29 Julai 2023
Dar es Salaam, Tanzania
MKUTANO WA KATIBU MKUU WA CCM, KUUTETEA KWA NGUVU MKATABA WA BANDARI
CCM yaanda mkutano uliowakusanya wana CCM kutoka mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam unaoendelea katika viwanja vya Kawe mjini Dar es Salaam
KISHINDO CCM KANDA YA MASHARIKI
Kama kawaida Katibu Mkuu wa chama kongwe dola cha CCM ameongozana na ujumbe wa makada katika kutetea mkataba wa bandari.
Na CCM hivyo imewaleta jukwaani majembe yao tegemezi kutetea mkataba ambao ni komredi Abdallah Hamis Ulega, Atupele Mwakibete, profesa Kitila Mkumbo, mwanasheria mbunge Jerry Slaa, mzee Stephen Masato Wasira a.k.a Tyson, wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa wakiongozwa na komredi Juma Gaddafi, Komredi Mwakitinya, Dr. Msengi, Dr.Fenella Ephraim Mukangara, Nikki wa II, wakuu wa mikoa Adam Malima, Albert Chalamila ...Abbas Tarimba, Songoro Mnyonge, Askofu Gwajima ...
Mjadala kuhusu bandari umekolea moto na huko Bukoba Kagera CHADEMA washangaa kuona haijawahi kutokea CCM kutembea nchi nzima kutetea mradi wa uwekezaji huko nyuma katika awamu za CCM mpya ya ubinafsishaji ya Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli ....
CCM tayari imefanya mikutano ya kikanda kama huu wa Kawe Dar es Salaam kule mjini Mbeya ambako ulikusanya wanaCCM wa mikoa jirani na Mbeya na pia kule kanda ya Kaskazini iliyokusanya mikoa kadhaa...
Leo jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa CCM komredi Daniel Chongolo ... profesa Kitila Mkumbo asifia mijadala mipana inayoendelea kuhusu mkataba wa bandari na hii ni demokrasia anasema mbunge wa Ubungo kada wa zamani wa CHADEMA ...
Hali kwa ujumla kwa wazito jukwaani na katika hadhara ya wanaCCM waliopo uwanjani ni sura za kinyonge, simanzi na za kukata tamaa ... shamrashamra hazipo watu wekosa utulivu wanazunguka zunguka hadi profesa Kitila Mkumbo anawashangaa waliohudhuria mkutano wa leo na kusema haufanana na ule wa kanda ya nyanda za juu kusini Mbeya au ule wa kanda ya kaskazini walioufanya vigogo hawa wa CCM ....