Wala sio kununuliwa nyumba na gari ya kisasa bali aambiwe kuwa ananunuliwa gari hata Mark 11 kwa ajili ya kuwa linampeleka mke wake saloon au watoto tution na huu ndio ubinafsi wenyeweMMK, performance inapokuwa mbaya unaweza kutukanwa kwa tusi lolote. Mimi siafiki kabisa kwamba tatizo letu watanzania (siyo waafrika) ni elimu japo in some cases ni kweli ufahamu mdogo wa mambo fulani unachangia. Tatizo letu kubwa ni kitu kinachoitwa kwa ujumla wake UBINAFSI. Mambo mengi yanayofanywa na viongozi wetu wawe ni wa kisiasa au watendaji ni UBINAFSI. Wengi wao kila walifanyalo wanaongozwa zaidi na UBIBAFSI. Wanapojadili mikataba baina ya nchi na nchi wanaangalia watapata nini wao kama wao na siyo nchi itapata nini. Mtu yupo radhi ajengewe nyumba na kununuliwa gari ya kisasa kwa milioni chache huku akitambua kuwa kwa kufanyiwa hivyo, anaikosesha nchi mabilioni ya fedha ambayo yangeinufaisha watanzania takriban wote.