Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Yaani hapa wala sihitaji kuweka maelezo mengi. Tunapoongelea kero za Muungano, mara nyingi ni ndugu zetu wa Zanzibar wanaoona kuna mambo mengi yanahitaji kurekebishwa. Sasa basi, badala ya kufurahia baraka ndogo ndogo za uraisi wa Samia kwa Zanzibar kama kumtuma raisi wa Zanzibar kumwakilisha Raisi wa Tanzania kwenye mikutano, fursa ni hii ya kupata katiba mpya ya Tanzania katika kipindi ambacho Samia yupo madarakani. Zoezi hili linapaswa kuanza mara moja kwa kuwa hatujui litakalotokea mwaka 2025 au hata mwaka huu huu 2021.
Suala la Katiba mpya lisionwe kuwa ni la Mbowe, Zitto na vyama vyao vya Chadema na ACT, na wala lisionwe kama litatoa nafasi kwa CCM kuondolewa madarakani! Ni suala la Watanzania, lakini hasa Wazazibari kwa kuwa mara nyingi Watanganyika wanataja kero pale tu Wazanzibari wanapotaja kero za Muungano kupita kiasi!