Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

mimi sina taaluma ya sheria lakini kuna mikataba nikisoma kurasa chache naona hatari iliyopo mbeleni. Tatizo ni kukosa uzalendo kwa taifa na ndio maana serikali imejiwekea record nzuri ya kushindwa kesi mahakamani.

Nadhani tuwe na mijadala huru kupitia radio na TV ili watu wajadili namna ya kuhandle rasilimali zetu mfano 'sera ya gas na mafuta' badala ya kuitisha makongamano ya siasa kama yale kigoda cha mwalimu. Naamini wapo watanzania wengi sana wanaoweza kutoa points za maana kupitia mijadala hii
Mkuu kwani sheria zinatungwa na nani?..Sheria zinatungwa na watu sisi wenyewe ndio tunatakiwa kuzitunga ili mwanasheria apate kuzitafsiri ktk mikataba yetu, sasa inapofika sisi hatuna sheria isipokuwa ile iloandikwa Ulaya kwa minajiri ya mwekezaji utamlalamikiaje mwanasheria ambaye kazi yake ni kutafsiri tu sheria na sio kuisimamisha. Hata huyo Muhongo siwezi kumlaumu maana sheria ya Ubinafsishaji ilikuwepo na viongozi wakaondolewa vizuizi vya kumiliki mali.. Muhongo angeweza vipi kumzuia Mkapa kununua Kiwila na kwa sheria gani ikiwa sio haramu imepitishwa bungeni.

Vita yetu kubwa ni UFISADI ambao umetokana na viongozi wetu watunga sheria na wapitishaji wa sera. Kama hawa wamelala na wamepitisha vitu pasipo kuzama undani wake wakajua mazuri na mabaya utaweza vipi kuwalaumu watendaji ambao wanafungwa na sheria butu. Hivyo natanguliza kupeleka lawama zangu kwa SERIKALI na BUNGE (lenye wabunge zaidi ya 230 wa CCM) ambao ndio ktk kundi la SIASA SAFI na UONGOZI BORA. Kama huko tumechemsha kupitisha vitu ktk SERA na sheria mbovu, mwanasheria hana budi pia kuchemsha anapotetea.
 
Elimu mnaisingizia tuu apa issue ni 10% mtu na elimu yake anaweka kando elimu anakula mlungula tena uku akijisemea kwani serikali ya baba yangu who cares wengi wanakula nami nile iki kidogo.
Bse kuna vitu kwenye mikataba they are beyond common sense yaani ata rational being hawezi kubaliana nayo
Imagine issue ya capacity charge kwenye mkataba kama wa Richmond yaani uzalishe umeme usizalishe jamaa wana raise invoice ya 152mil daily ivi apo ata layman si atauliza ivi kwa nini nikulipe wakati ukiwa hauzalishi umeme mbona kama kazi ya kanisa vileee
 
Kuna Legal firms kama 3 hivi kubwa ambazo ndizo zimeifikisha Tanzania kibla. Wako kila mahali kwenye mikataba mikubwa ya kinyonyaji na iliyojaa laana kwa human kind. Na kama shukrani wamepata nafasi ya kuwa na wawikilishi kwenye mahakama (majaji), balozi nje ya nchi na bunge.

Hizi kelele tunazopigiwa kuhusu FDI si pure comedy. TIC inaweza kutoa mwanga wa mkorogo uliopo kati hiki tunachoambiwa ni uwekezaji na 'uwezo wa watalaam' wa kuandaa mikataba. Hii nchi inatafunwa kama sambusa.

Madai kwamba mikataba mibovu ni kwa sababu ya elimu ya watalaam ni very insulting. Ni tabia ya kudharau na ifike mahali tuwaambie viongozi wa nchi hii wakome kusema hatuna wataalam wenye uwezo. Mikataba yote mibovu imeandaliwa na watanzania, na wanaolalamika kuwa ni mibovu ni watanzania. Kama hawa wataalam hawana uwezo mbona hatusikii hao wawekezaji wakilalamika kuwa wameandaliwa mikataba mibovu na wanasheria wa Tanzania?

Kuna mdau mmoja amesema kuwa tatizo linaweza kuwa beyond contract, kwamba wataalam wamepwaya kwenye negotiation. Bado kwangu mimi huu ni utani. Viongozi wamekubali kuchukuwa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi, wanajua (wanadai) kuwa hatuna wataalam and what do they do? Unajiri mtu yule yule unayesema hana uwezo? Hivi Botswana wana 'wazawa' wenye ujuzi wa mikataba kushinda Tanzania?

Nirudie, tabia ya viongozi wa nchi hii ya kusema mikataba mibovu ni kwasababu ya elimu, ikome.

Kabla ya Tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya kuanza kazi, wakubwa wengi (including wabunge) walikuwa wanapiga kelele kuwa watanzania hawaijui katiba iliyopo sasa! Hiki kitu kilimtibua mjane wa baba wa Taifa -mama Maria Nyerere na alinukuliwa na TBC1 akisema hayo ni 'mawazo ya kikoloni'. Mtanzania anaweza asijue ni kifungu number ngapi kwenye katiba kinachompa rais mamlaka ya kuteuwa mkuu wa mkoa, wilaya, mkuregenzi wa jiji mpaka managing director wa gazeti. Hili mtanzania wa kawaida alijua kabisa na linamkera, na anataka libadilishwe. Kutojua ni number ngapi haiondoi ukweli kuwa mtanzania anajua mfumo wa mtu mmoja kuwa na madaraka lukuki ni tatizo.

Hivyo hivyo, huhitaji PhD kujua nchi haifadiki sawasawa na rasilimali zake kwa sababu watu wachache wamekaa chini na kukubalina mfumo wa 'ujambazi'.
 
....
mimi nishachoka na naskia kichefu chefu nikisoma hizi habari eti kusoma kusoma sasa hao wasomi wametufikisha wapi?
Kwa kweli nchi bila wajuvi waliobobea haiwi nchi mkuu, tatizo kubwa tulilo nalo ni wasomi wetu kuwa wajasiriamali. Na hii inatokana na nini:
1. Walikwishapoteza uzalendo,
2. Walipewa kazi au elimu kwa kujuana,
3. Wanalipana hisani kwa mikataba hiyo n.k.
hivyo basi kwa wasomi aina hii tusitarajie kwenda kokote wala popote... sanasana wengine wanageuka kuwa wanaharakati kama si wana siasa! ndiposa unajiuliza hivi nini maana ya kuelimika? elimu yako inafaaje kwa jamii na taifa?
sihitaji kuitwa msomi ikiwa elimu yangu haina manufaa kwa jamii..
 
Mkuu kwani sheria zinatungwa na nani?..Sheria zinatungwa na watu sisi wenyewe ndio tunatakiwa kuzitunga ili mwanasheria apate kuzitafsiri ktk mikataba yetu, sasa inapofika sisi hatuna sheria isipokuwa ile iloandikwa Ulaya kwa minajiri ya mwekezaji utamlalamikiaje mwanasheria ambaye kazi yake ni kutafsiri tu sheria na sio kuisimamisha. Hata huyo Muhongo siwezi kumlaumu maana sheria ya Ubinafsishaji ilikuwepo na viongozi wakaondolewa vizuizi vya kumiliki mali.. Muhongo angeweza vipi kumzuia Mkapa kununua Kiwila na kwa sheria gani ikiwa sio haramu imepitishwa bungeni.

Vita yetu kubwa ni UFISADI ambao umetokana na viongozi wetu watunga sheria na wapitishaji wa sera. Kama hawa wamelala na wamepitisha vitu pasipo kuzama undani wake wakajua mazuri na mabaya utaweza vipi kuwalaumu watendaji ambao wanafungwa na sheria butu. Hivyo natanguliza kupeleka lawama zangu kwa SERIKALI na BUNGE (lenye wabunge zaidi ya 230 wa CCM) ambao ndio ktk kundi la SIASA SAFI na UONGOZI BORA. Kama huko tumechemsha kupitisha vitu ktk SERA na sheria mbovu, mwanasheria hana budi pia kuchemsha anapotetea.

mkuu, ndio maana hapo juu nilianza na "Tatizo ni kukosa uzalendo kwa taifa". Hawa wabunge wetu kila mara utasikia wapo nje ya nchi kujifunza na moja kati ya kamati zinazo safiri sana ni hii ya nishati na madini, labda mh Zitto atueleze hizo safari za nje zimesaidia nini kwenye kuanzisha na kuboresha sheria na sera ya nishati na madini

Mbali na hapo juu, jumuiya ya viongozi wa dini katika tafiti yao ya mwisho walieleza kwamba wamegundua kuwa bunge halitungi sheria na badala yake limekuwa likipokea miswaada kutoka serikalini (sijawahi kusikia mbunge akipinga statement hii).. sijui kama wewe mwenzangu unapoangalia au kusikiliza bunge huwa unauona muhimili wa bunge, kwangu mimi huwa nauona muhimili mmoja 'govt'.. kwakweli wabunge wengi hawaelewi tofauti kati ya bunge na serikali mpaka inafikia mahala mtazamaji/msikilizaji huelewi tofauti kati ya mbunge wa kawaida na waziri. Pia kuna swala la kuunga hoja ili usionekane mbaya/msaliti kwa chama kinachoongoza serikali, kukomoana kivyama au mtandao kwenye hoja za msingi, njia alizozitumia mbunge kuingia bungeni na mbaya zaidi kwenye utafiti wangu nimegundua baadhi ya wabunge na mawaziri huwa hawasomi makablasha.. hizoo ndizo sababu kubwa za kupitisha miswaada mibovu na baadae sheria mbovu.

Suluhisho, serikali isingeweza kuliingilia bunge kimamlaka iwapo wabunge wangekuwa wazalendo wa kulitetea bunge na katiba ya JMT
 
Kuna kusoma na kuelimika. Unaweza kuwa na kundi kubwa la wasomi nchi nzima lakini hawajaelimika. Hawana maarifa. Hawana uwezo wa kutumia elimu waliyoipata kwa faida ya jamii yao.
Elimu ni changamoto kubwa sana katika suala zima la mikataba kama ilivyo kwa uroho, tamaa, ulafi, wizi, uwongo, uzushi, kutokuwa makini, ulalamishi, ufisadi uliokithiri, kutotosheka nk.
Kuwa na rundo la wenye vyeti sio kuwa na wasomi. Wasomi ni wale wenye uwezo wa kutafsiri elimu zao walizopata ndani na nje ya Darasa kubadili maisha ya jamii zao.
Nitakupa mfano wa wasomi walioshindwa kutumia elimu zao na hivi sasa wanaonekana kama tumaini kwa serikali ya CCM. Prof. Muhongo - alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO mwaka 2005. Aliruhusu Kiwira kuuzwa kwa Mkapa, Yona na wenzake. Alikuwa mshauri mtaalamu kwa kampuni ya Sutton Resources ilipokuwa inauza mgodi wa Bulyanhulu kwa Barrick. Alikuwa kwenye timu iliyoandika sera ya madini ya mwaka 1997 na sheria ya madini ya mwaka 1998 ambayo ndio chanzo cha mikataba ya sasa ya madini ambayo imeligharimu sana Taifa.
Huyu ni msomi lakini at the hour of need hakusaidia jamii yake. Hata tulipokuwa tunahangaika (ukiwemo wewe MwanaKijiji) kuleta mabadiliko katika sekta ya madini hakupaza sauti yake. Hawa ndio wasomi wetu.

Ninapingana na hitimisho lako ambalo ndio ulianza nalo kwenye kichwa, mikataba mibovu inatokana na elimu mbovu. Elimu ambayo inaangalia maslahi binafsi badala ya maslahi ya Umma.


Haya ndiyo mambo tunayotaka kusikia ili kuendelea kufukuza hawa mafisadi....Never use their strength side to attack them but rather the weaker side....Hapo public yote itakuwa nyuma yako na tuta maximize votes, maana unaeleza ufisadi wa huyu jamaa in its real face!

Hata mimi nimefurahi kumjua japo kidogo....Thanks for answering one of my IFFs.....

Keep on pressing mheshimiwa usichoke asubuhi inakaribia kuingia!
 
Mimi nadhani tunaposema tatizo ni elimu ina maana kwamba haiwezekani kabisa nchi kuanza kuingia mikataba ya gasi na madini wakati haina sera ya gasi na mafuta. ELIMU tunayosoma ni lazima itambue mazingira tuliyopo na sio kusoma elimu ya kimataifa kisha unakuja itumia nyumbani kama ilivyoandikwa..

Mwanakijiji inashangaza sana kuona shirika linakuja wekeza nchini wakati sisi hatua sheria inayolifunga shirika hilo kuingia Ubia, hakuna sheria kwa wote inayolazimisha shirika yote nchini kulipa corperate tax isipokuwa tuna sheria za kuunganisha. Mwananchi anatozwa kodi kuliko mgeni paispo mshama lakini mgeni anapewa miaka 10 ya msamaha wa mafuta na vifaa..USOMI ni uelemika hivyo unapoweka mkataba mbovu hakika elimu yako inatupa wasiwasi ikiwa hutazingatia Watu na Mazingira..

Hata yule mzee wa Kariakoo leo hii akiuza nyumba yake anataka akatiwe maghorofa yake ktk jengo litakalo jengwa. Sheria za usajili na mkataba wanakwenda kwa Lawyer lakini tayari mwenye nyumba kisha weka msimamo wake kwa kutazama na kujali maslahi yake na familia yake. Usomi wetu hautazami maslahi ya taifa isipokuwa maslahi ya wageni kwa kutumia sheria na vitabu vya wageni vilivvyo andikwa kwa ajili yao. Tumesoma lakini hatujaeleimika na hata kama iwe matusi lakini ndio ukweli. Tumesoma sana ili kumtumikia mzungu ambaye katunga sheria zinazoambatana na mazingira yake sio yetu, hii sio elimu bali kujazwa Ujinga zaidi..

Mkandara thanks for these points...Kwanza tukubali tu hata sera yetu ya elimu ya juu ni utata mtupu..Huwezi kuwa na academia wazuri kama huna planning na forecasting kutegemea na mahitaji ya nchi. Waajiriwa wote katika academics wanategemea scholarship za sandakalawe toka kwa wahisani bila kuangalia mahitaji halisi ya Taifa kiasi ambacho ni wachache sana ambao wamepata proper training kwa hitaji la taifa. Wengi ni kachumbari kashika hili kacha karukia lingine kutokana na kinachomjia mbele yake...Hii impact haionekana sana sasa hivi lakini nawambieni hali itakuwa mbaya sana vyuo vikuu hawa old academia watakapo phase out maana atleast japo wengi ni complete metamophosis kwa maana walianzia certificate mpaka level ya u-profesor huku wengine wakipanda kwa njia za utata lakini atleast walikuwa consistent...

Lazima tutambue individual cost haiwezi kumpa incentive ya yeye kuamua ku-forego life yake na familia kwa lengo la kuitumikia Taifa..Kuelewa hii fact nchi za wenzetu wana subsidies elimu ya watu ambao wanaaminika wataleta proper innovations katika nchi na mara nyingi ndiyo maana kabla ya chochote kuamuliwa lazima vyuo vikuu vihusike katika invention na innovation kabla ya kupeleka kitu kwenye market kwa hapa chukulia mfano sera ya nishati na madini..

Kwa context ya Tanzania lazima kungekuwa na some kinds of inventions kwenye concepts ili kui-contextualize iwe tested ndipo iende kwenye decision body kama Bunge na exploitation ianze na hapo ndipo PhDs topics zingetokea na wataalamu wa hiyo sector ku-evolve na ku-grow kadri sector inavyo grow. Lakini sisi modeling ya uchumi wetu sijui nani huwa anahusika...

Pia natural resources ni multifunctional in nature hivyo sera moja haiwezi kuweka sustainable management na exploitation. Pia field moja haiwezi jibu complex issues zinazo emerge na transactions ya exploitations of such resources...Kwakuliona hili basi hapo ndipo multi-disciplinarity na interdisciplinarity inapokuwa applicable na lazima baada ya visera vidogo vidogo vinavyotakiwa kuandikwa kwenye associated sectors kama za mazingira, kilimo, elimu, maendeleo etc lazima kuwe na comprehensive policy na act ambazo zitahusika na enforcement ya hizo existing rules and regulations kwenye sector nyingine....

Kwa sababu hii utaona tunachokifanya ni utani na kichekesho mbele ya mataifa na ndiyo maana wanaamua kuchuma na kuondoka...

Kuna tatizo kubwa tena sana!
 
Kwa kiasi fulani nakubaliana na Prof. Muhongo, kuwa kuna tatizo la Elimu. Elimu inayoongelewa hapa siyo ile tu ya kuwa na PhD ya sheria. Ni Elimu ya sheria ya mikataba ya madini. Ili uweze kutengeneza mkataba mzuri wa mradi wa madini unahitaji pia kuelewa lugha ya kisheria inayoendana na fani, na maana yake halisi.

Lakini pia nakubaliana kuna tatizo la ubinafsi, na ubinafsi hapa siyo tu kuchukua rushwa bali hata kuacha kujibidisha kuhakikisha unatumia akili yako yote, ujuzi wako wote kuhakikisha unafanya kitu chema kwaajili ya nchi yako na watanzania wenzako. Lakini kwa watanzania walio wengi, hata asipochukua rushwa, anaweza asijihangaishe, na kusema kuwa kwa kwa nini niteseke, kwani napata nini?

Nawapeni mifano miwili ya ukosefu wa elimu ambapo wataalam wa sheria wasio na uelewa wowote wa elimu na lugha ya madini walivyofanya kosa kwenye mkataba wa uchimbaji wa dhahabu, Bulyanhulu, Kahama, mgodi unaomilikiwa na Barrick. Kwenye malipo ya mrabaha (royalty) wa 3%, iliandikwa kuwa 'the government will get a total of 3% of smelter gold or its equivalent value.

Wanasheria wetu inaonekana hawakuelewa maana ya 'smelter gold' lakini neno hilo lilikuwa na maana kubwa sana katika mapato. Hapo kilichotajwa ni dhahabu kamili tu iliyopatikana kutoka kwenye 'mill' na haikuhusisha ile dhahabu ambayo Barrick walikuwa wakiisafirisha kwenye mchanga ambayo siyo 'smelter gold' bali gold ore.

Barrick walipoanza uzalishaji walikuwa wakitoa 'smelter gold' 80%, wakibakiza 20% kwenye mchanga uliokuwa ukisafirishwa Japan. Walipotaka kukwepa zaidi ile 3% royalty, waliamua kutoa smelter gold 60% na gold 40% kubakia kwenye mchanga (gold concentrate). Kwa hiyo serikali haikuwa ikipata 3% ya thamani ya dhahabu bali 3% ya 60% ya dhahabu. Tatizo hapo lilikuwa ni Elimu.

Mfano mwingine wa pungufu wa Elimu ya Mtanzania, siyo wanasheria tu: Pale Bulyanhulu gold mine siku za nyuma wafanyakazi wote wa mgodini walikuwa wakiishi kwenye camp ya mgodi, wakigharamiwa chakula na malazi na kampuni ya Barrick, lakini huduma hizo za malazi na chakula zilikuwa zikitolewa na kampuni ya Ufaransa Sodexho kwa kiwango cha U$35 kwa siku kwa kila mfanyakazi.

Kwa hiyo kwa wastani ilikuwa ikiigharimu Barrick wastani wa U$35 x 30 =$1,050 kwa mwezi kwa kila mfanyakazi. Katika kupunguza gharama, Barrick waliamua kujenga nyumba kijijini na kuwakopesha wafanyakazi, na katika makubaliano ya kupata nyumba hizo ni kuwa mfanyakazi atalipa nusu ya gharama ya nyumba, na akikabidhiwa ni lazima ahame kwenye kambi ya kampuni (kwa hiyo kampuni itakuwa imeokoa U$1,050 kwa mwezi kwa kila mfanyakazi).

Nyumba hizo zilizojengwa na kampuni ya Caspiana (RA) gharama yake ilikuwa 1.4m (ya chini kabisa) mpaka milioni 40 (ya juu kabisa). Unaweza kuelewa kuwa kwa wafanyakazi kuondolewa kambini, Barrick iliweza kuepuka gharama ya U$1,050 x 12 =$12,600 kwa mwaka kwa kila mfanyakazi kwa kumjengea mfanyakazi nyumba ya TZS laki 7 mpaka milioni 20 (maana nusu ya gharama analipa mfanyakazi). Je katika kipindi cha miaka 5 ya ajira ya mfanyakazi, Barrick waliokoa shilingi ngapi? Lakini kwa Elimu ndogo ya Watanzania, wafanyakazi wale walishangilia kwa furaha sana wakidai kampuni inawajali.

Mfano mwingine niliuona nilipoangalia mkataba wa uchimbaji dhahabu, mgodi wa Nyamongo (North Mara Mines), kati ya serikali na Kampuni ya Afrika Mashariki (ambayo baadaye iliiuzia Place Dome, na sasa unamilikiwa na Barrick), mkataba ule ulimalizia kwa kusema, 'Hata kama sheria na sera za nchi zitabadilika, makubaliano haya hayatabadilika', --------------- Waziri wa Madini na Nishati akaweka sahihi yake (you know who was the Minister for Energy and Minerals by then).

Kuna tatizo la elimu, utashi, uzalendo, na ubinafsi wa kutaka kunufaika lakini pia wa kutokutaka ujuzi ulio nao au kile ulicho nacho na wenzako wafaidike. Angalia wafanyabiashara wenye pesa wanavyohangaika kuagiza bidhaa toka China badala ya kujenga viwanda nchini, ambapo wangetoa ajira kwa Watanzania wenzao, lakini hawawezi kufanya hivyo kwa sababu kujenga kiwanda kutachelewesha mfanyabiashara kupata faida (anajifikiria yeye tu na siyo watanzania wengine) kuliko kama akijenga kiwanda ambacho kingekuwa na faida kubwa zaidi kwa jamii na nchi pia.


Nimependa sana mifano hii. Sasa unless unaniambia kuwa wewe si Mtanzania. Kwa sababu kama umeweza kuyaona makosa haya yote na kuona nini kilichopaswa kufanywa bila ya shaka umetumia elimu yako. Na nitakuwa na uhakika wa kutosha kuwa labda baadhi ya watu uliosoma nao (assuming wewe ni Mtanzania na umesoma na Watanzania) watakuwa wapo humu humu au wanashika nafasi mbalimbali kwenye haya haya mawizara. Swali litakuwa inakuwaje wewe Mtanzania mmoja uweze kuyaona yale ambayo hawa Watanzania wengine hawakuweza kuyaona?
 
Kuna kusoma na kuelimika. Unaweza kuwa na kundi kubwa la wasomi nchi nzima lakini hawajaelimika. Hawana maarifa. Hawana uwezo wa kutumia elimu waliyoipata kwa faida ya jamii yao.
Elimu ni changamoto kubwa sana katika suala zima la mikataba kama ilivyo kwa uroho, tamaa, ulafi, wizi, uwongo, uzushi, kutokuwa makini, ulalamishi, ufisadi uliokithiri, kutotosheka nk.
Kuwa na rundo la wenye vyeti sio kuwa na wasomi. Wasomi ni wale wenye uwezo wa kutafsiri elimu zao walizopata ndani na nje ya Darasa kubadili maisha ya jamii zao.
Nitakupa mfano wa wasomi walioshindwa kutumia elimu zao na hivi sasa wanaonekana kama tumaini kwa serikali ya CCM. Prof. Muhongo - alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO mwaka 2005. Aliruhusu Kiwira kuuzwa kwa Mkapa, Yona na wenzake. Alikuwa mshauri mtaalamu kwa kampuni ya Sutton Resources ilipokuwa inauza mgodi wa Bulyanhulu kwa Barrick. Alikuwa kwenye timu iliyoandika sera ya madini ya mwaka 1997 na sheria ya madini ya mwaka 1998 ambayo ndio chanzo cha mikataba ya sasa ya madini ambayo imeligharimu sana Taifa.
Huyu ni msomi lakini at the hour of need hakusaidia jamii yake. Hata tulipokuwa tunahangaika (ukiwemo wewe MwanaKijiji) kuleta mabadiliko katika sekta ya madini hakupaza sauti yake. Hawa ndio wasomi wetu.

Ninapingana na hitimisho lako ambalo ndio ulianza nalo kwenye kichwa, mikataba mibovu inatokana na elimu mbovu. Elimu ambayo inaangalia maslahi binafsi badala ya maslahi ya Umma.

Hili ni zuri sana kwani nilitarajia watu wangeangalia hili. Tunafundisha watu ili wahitimu (we educate people to graduate them). Mtu anaenda shuleni ili "amalize darasa la saba", ili "afike kidato cha nne" au "ahitimu kidato cha sita". Na atatafuta chuo ili na yewe awe "ameenda chuo" na atapata shahada ili na yeye "apate shahada ya kwanza". Huyu ataamua kujiendeleza kwa sababu kuwa na "BA, BS" haitoshi anataka awe na "M.A" au M.Sc". Na akipata hizo anaona bado kuna nafasi ya kuwa na PhD kwa hiyo ataenda chuo na hatimaye atahimu na kupata elimu ya BA, MA, au PhD na vyeti vingine vingi. Hivi vitamuonesha kuwa "amehitimu" na kwenye madaraja ya elimu atakuwa amefika.

Kwa kila kipimo mtu huyo anaweza kuwa 'msomi' kweli na akawa na uelewa wa kutosha kabisa katika fani yake. Na ukimpa nafasi ya kufundisha utashangaa atakavyofyatua wasomi kwenye hicho chuo. Mtu huyo huyo kwa vile elimu yake imemtangulia jamii itamuamini kuwa anafaa kuwa kiongozi. Watu wetu wameshaaminishwa kuwa viongozi ni wasomi na hivyo wasomi wanapewa nafasi nyingi za uongozi si kwa sababu wamejioonesha kuwa ni viongozi bali kwa sababu wana elimu ya kutosha.

Sasa viongozi utawakuta ni wale ambao labfda hawana elimu sana ya kutosha. Hawa wanaongoza mabadiliko, wanasimamia mazingira, wanagombania shule zao ziwe safi, wanaanzisha vikundi vya kujisaidia wenyewe, na wanaanzisha miradi ya hapa na pale ya kusaidia familia zao. Utawakuta wengine (wasio na shahada kabisa) wanagusa jamii zao kwa kiasi kikubwa sana na wanabakia kuwa na mabadiliko makubwa. Na wapo - of course - wasomi ambao wanaonesha kwa vitendo kuwa elimu yao imewafikia. Mfano wa hayati Prof. Wangari Maathai ni wa kuuonesha. Angeweza kuwa msomi wa darasani na kuandika vitabu vingi kweli lakini she went beyond academic excellence. Alipoanza Green Belt movement wasomi wengine (wa darasani) walimuona kama ni crazy fulani hivi.... lakini aliweza kutafsiri vizuri elimu yake kwa vitendo.

Point ambayo ipo kwenye mjadala huu na hapa umegusia na mtu mwingine vile vile ni kuwa elimu kama elimu ni tatizo? Wewe mwenyewe ni zao la Chuo Kikuu cha Dar na nina uhakika umesoma kwenye shule zetu za Sec na msingi. Kwanini mtazamo wako wa matatizo ya jamii yetu uko tofauti sana? Inakuwaje (ukiwa umesoma na watu hawa hawa) unaweza kuyafikiria masuluhisho ambayo ni nje ya wanayofikiria wao?

Je yawezekana tatizo ni zaidi ya elimu inayotolewa?

NInaamini - honestly speaking - lipo pia tatizo la elimu inayotolewa ambalo unaweza kulioan hivi. Kama watoto wanaofeli ni wengi sana, na wanaopasi wanapasi kwa alama za chini basi kundi la wale wanaopasi kwa alama ya juu ina maana ni watoto ambao kwa kweli wana vipaji sana. Kwa mfano nadhani mwaka juzi mtoto aliyefaulu sana alikuwa ametoka mojawapo ya shule zisizo na vifaa kabisa na alifaulu yeye zaidi kuliko darasa lake zima (nadhani alitoka shule ya kata). Na watu walisifia kuwa shule za kata zinatoa mazao mazuri. Sasa kama darasa zima lingefanya vizuri tungeweza kuhusisha huko lakini kama kwenye shule ya kata mtoto mmoja anafaulu vizuri zaidi kuliko shule nzima ni wazi kuwa ni yeye mwenyewe huyo mtoto ana kipaji zaidi au kweli watoto wengine wote ni mambumbu.. au walimu..

Lakini, kama tatizo ni aina ya elimu inayotolewa imesababisha kuwa ni elimu ya kuhitimu ni wazi kile ambacho tumekuwa tukikisema muda mrefu na umekirejea sehemu nyingine ni kuwa sera ya CCM kwa kweli imefeli na tunachovuna ni matokeo tu ya sera hiyo. Haiwezekani basi kubadilisha tu watu bila kubadilisha mfumo na si rahisi kubadilisha mfumo kama CCM bado iko madarakani.

Kumbe ni maslahi ya kila Mtanzania kuona CCM inaondolewa madarakani. Lakini ikiondolewa madarakani chama kitakachoingia kinatuhakikishia vipi kuwa chenyewe kitakuja na sera nzuri na ambayo itakuwa na matokeo mazuri kwa taifa?
 
Hili ni zuri sana kwani nilitarajia watu wangeangalia hili la sera ya CCM kwa kweli imefeli na tunachovuna ni matokeo tu ya sera hiyo. Haiwezekani basi kubadilisha tu watu bila kubadilisha mfumo na si rahisi kubadilisha mfumo kama CCM bado iko madarakani.

Kumbe ni maslahi ya kila Mtanzania kuona CCM inaondolewa madarakani. Lakini ikiondolewa madarakani chama kitakachoingia kinatuhakikishia vipi kuwa chenyewe kitakuja na sera nzuri na ambayo itakuwa na matokeo mazuri kwa taifa?
Wapinzani wakuu Chadema wanaendelea kufanya kazi kibunge, kusubiri kwanza mawaziri kamili kuleta sera zao kisha wao mawaziri vivuli watoe sera mbadala!.

Kwa maoni yangu, kama ni kweli Chadema mnataka kujipambanua kuwa sasa mmeisha wiva vya kutosha na mko tayari kukabidhiwa nchi mwaka 2015, lazima mmbadilike, msiisubiri CCM iendelee to lead the way, you must come forward and show the way, the right way ili CCM nao wakija ama wafuate njia ya kweli au wawe forced to show the wrong way na wananchi wawe na options ya choice wachague nini na chochote watakacho chagua iwe wamekichagua for justified reasons kuwa kitatutoa hapa tulipo na kutufikisha pale!.

Zitto, kwenye suala hili la mafuta na gesi, kwa vile hatuna sera, this is an opportunity kwa Chadema to come with the best ever policy ahead of policy ya serikali na serikali will be left with no options lazima kuna vitu wataviiga watake wasitake na hii sasa ndio plus for Chadema na justified reasons to vote out CCM come 2015 besides kuichoka!, na iwe ndio justified reasons to vote in Chadema besides kuipenda. Chadema ijenge reasons to be votted in!.

Kama sera ya madini ya CCM mrahaba ulikuwa asilimia 03% na kwa sheria mpya ni asilimia 04% ambayo makampuni ya madini yameigomea kwa kisingizio cha kuheshimu mikataba ya zamani ya kinyonyaji, Chadema inapaswa ije na sera mbadala ikionyesha what is the best deal ili wananchi waweze kutofautisha CCM na Chadema na kuelewa kuendelea kuichugua CCM ni kuendelea kuwa masikini na kuichagua Chadema ni kuchagua ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.
Pasco.
 
Tatizo la Tz katika mikataba mibovu ni utawala mmbovu na usiofuata taratibu wa ccm.
 
Mikataba mibovu inatokana na mfumo mzima wa kiutawala kuwa mbovu. Tanzania ina wanasheria na wasomi wengine wazuri tu ila mfumo wa serikali usio na uwajibikaji na uliojikita katika rushwa ndivyo visabasishi vya kuzaliwa kwa mikataba mibovu na utendaji wenye tija hafifu. Pamoja na hivyo wasomi wanaotatufuta ukweli na haki wanawekwa kando (outside the mainstream of decision making) kwa kuwa wanaweka kiwingu kwenye dili. Utashi na ufahamu wa kung'amua mambo haraka unatofautiana kati ya wasomi. Hili nalo lingeangaliwa wakati wa kugawa majukumu ili kuleta ufanisi katika shunghuli za serikali badala ya kupendelea kwa sababu za kibinafsi.
 
Umemaliza yote kiongozi

Ukikaa na msomi wa kitanzania mkajadili jambo la kawaida kabisa ambalo lipo nje ya taaluma yake....utashangaa!!!

Hata kufanya analysis ya masuala ya kawaida tu... inakuwa tatizo...nafikiri kuna umuhimu wa kufumua mfumo wa elimu yetu na kuutengeneza upya....

Hili la kuongeza idadi ya wahitimu wa shahada wasio na uwezo na tunawapa majukumu makubwa kitaifa na kimataifa ni tatizo kubwa sana
Wayne: Yote tisa hata tukibadili mfumo wa elimu, kujifunza hakuna mwisho. Baada ya elimu ya nadharia vyuoni ni muhimu sana wasomi wasibweteke, wawe na mazoea ya kujifunza na kujisomea vitabu na majarida. Mambo yanabadilika vile vile changamoto ambazo hakuna anayeweza kuzibuni akiwa katika mfumo rasmi wa elimu. Tenknolgia na mawasiliano na habari wasomi wengi wana access wautumie kujiongezea elimu ili waweze kupambana na changamoto zinazoibuka kadri wakati unavyobadilika!! Wakati ukuta.
 
Jamani, nadhani kuna kitu sikielewi au nakielewa vibaya.
Suala la kutokuwa na elimu ya mikataba ya madini siliafiki kabisa. Hebu tujiulize tuna chuo kikuu pale Dar, kina wasomi waliobobea sana tena hizo degree zao zilizopandana zinatoka huko vitabu vya mikataba vinapoandikwa.
Tuna idara za sheria na jiolojia. Sasa kama hatuamini kuwa zinaweza kuisaidia nchi ni hadi tutakapopeleka watoto wakasome nje, tatizo sio madini wala mikataba tena!

Tujiulize lini umesikia wataalamu wakishirikishwa katika kutoa ufafanuzi, maelezo, analysis n.k katika masuala yanayohusu mikataba katika nchi yetu? Nakumbuka msomi mmoja alisimama na kusema ubinafsishaji wa TRC kwa kampuni za India haukufuata taratibu. Nani alimsikiliza! Je, tupeleke vijana waksome namna ya ubinafsishaji?

Tujiulize katika mikataba yote tuliyoingia ni upi ambao alikuwepo mgeni na kuuandika kwa niaba yetu?
Tujiulize, mashirika yote yanayokuja ikiwa ni pamoja na yale yanayotuibia mikataba yao inaandikwa na wanasheria wa makampuni ya hapa nchini mengine yakimilikiwa na wabunge na mawaziri.

Hata kama mikataba hiyo ni ya kipuuzi lazima tukubali kuwa iliandikwa na wataalam na kwa utaalam ndiyo maana baraza la mawaziri, Rais, Bunge na serikali yote havikuweza kubaini kuwa tulikuwa tunaliwa.
Hawa walioandika ni wasomi wa nchini kwetu hata kama wanatulaghai.
Sijui kama tunataka kupeleka vijana wapate elimu ya mikataba au uzalendo.
Kinachowashinda hawa wa nyumbani si usomi bali ni maadili duni na nidhamu mbaya kuanzia juu hadi kuwafikia wao.

Kuna mikataba inatuumiza sana lakini tujiulize, hivi tunahitaji vijana kwenda kusoma nje ili tusije tapeliwa tena na Kagoda?

Najaribu kujiuliza endapo tatizo ni wasomi na usomi basi tusingekuwa na kitu cha kuongelea leo. Nyerere na wenzake wasiozidi 10 ndio wasomi waliochukua nchi. Wangetapeliwa hadi kuuza pande la nchi wala si madini.

Najiuliza hivi Kidatu, Nyumba ya mungu, Hale, Reli ya Korogwe-Ruvu,TAZARA, viwanda n.k. tulivyovikuta akina Nyerere walikuwa na wasomi gani ambao leo hakuna kiasi tuamini kuwa tunahitaji kutuma wengine nje?

Najiuliza hivi tangu Nyerere atoe kauli kuwa 'acheni madini ardhini hayaozi Watanzania watakapokuwa na uwezo watayachimba' alimaanisha miaka 50 tutume watu kusoma nje ili kujua namna ya kusoma na kuandika?
Nasema kusoma na kuandika kwasababu siamini AG aliyesaini Richmond hajui kweli alikuwa anasaini nini.
Kama hajui je tunahitaji kupeleka vijana kusomea u-AG.

Tatizo letu ni kutokuwa na management iliyo na vision na nidhamu.
Ndugu zangu, majuzi rais kaulizwa vipi kuhusu TANESCO kuna mpango wa ubinafsishaji? Jibu rahisi la mheshimiwa ni kuwa hilo liachwe hadi rais atakayekuja. Serious! kwamba miaka 2 iliyobaki itaitumia kwa nini?
Sasa angekuwa amepata ushauri wa mmoja wa vijana tutakaosomesha kuhusu TANESCO, tumlaumu nani, msomi au kiongozi?

Jiulize wale wote waliotufikisha hapa wamechukuliwa hatua gani? Au wamesamehewa kwasababu hawajui.

Tatizo letu narudia tena siyo mikataba jamani, hatuna uongozi na hatuna nidhamu.
 
Wengi wanaoleta hoja za mikataba mibovu yaelekea wanaajenda za kisiasa zaidi kuliko hali ilivyo. Nijuavyo mimi, mikataba inategemea na mazingira ya wakati ilipofikiwa, taarifa zilizokuwa mbele ya jopo la wataalamu waliojadili mkataba husika, hali kwenye soko la dunia na mambo mengine mengi.

Ni vizuri ikatambulika kuwa mingi ya mikataba ya Serikali hujadiliwa na majopo ya wataalam na haishii hapo kwani mingi kuwasilishwa hadi kwenye Baraza la Mawaziri.

Kwa mantiki hiyo ni vigumu sana kuamini kuwa washiriki wamekula njama au hata Baraza lenyewe halikuzingatia maslahi ya nchi. Aidha, badala ya kulaumu kila wakati ni vizuri tukatoa mapendekezo ya kuboresha.
 
Sidhani kama kweli mikataba mibovu ya kinyonyaji tuliyonayo ni ukosefu wa elimu au ujuzi wa wanataaluma wetu katika mikataba. Si kwenye madini tu bali katika sekta zote. Ni ukosefu wa uzalendo na ile tabia ya wanasiasa kuwa waamuzi wa masuala mengi hata ya kitaalamu.

Mawazo ya mwanasiasa ni mabaya sana kwani huwa yanaharibu hata mawazo ya wataalamu. Katika maamuzi ya wanasiasa, huwa anaangalia miaka kadhaa ya uchaguzi ijayo, pale anapofanya maamuzi. Kwamba hayo maamuzi yatamnufaisha vipi katika nafasi yake ya siasa katika uchaguzi hasa kupata kiasi cha fedha kuwanunua wapiga kura au kuwafurahisha wakubwa wake waliomweka pale.

Fikiria katika nchi moja hii na wizara ile ile, waziri mtangulizi cha kwanza kabisa katika kujadili mikataba ya ufuaji umeme, ni Capacity Charges ambazo zinaliingiza taifa na shirika la Tanesco gharama na hasara kubwa sana.

Anakuja waziri mwingine, katika wizara hiyo hiyo (Sijui kama ni mzalendo au naye ni kwa masilahi yake fulani), hataki kusikia habari za Capacity Charges, katika mikataba hii ya kuzalisha umeme akiwa na wataalamu wale wale waliokuwa na waziri aliyepita.

Kama huyu asiyependa kusikia gharama hizi ameona zina madhara, kwa nini watangulizi wake wasiulizwe au wasifikishwe mahakamani, waeleze kwa nini waliingiza gharama hizo katika mikataba.
 
NInaamini - honestly speaking - lipo pia tatizo la elimu inayotolewa ambalo unaweza kulioan hivi. Kama watoto wanaofeli ni wengi sana, na wanaopasi wanapasi kwa alama za chini basi kundi la wale wanaopasi kwa alama ya juu ina maana ni watoto ambao kwa kweli wana vipaji sana. Kwa mfano nadhani mwaka juzi mtoto aliyefaulu sana alikuwa ametoka mojawapo ya shule zisizo na vifaa kabisa na alifaulu yeye zaidi kuliko darasa lake zima (nadhani alitoka shule ya kata). Na watu walisifia kuwa shule za kata zinatoa mazao mazuri. Sasa kama darasa zima lingefanya vizuri tungeweza kuhusisha huko lakini kama kwenye shule ya kata mtoto mmoja anafaulu vizuri zaidi kuliko shule nzima ni wazi kuwa ni yeye mwenyewe huyo mtoto ana kipaji zaidi au kweli watoto wengine wote ni mambumbu.. au walimu...


MMM asante kwa mfano huu vizuri lakini naomba kukuhakikishia ukichunguza kwa undani huyo mtoto aliyefaulu kuwazidi wenzake lazima kulikuwa na external factor iliyosaidia awe tofauti sana na wenzake...Kwa kesi kama hiyo wizara ya elimu ilitakiwa ifanye utafiti kugundua je ni IQ pekee ama kuna environmental factors? Nitolee mfano wa mimi mwenyewe...Na hili tatizo la watoto wasio na vipaji ila wako kwenye gud environment kufauli lilianza wakati wa enzi yangu mm na wewe nadhani kuanza awamu ya pili ambapo kulikuwa na corruption sana kwenye sector ya elimu kutokana na nafasi kuwa chache na mifano ipo hapa hapa JF ambapo kuna cases ambapo watu walitumia majina ya watu wengine ili waendelee mbele..

Nili expound hili la kwangu; mimi nilikuwa na soma shule nzuri comperatively na nilipokwenda kumalizia baada ya matatizo ya kifamilia...Nilipofika kule kijijini nilikuwa mbele mno kupita wenzangu ukichanganya kidogo na kauwezo nilikokuwa nako basi niliweza kupata sometimes average ya 98% katika masomo yote...Lakini hii ilitokana na maswali yaliyotolewa katika ile shule yalikuwa ya chini kuliko kule nilikotoka....Nikiri kuwa kulikuwa na watoto wenye IQ kubwa mno kuliko mm katika lile darasa lakini kutokana na mazingira kwanza ya familia zao na factor ya waalimu na vifaa vya shule walikuwa hawafanyi vizuri kama mimi..Ikaonekana mimi ni genius fulani so walimu wakaamua nisome ofisini ili nisirudi nyuma...Kweli hiyo special treatment ilinifanya nielewe mno kupita kiasi hadi kutokea mimi kufaulu vibaya mno darsa la saba peke yangu katika ile shule na kufaulu shule zote kumi za private nilizozifanyia mitihani...Je mimi kweli ni genius kupita wanafunzi wa enzi zangu? Hili nalikataa kabisa kwani ilijidhihirisdha baadaye kuwa I am not ila mazingira ndiyo yalichangia..Form one was the first in my class form two I became 2nd form three the seventh and form four the 10th japo nilifaulu to first class level lakini si ya u-genious wa primary level...

Kwahiyo basi ingekuwa ni IQ factor pekee basi ningeweza ku-maintain...So siku hizi hicho ndicho kinachotokea kwakweli mtoto wa shule ya kata hata awe na IQ kubwa kiasi gani hawezi ku-compete na yule wa school basi mwenye IQ sawa na ya kwake hata anayemzidi kwa margin ndogo...Hili limekuwa proved na university mmoja ambapo kulikuwa na special admission kwa wanafunzi waliokuwa na viwango duni...Wengi wa hao viwango duni ndiyo waliokuwa na GPAs kubwa na wengine kuwa na first class; wengine over all best student for all consecutive years waliyokuwepo hapo chuoni...Hii tu ni indication something is not right some where kwenye sera ya elimu yetu....

Lakini kuna kitu kina emerge kwa sasa hao hao wanafunzi wa kata ndiyo wanaokosa mikopo ya uhakika given the family condition walipotoka basi wanajikuta hawasomi vizuri so wanaishia kupata pass na hao wa school bus ndiyo wanaendelea kupata GPAs kubwa. Hao ndiyo tunaowapandisha haraka haraka kwani wazazi wao ndiyo wapo kwenye higher posts ndiyo wanaokuwa wansheria wetu na ndiyo ambao wanasaidiana na wazazi wao kutengeneza mikataba yenye faida at family levels na siyo taifa.....(tafadhali hii analysis siyo comprehensive maana haijafanyiwa utafiti so isiwe reference) Nia ni kutoa assumptions na hypotheses ambazo zinaweza saidia kufanya mabadiliko.

Our country is wrecked jamani let us agree to go to the drawing board....
 
Kumbe ni kati ya watu waliochangia kuharibu sector ya madini? umetufumbua macho, uzalendo wake uko wapi? hakika naona kama anataka kusahihisha kile alichoharibu. Kweli swala siyo usomi bali uzalendo.
 
Dada hawa wasomi wetu wameelimika ktk elimu ya vitabuni na hivyo sheria wanayoweza kuitumia ni ile inayowalinda wakoloni wawekezaji maana ndio ilokuwepo vitabuni. hakuna sheria ya kimataifa inayoandikwa kwa ajili yetu. Hata Marekani au Canada wana sera zao, hivyo kama hukusema ni lazima mwekezaji atoe share, asajili ktk soko letu DSE huyo mwanasheria ataweza vipi kutetea haki hiyo. Nini nafasi yetu ktk mikataba na kadhalika itakuwa kazi kubwa kupata utetezi wa haki..

Sheria za madini ni sawa na man's law, Ni sheria ya mfumo dume, inayotazama upande mmoja kumlinda mwekezaji zaidi ya sisi maskini na ndo maana vifo vingi ktk migodi ya madini huwezi kukuta shirika linahusishwa na mauaji. Mashirika ya madini wanalindwa na International law zaidi ya wananchi na nchi husika, hivyo mwanasheria msomi wetu ataitafsiri tu sheria iliyopo kuwalinda mabeberu na sii kutulinda sisi. Mgogoro wetu na Malawi tunatumia sheria ya mkataba wa Muingereza na Mjarumani tena karibu tunatoana macho lakini makubaliano na sheria yetu sisi ni ipi? Je, sisi wenyewe tumekubaliana vipi ama tuna sheria gani - hakuna! isipokuwa ile sheria ilitungwa karne 2 zilizopita kuwalinda wao na kwa maslahi yao lakini tunajiita wasomi.

Pasi shaka mabwana hawa wamefanikiwa systematically kuweka akili zetu bado kuwa dependant na za kitumwa. Mimi bado najaribu kuona exactly how do they do it? wanakuwaje wakati wakijadili hii mikataba, wanaweka nini mezani wenzao wakiweka maslahi yao mezani..............ni kama mazombie tu wanakubali tu pale inaposemwa tutachukua 80% na nyie 20% na vipi hawa wanaokuja bila hata mtaji na kutumia rasilimali zetu kama collateral..........hapa tamaa na maslahi binafsi yanahusika..........mbali ya kusema akili zetu ndogo zinaongoza akili kubwa. Kweli hatuna hata chembe utashi wa kawaida wa binadamu mbali ya kuweka kisomo?
 
Back
Top Bottom