwakyembe kwani wameshalishwa aina nyingi za sumu lakini bado wanadunda tu, kwanza sumu ya kwanza kuwalisha ni katika kikao cha kwanza cha bunge mwa 2011, hawakupata madhara yoyote.
Wakabadilishiwa aina ya sumu, hakika hii ilimpata zaidi Mwandosya kwani ilipandikizwa katka simu yake ya mkononi bila yeye kujua saa 4:40 asubuhi ofisini kwake tarehe 7/3/2011.
Aina hii ya sumu (jina sikupata kujua lakini hapa huitwa LTK/XXX) nayo ilishindwa kuzaa matunda kwa Mwakyembe na Sita licha ya kupewa katika mazingira tofauti,hii ilitokana na kuwa kidogo.
Zoezi hili zito na la hatari baada ya kuwa gumu kupita kiwango kwakuwa hata Mwandosya hakudhurika sana, ilibidi uhitajike msaada toka nje ya nchi na ndipo jasusi mashuhuri wa kitanzania Exaveri H.Limo akaenda Urusi kutafuta aina nyingine ya sumu kali.
Tarehe 11/7/2011 akafanikiwa kukutana na Zudrav Ghev mmoja wa wakemia wa KGB katka kituo cha Moscow akapata Polonium 236, kutokana na unyeti na hatari ya sumu hiyo ilimlazimu bwana Zudrav Ghev kuchukua ndege ya watu wa tano na kuruka mpaka tz .
Baada ya kufika tz bwana Zudrav alitoa mafunzo ya wiki moja jinzi ya kuhifadhi na kutumia kisha akatokomea kurudi kwao na vijana wake wanne.
Baada ya Mrusi kuondoka misheni zikaendelea na mnamo tarehe 24 /7/ 2011 wakati afya ya Mwandosya ikiendelea kuzorota mmoja wa LTK/D00/B10 wa kike alifanikiwa kumuwekea Polonium 236 katika chai nyumbani kwake akiwa ni miongoni mwa watu waliokwenda kumjulia hali,
Na Mwakyembe alikuja kuwekewa ktk maji ya kunywa na kwenye kitambaa cha kufutia uso LTK/D00/B17 siku ya uzinduzi wa kikao cha Makandarasi,Wahandisi na Wakadiriaji majenzi pale Mlimani City kilichohudhuriwa na rais.
Kuonyesha kuwa Mwakyembe ni jasusi aliye kubuhu siku hiyo maji hakuyanywa wala kugusa kabisa lakini mungu si athumani kitambaa akakitumia, jambo la kushangaza nikuwa baada ya kama dakika 20 kukitumia kile kitambaa alikitupa wakati anatoka eneo la Mlimani City.
Hivi sasa LTK wameshamaliza kazi yao kwa watu wawili na anayefuata ni Samweli Sitta
Na uwezekano wa kupona kwa India ni mdogo ila wanaweza kupunguza makali na kusogeza mbeli mauti yao hiyo ni kwa mujibu wa mkuu wa LTK.
Slaa maandalizi yake yanaangalia zaidi uchaguzi ujao ingawa kumeingia aina ya mabishano makali juu ya kumuua hasa wakihofia kutokea kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe kwakuwa jamii ya kitanzania na kimatafa inamtambua
Said Kubenea amekabidhiwa LTK/D00/B21 ambae anasubiri kitendea kazi toka Bulgaria ambapo jasusi Yugrov Dittzov ndie atakae ileta.
Huu ndio uchunguzi wangu binafsi baada ya kupata taarifa juu ya hali ya Dr Harison Mwakyembe kuwa ni tete.
Nasema kuwa serikali ya Tanzania inafanya mauaji ya rai wake hasa viongozi wenye mtazamo tofauti na serikali.
Naiomba serikali ya Mh rais isikilize kilio cha watanzania isisikilize kilio cha wa kwasi na mafisadi. Nina waomba watanzania tuungane pamoja bila kujali dini zetu,makabila yetu wala rangi zetu kulikataa kundi hili la wahalifu lisilozidi watu 30.
Huu ni uchunguzi wangu, unahaki ya kusubiri uchungu wa madaktari wa India
ASANTENI SANA:

JASON BOURN.....JE WAMJUA JASON BOURN NI NANI???
 
Kwenye vita kila habari ni mhuhimu! Asante kwa taarifa mkuu!
 
Habari kama hizi hawezi kuzipata na kuzipanga kwa utaalamu huu mtu mwenzangu kama mie, lazima mwandishi wa habari hizi ni jasusi aliyekubuhi na mwenye kujua nyendo zote zinavyoenda. Kuna dalili za mwunganiko wa habari hizi na ukweli wa yanayojilia.
 
Habari kama hizi hawezi kuzipata na kuzipanga kwa utaalamu huu mtu mwenzangu kama mie, lazima mwandishi wa habari hizi ni jasusi aliyekubuhi na mwenye kujua nyendo zote zinavyoenda. Kuna dalili za mwunganiko wa habari hizi na ukweli wa yanayojilia.
Yah naona hii kitu imerudi tena!
 
Back
Top Bottom