Na Bwanku M Bwanku.
Jumamosi Machi 12, 2022 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka alitangaza Uamuzi wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kujadili pendekezo la kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa CCM lililotolewa kwenye Kikao chake cha Desemba 18, 2021 na hivyo kutangaza Ijumaa Aprili 01, 2022 kuwa ni siku ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jijini Dodoma kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre.
Sasa nini maana ya Mkutano Mkuu wa CCM, Chama kinachoongoza Taifa letu?
Kwa Mujibu wa Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, Toleo la Mwaka 2017, Fungu la 7, Ibara ya 99 (2) imeeleza wazi kwamba Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa utakuwa ndio Kikao Kikuu cha CCM kupita vyote na ndicho kitakachokuwa na madaraka ya mwisho. CCM ina jumla ya Vikao 7 kuanzia Vikao vya chini kabisa vya Shina, halafu vikao vya Tawi, Kata, Jimbo, Wilaya, Mkoa na vya juu kabisa, Vikao vya Taifa. Kwahiyo katika Vikao hivyo 7 vya CCM, Mkutano Mkuu wa CCM ndicho Kikao cha juu kabisa, chenye nguvu kubwa na chenye madaraka ya mwisho.
Kwa lugha rahisi, Mkutano Mkuu wa CCM ndicho Chombo Kikuu cha maamuzi yoyote makubwa yanayoathiri Chama kizima Kitaifa na Ibara ya 100 kuanzia sura ndogo (1) hadi (7) imeeleza vyema kazi za Mkutano Mkuu wa CCM kuwa ni pamoja na kusimamia siasa nzima ya CCM Taifa na kupanga na kusimamia Utekelezaji wa shughuli zote za CCM, kubadili sehemu yoyote ya Katiba yake ya Chama ili kujiimarisha, kuchagua na kuthibitisha Jina la Mwanachama mmoja wa Kugombea Urais wa Tanzania na Zanzibar pamoja na shughuli zingine nyingi za kuongeza ufanisi wa Chama chote.
Ibara ya 99 (7) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 inaeleza pia kwamba Kikao hiki cha juu kabisa ndani ya CCM na chenye nguvu kubwa kuliko Kikao chochote kile kitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM- Taifa ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu ama asipohudhuria basi mmoja wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa awe wa Bara au Visiwani basi ataongoza Kikao hicho na ikitokea wote watatu hawapo ama hawawezi kuhudhuria basi Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itamchagua Mjumbe mwingine miongoni mwao kuwa Mwenyekiti wa muda wa kuongoza Mkutano Mkuu.
Mkutano Mkuu wa CCM unajumuisha Wajumbe zaidi ya elfu 2 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani (Zanzibar) na Mkutano Mkuu huu wa mwaka huu wa Ijumaa Aprili 01, 2022 pamoja na mambo mengine utajadili mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la 2020, marekebisho yenye lengo la kuongeza kasi na ufanisi wa Chama kwenye maeneo mbalimbali.
Leo ni takribani bado siku 4 tu kuelekea kwenye Kikao ama Mkutano huo mkubwa kabisa wa CCM pale Jijini Dodoma.
Hizo ndizo dondoo chache na fupi kuhusu Mkutano Mkuu wa CCM, Kikao chenye nguvu zaidi ndani ya CCM na chenye maamuzi makubwa yenye maslahi kwa Watanzania na Taifa zima.
Tutege sikio kusikia Mkutano Mkuu huu wa CCM Aprili 01, Mkutano Mkuu Maalum utakaokuwa na agenda maalum ya marekebisho ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 toleo la mwaka 2020.
Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com