Tazama video hii uone Dkt. Tulia anavyomimina maelfu ya vitabu kwa wanafunzi jijini Mbeya

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika wana Mbeya hawakukosea wala kufanya makosa katika kumpa kura za ndio Mheshimiwa spika na Rais wa IPU na msomi Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini na dada wa Taifa Mh Dkt Tulia Acksoni Mwansasu kuwa mbunge wao.wana Mbeya wapo sahihi kabisa wanaposema kuwa hawataki kuiona kabisa sura ya Sugu ikija kuomba kura za ubunge jiji la mbeya.wapo sahihi sana pia wanaposema kuwa wanajuta sana kuwa katika Historia ya kuongozwa na Sugu maana wanajisikia aibu sana na hasira kubwa sana wakikumbuka jambo hio.

Katika video hii hapa chini inaonyesha namna Dkt Tulia anavyokwenda kugawa maelfu kwa maelfu ya vitabu kwa wanafunzi wote wa jiji la mbeya.hii maana yake nini? Hii inamaanisha kuwa dkt Tulia anataka kila mwanafunzi awe na kitabu chake mwenyewe mkononi pake ili aweze kujisomea akiwa mahali popote pale iwe nyumbani au shuleni au njiani au mtaani kwake.hii inakwenda kumrahisishia mwanafunzi kujisomea mwenyewe awapo nyumbani baada ya muda wa shule kuisha.

Dkt Tulia mbali na kuwekeza katika maeneo mbalimbali lakini anatambua kuwa elimu ndio msingi wa maendeleo ya aina yoyote ile.anatambua kuwa ukiwekeza katika Elimu unakuwa umewekeza katika maendeleo ya watu na Taifa zima kwa ujumla.hata mataifa tajiri leo hii yamefika hapo yalipo baada ya kufanya uwekezaji mkubwa katika Elimu.kinachofanya nchi yoyote ile iendelee siyo wingi au idadi kubwa ya watu wala siyo wingi wa utajiri wa madini yaliyopo wala siyo wingi wa vivutio vya utalii wala siyo wingi wa vyanzo vya maji wala siyo ukubwa wa ardhi yenye rutuba wala siyo ukubwa wa nchi kieneo au wingi wa bandari.

Kinachofanya nchi ikapiga hatua za kimaendeleo ni Elimu waliyo nayo watu wake na ubora wa elimu waliyoipata .ni ujuzi na maarifa waliyo nayo wananchi wake yanayotokana na Elimu bora waliyoipata.maana kama watu wako hawana Elimu nzuri na bora na ujuzi mzuri na maarifa ya kutosha pamoja na uzalendo wa kutosha unaweza ukawa na madaraja yanayobomoka kila mwaka licha yakuwa unamainjinia nchini, unaweza ukawa na njaa isiyo koma nchini na kuagiza mahindi na mchele kutoka nje ya nchi licha ya kuwa una ardhi kubwa na yeye rutuba .

Unaweza jikuta kila mwaka unatumia mapesa kwa mapesa kupeleka nje ya nchi kwa ajili ya kununua sofa za maofisini,unga wa chapati au maandazi ,wataalamu wa mikataba ,vijiti vya kujichokonolea meno kutoka china,nyama kutoka nje,maziwa kutoka nje,nyama kutoka nje ,leso za mafua kutoa nje na vingine vingi kutoka nje ya nchi.

Wakati huo huo una kila kitu kinachoweza kukufanya vitu hivyo vikazalishwa hapa hapa nchini ,kwa kuwa una ardhi ya kutosha kwa ajili ya kulima ngano,una miti na misitu ya kutosha kwa ajili ya kutengeneza sofa na viti vya maofisini,una vyuo vikuu vyakuweza kuzalisha wataalamu kwa ajili ya mikataba na utaalamu mbalimbali. Kwahiyo kinachohitajika ni kuwekeza kwa watoto na vijana wa kitanzania Elimu bora yenye kutoa na kuzalisha wasomi wazuri wenye ujuzi na maarifa ya kutosha na yanayokubalika katika soko la kimataifa na wanakwenda na wakati.

Elimu ndio kila kitu ,watu na vijana wako wakikosa Elimu na ujuzi wa kutosha maana yake utakosa mengi sana na kuachwa nyuma .lakini kubwa zaidi na baya zaidi ni kuwa utakuwa unategemea kila kitu kutoka nje ya nchi pamoja na wataalamu kutoka nje ya nchi. Hii ndio sababu ya dkt Tulia Acksoni Mwansasu kuamua kuunga juhudi za Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan katika kuwekeza vya kutosha katika Elimu ,ili tupate wataalamu wa kutosha katika kila Secta na kila Eneo.

Angalia tu nchi tudogo kieneo kama japani tumepiga hatua kubwa sana kimaendeleo kuzidi nchi kubwa kieneo kama congo Ambayo kila siku ipo vitani ikipigana vita mpaka miaka hii ya 2024, tena siyo kati ya rangi nyeupe na rangi nyeusi yaani wa Afrika na wazungu bali ni waafrika wenyewe wa Congo wakiua ndugu zao wa Congo.sasa sijuwi pengine inaweza ikawa ni laana ambayo tulimkosea Mwenyezi Mungu baadhi yetu wa Afrika mpaka kufikia hatua ya kuuwana sisi kwa sisi kwa vitu visivyokuwa na msingi.yaani badala ya kufanya maendeleo tunabakia kuuwana na kushindana kuiba mali zetu wenyewe kwenda kupeleka kwa wale wale wazungu waliotutawala siku na miaka ya nyuma.

Hii ndio maana Mheshimiwa jemedari wetu Dkt Samia Suluhu Hasssan amewekeza vya kutosha sana katika elimu ili kuwajengea ujuzi watanzania.ndio maana anatoa Billion 33 kila mwezi kugharamia Elimu bure tena iliyo bora . Hii ndio maana msomi Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini Dkt Tulia Anaendelea na kazi ya kuwekeza katika Elimu kwa kugawa maelfu ya vitabu pamoja na mambo mengine mbalimbali anayoendelea kufanya katika jiji la mbeya.

Lakini kuna mtu anaitwa Sugu alikaa miaka kumi kama mbunge wa Mbeya alishindwa kutoa hata kitabu kimoja tu kwa mwanafunzi wa darasa la kwanza .kwa kweli ilikuwa ni mkosi mkubwa sana kuongozwa na Sugu katika jimbo la Mbeya mjini. Ni mtu ambaye naamini hata yeye mwenyewe hakuelewa kwanini watu wamemchagua .ndio maana hakuelewa afanye nini zaidi ya kuzurula tu na kufaya Vitendo visivyo na staha bungeni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

 
Nilichogundua huna kazi ya kufanya ndio maana unao muda wa kuandika magazeti marefu ya sifa tuu.
Kisha kwa vile unaweka namba ya simu unatumiwa vijisenti vya kujikimu.
Njia ya hovyo sana kijana kujikimu maana inapelekea wengi katika kundi la
 
Nilichogundua huna kazi ya kufanya ndio maana unao muda wa kuandika magazeti marefu ya sifa tuu.
Kisha kwa vile unaweka namba ya simu unatumiwa vijisenti vya kujikimu.
Njia ya hovyo sana kijana kujikimu maana inapelekea wengi katika kundi la
Nina kazi za kufanya ndugu yangu na siyo kwamba hapa jukwaani ndio kazini kwangu. Kwa hiyo ondoa mawazo hayo kichwani mwako.
 
Back
Top Bottom