Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

Tatizo tulilonalo ni mfumo mbovu wa uendeshaji nchi.Hatuna vipaumbele kama taifa ndio maana kila Rais na serikali yake anapoingia madarakani anakuja na vioja vyake.Mara wengine wafute masomo ya kilimo na biashara ambayo ndo chanzo cha maendeleo katika dunia hii. Ni katika tanzania tu ambapo Rais anaweza kufanya chochote atakacho bila ushauri wa mtu yeyote kwa ajili ya taifa.Hii ni hatari sana kwa taifa.

Suluhisho ya matatizo yote yataondoka tu mara tutakapoweza kuiondoa ccm na serikali yake na kuwawajibisha kwa manufaa ya umma. Pili, tutengeneze katiba nzuri ambayo itaweka maslahi na vipaumbele vya taifa mbele na kuacha pembeni maslahi ya vyama na mtu mmoja mmoja.

Bila kufanya hayo tutaendelea kuteseka bila sababu yeyote ya msingi wakati Mungu ametupa rasilimali zote za utajiri ambazo zinawanufaisha wachache pamoja na wageni.
 
Taaluma ya SHERIA ambayo ndio inayotumika sana kuiandaa mikataba hii haina udhibiti wowote. Hawana bodi ya kitaaluma kama ilivyo NBAA kwa wahasibu na wakaguzi au ERB kwa wahandisi. Digrii za sheria zinaokotwa kila mahali sasa hivi kiasi kwamba hata mfungwa akiwa JELA anaipata!
 
Kwa kiasi fulani nakubaliana na Prof. Muhongo, kuwa kuna tatizo la Elimu. Elimu inayoongelewa hapa siyo ile tu ya kuwa na PhD ya sheria. Ni Elimu ya sheria ya mikataba ya madini. Ili uweze kutengeneza mkataba mzuri wa mradi wa madini unahitaji pia kuelewa lugha ya kisheria inayoendana na fani, na maana yake halisi.

Lakini pia nakubaliana kuna tatizo la ubinafsi, na ubinafsi hapa siyo tu kuchukua rushwa bali hata kuacha kujibidisha kuhakikisha unatumia akili yako yote, ujuzi wako wote kuhakikisha unafanya kitu chema kwaajili ya nchi yako na watanzania wenzako. Lakini kwa watanzania walio wengi, hata asipochukua rushwa, anaweza asijihangaishe, na kusema kuwa kwa kwa nini niteseke, kwani napata nini?

Nawapeni mifano miwili ya ukosefu wa elimu ambapo wataalam wa sheria wasio na uelewa wowote wa elimu na lugha ya madini walivyofanya kosa kwenye mkataba wa uchimbaji wa dhahabu, Bulyanhulu, Kahama, mgodi unaomilikiwa na Barrick. Kwenye malipo ya mrabaha (royalty) wa 3%, iliandikwa kuwa 'the government will get a total of 3% of smelter gold or its equivalent value.

Wanasheria wetu inaonekana hawakuelewa maana ya 'smelter gold' lakini neno hilo lilikuwa na maana kubwa sana katika mapato. Hapo kilichotajwa ni dhahabu kamili tu iliyopatikana kutoka kwenye 'mill' na haikuhusisha ile dhahabu ambayo Barrick walikuwa wakiisafirisha kwenye mchanga ambayo siyo 'smelter gold' bali gold ore.

Barrick walipoanza uzalishaji walikuwa wakitoa 'smelter gold' 80%, wakibakiza 20% kwenye mchanga uliokuwa ukisafirishwa Japan. Walipotaka kukwepa zaidi ile 3% royalty, waliamua kutoa smelter gold 60% na gold 40% kubakia kwenye mchanga (gold concentrate). Kwa hiyo serikali haikuwa ikipata 3% ya thamani ya dhahabu bali 3% ya 60% ya dhahabu. Tatizo hapo lilikuwa ni Elimu.

Mfano mwingine wa pungufu wa Elimu ya Mtanzania, siyo wanasheria tu: Pale Bulyanhulu gold mine siku za nyuma wafanyakazi wote wa mgodini walikuwa wakiishi kwenye camp ya mgodi, wakigharamiwa chakula na malazi na kampuni ya Barrick, lakini huduma hizo za malazi na chakula zilikuwa zikitolewa na kampuni ya Ufaransa Sodexho kwa kiwango cha U$35 kwa siku kwa kila mfanyakazi.

Kwa hiyo kwa wastani ilikuwa ikiigharimu Barrick wastani wa U$35 x 30 =$1,050 kwa mwezi kwa kila mfanyakazi. Katika kupunguza gharama, Barrick waliamua kujenga nyumba kijijini na kuwakopesha wafanyakazi, na katika makubaliano ya kupata nyumba hizo ni kuwa mfanyakazi atalipa nusu ya gharama ya nyumba, na akikabidhiwa ni lazima ahame kwenye kambi ya kampuni (kwa hiyo kampuni itakuwa imeokoa U$1,050 kwa mwezi kwa kila mfanyakazi).

Nyumba hizo zilizojengwa na kampuni ya Caspiana (RA) gharama yake ilikuwa 1.4m (ya chini kabisa) mpaka milioni 40 (ya juu kabisa). Unaweza kuelewa kuwa kwa wafanyakazi kuondolewa kambini, Barrick iliweza kuepuka gharama ya U$1,050 x 12 =$12,600 kwa mwaka kwa kila mfanyakazi kwa kumjengea mfanyakazi nyumba ya TZS laki 7 mpaka milioni 20 (maana nusu ya gharama analipa mfanyakazi). Je katika kipindi cha miaka 5 ya ajira ya mfanyakazi, Barrick waliokoa shilingi ngapi? Lakini kwa Elimu ndogo ya Watanzania, wafanyakazi wale walishangilia kwa furaha sana wakidai kampuni inawajali.

Mfano mwingine niliuona nilipoangalia mkataba wa uchimbaji dhahabu, mgodi wa Nyamongo (North Mara Mines), kati ya serikali na Kampuni ya Afrika Mashariki (ambayo baadaye iliiuzia Place Dome, na sasa unamilikiwa na Barrick), mkataba ule ulimalizia kwa kusema, 'Hata kama sheria na sera za nchi zitabadilika, makubaliano haya hayatabadilika', --------------- Waziri wa Madini na Nishati akaweka sahihi yake (you know who was the Minister for Energy and Minerals by then).

Kuna tatizo la elimu, utashi, uzalendo, na ubinafsi wa kutaka kunufaika lakini pia wa kutokutaka ujuzi ulio nao au kile ulicho nacho na wenzako wafaidike. Angalia wafanyabiashara wenye pesa wanavyohangaika kuagiza bidhaa toka China badala ya kujenga viwanda nchini, ambapo wangetoa ajira kwa Watanzania wenzao, lakini hawawezi kufanya hivyo kwa sababu kujenga kiwanda kutachelewesha mfanyabiashara kupata faida (anajifikiria yeye tu na siyo watanzania wengine) kuliko kama akijenga kiwanda ambacho kingekuwa na faida kubwa zaidi kwa jamii na nchi pia.
 
Kama hii nimeikuta kule kwa yule aliyeteuliwa kumnaibu Kitillya wakati ukweli upo wazi kuwa ndiye aliye iporomosha Barclays Bank.

Classmate huyu, jamaa kwao ni vichwa sana. Sijawahi kukutana na mtu jinias kama huyu na dada zake.

Shuleni high school, jamaa alikuwa analala haendi darasani halafu tukitoka darasani unamuhadithia mlichosoma kesho yake test anapata 100. Alikuwa EGM lakini alikuwa anakokotoa na kufunza watu wa form six, yeye akiwa 5 physics, namba, n.k.


Balaa huyu.
 
Kabla ya kuingia mikataba hii ya madini huyu AG wetu wa sasa alizunguka dunia nzima na timu ya wataalam mbalimbali kuangalia namna mikataba ya uchimbaji madini inavyoandikwa na utekelezaji wake.

Wakati huo AG alikuwa Chenge, msomi wa Havard. Tatizo sio ELIMU. Tatizo ni namna gani mkataba uandikwe kwa manufaa ya mtu kwanza.

Kuna wakati mkataba unakuwa ni mzuri tu ila kinachotekelezwa ni kingine kabisa. Na kwa kuwa hatuna "monitoring & evaluation teams" za mikataba hii, madudu yanafanyika kwa sana tu. Angalia kwa mfano wale wazungu tulioambiwa wamekamatwa juzi kule Geita.
 
Lakini pia nakubaliana kuna tatizo la ubinafsi, na ubinafsi hapa siyo tu kuchukua rushwa bali hata kuacha kujibidisha kuhakikisha unatumia akili yako yote, ujuzi wako wote kuhakikisha unafanya kitu chema kwaajili ya nchi yako na watanzania wenzako. Lakini kwa watanzania walio wengi, hata asipochukua rushwa, anaweza asijihangaishe, na kusema kuwa kwa kwa nini niteseke, kwani napata nini?

Ndiyo maana kuna umuhimu wa kuwa na experts. Ukimpa ZZK ashughulike na mikataba ya madini hawezi kufanya with deligence kwasababu hiyo siyo field yake. Akomae ili aprove nini?
 
Kwa kiasi fulani nakubaliana na Prof. Muhongo, kuwa kuna tatizo la Elimu. Elimu inayoongelewa hapa siyo ile tu ya kuwa na PhD ya sheria. Ni Elimu ya sheria ya mikataba ya madini. Ili uweze kutengeneza mkataba mzuri wa mradi wa madini unahitaji pia kuelewa lugha ya kisheria inayoendana na fani, na maana yake halisi. Lakini pia nakubaliana kuna tatizo la ubinafsi, na ubinafsi hapa siyo tu kuchukua rushwa bali hata kuacha kujibidisha kuhakikisha unatumia akili yako yote, ujuzi wa ..........NAPENDA KULIHAKIKISHIA BUNGE LAKO TUKUFU KUWA SERIKALI IMEPATA USHAURI WA KINA TOKA KWA KAMPUNI YA KISHERIA ILIYOBOBEA KWENYE MIKATABA YA KIMATAIFA KUWA TUVUNJE HUU MKATABA NA DOWAS HAUTATULETEA MATATIZO. Nukuu hiyo nimerejea kauli ya pinda bungeni kama nimepunguza au kuzidisha maneno naomba nisahihishwe.kumbe kampuni ya kimataifa ni REX.Na pale mambo yalipofinyingika ni REX hao hao waloitaka serikali ikubali kuilipa dowas faini . mimi nabaki najiuliza baada ya serikali kuingizwa mkenge na REX je bado kampuni hii inaendelea na kazi yake ndani ya mipaka ya nchii hii? kama ndio kwa nini? je mikataba inayopitia kwenye mikono ya wanasheria wetu baadaye ikaoneka ni mibovu je hao wanasheria tuendelee kuwa mikataba nao ya ajira? kama ndio kwa nini??.mambo ni mengi sana kwa ufupi watu ni mafisadi. wanaingia mikataba mibovu si kwa vile hawajui ,hasha ni ili wapate cha juu na wanajua hakuna wa kuwawajibisha. kwa ujumla inakera sana.masharti ya ajira lazima yabadilike.kwamba kama kampuni yetu ya umma imekuajiri kama mwanasheria then ushauri wako wa kisheria ukasabisha kampuni kupata hasara basi ajira yako inakoma mara na utawajibika kulipa hasara ilotokana na ushauri wako mbovu.je kwa utaratibu wa aina hiyo nani angetaka kuchezea jela????
 
Halafu kuna kipengele kimoja ambacho hatukiongelei. Amesema we are still learning maana yake yeye pia pamoja na PhD yake anahitaji elimu kwenye sekta ya gesi na mafuta. Sasa kejeli na matusi yamekusudiwa kwa nani?
 
Mama wa matatizo yote haya ni utawala dhaifu na rushwa,unazalisha ubinafsi,watumishi wa serikali wasiojali na wezi! Niliwahi simuliwa jirani zetu Kenya walipokua wanajadiliana na Tanzania kujenga bomba la gesi toka Dsm kwenda Mombasa jinsi gani timu ya majadiliano ya Tanzania ilivyokua imepwaya mno na ikionyesha watu walikua wanapelekwa Arusha ktk majadiliano bila maandalizi yoyote!
 
Nilijisikia hasira na aibu kwa pamoja pale niliposikia kwenye mahojiano BBC hapo jana eti Tanzani tunapoteza kwa sana kwenye madini na mi-gesi eti kwa kuwa HATUNA WASOMI WENYE UPEO WALA UTAALAM WA KUTOSHA KUPAMBANUA MAMBO huko ma-wizarani katika serikali yetu nchini????????????
 
Wale wanaotumwa kutuwakilisha kwenye hayo majadiliano mpaka kwenye hatua ya kutiliana saini kwenye mikataba huwa hawajali contents za mkataba na athari zake kwa Taifa bali wao wako waru waru tu wakitaka kujua watakatiwa kiasi gani ili huo mkataba upite na kusainiwa. Kifupi wanaweka maslahi yao mbele na ya Taifa hawana habari..
 
Its obvious kama issue ingekuwa ni kupata mikataba bora hata tungefanya kama tulivyozoea (Copy and Paste) kwa nchi zilizofaidika na madini yao.., LAKINI issue sio kupata mikataba bora ni nani ana 10% nzuri na nani ataniwekea posho nzuri kwenye account yangu Zurich
 
MM

Nilimsikiliza Waziri wa Madini kuhusu ukosefu wa elimu lakini either alichommanisha needed to contextualised or supplememented by more explanations of what he meant by lack of education. Lakini nakubaliana naye kuhusu ukosefu wa elimu kwanza nikimnukuu Mwalimu Nyerere alipokuwa akihutubia wanafunzi wa Makerere University "education begins when you graduate....." Alimaanisha kuwa kwa muda mrefu mwanafunzi anakuwa amejikita kwenye nadharia na anapomaliza chuo ndio mwanzo wa elimu kwani kile alichojifunza kinahitaji kutafsiwa na yeye kivitendo. Hapo ndio kuna mtihani mkubwa na hasa likija swala la ubinafsi, ulafi (greediness), megalomenia (kuamini unajua kila kitu), siasa kwenye utaalamu, ukosefu wa maadili, ukosefu wa uzalendo na mengine.

Wanasheria wetu wa Tanzania wamesoma na bado wanasoma mfumo ambao uko too specialised and disciplined based lakini ambao umewafanya kuwa too conservative and hence do not like to learn from others. Wapo ambao bado wanaamini law school of UDSM is the best in East Africa as it were in 1960s na wanakataa kuamini kuwa dunia imebadirika na inahitaji kitu cha ziada. Hawataki kujifunza toka kwa wengine ili wapate negotiation skills ambazo haziko kwene sylabus yake ya chuo. Sasa hawa wanakuja wanakutana na wanasiasa ambao megalomenic ambao wakishapata vyeo wanajiona wanajua kuliko wote as if akili hiyo imekuja overnight walipopata vyeo hivyo. Wote wawili wanageuka kuwa megalomenic na matokeo a blind man leading another blind man. Na hata wakipata nafasi ya kutemeba kwenda kujifunza kitu toka nchi nyingine wanatafuta nchi ambazo haziwezi kulinganishwa na Tanzania in all aspects. Kwa mfano kwenye sheria ya manunuzi sasa hivi kimeletwa kitu kinaitwa GPSA wakala anayeshughulikia procurement of common goods. Empirical examples zinazotolewa ambapo mfumo huo umekwa successful ni Singapore na Uingereza. The former's geographical size ni kama wilaya moja ya Dar. Sasa how this sustem work in Tanzania? Baada ya hawa wawili kujiona wao ndio wao wanajua kila kitu basi wanawaona Wananchi waliobaki ni mazezeta na hivyo wanaweza kuingia mikaba yoyote yenye 10% na zaidi maana wanaamini hatutahoji na hata tukihoji mikataba yenyewe hatuioni(ni siri) ya serikali. Tukiandamana kuna virungu na siku hizi tumeenda mbali tutatoa utumbo wa waandanamaji.

Nchi nyingi zilizotuzunguka na za mbali ambazo zimeleta mabadiliko through strikes and demonstrations lawyers wake wamekuwa among pressure groups. Wa kwetu hapa wamelala. Ukiwauliza kwamba you are supposed to show the lead watakwambia Tazanians are different from citizens in the sister countries. Poor argument. Have they ever tries rallied under one philosphy and for some reasons let down by wananchi. Hakuna. Sasa hapo ndipo tulipo. Ukija ukaweka na uzalendo unaoyeyuka kwa speed ya ajabu ndio maana unaona maajabu haya.

Nikirudi kwenye elimu, sasa hivi kuna vyuo vingi vimeanzishwa vinatoa degrees za sheria. Hapa napo kuna neno. Wapo wanasheria wengi hawawezi hata kuandika robo page of application letter. Sijui hawa wakipewa mikataba wataweza kuisoma na kuilewa?
 
kaka wewe pia ni part of the problem
Nakala ndefuuuuu wakati ukweli unaujua. Upuuzi huu ndio aliokwenda nao FREEMAN MBOWE huko DMV....kaja na filosofi ya ELIMU, ELIMU, ELIMU kisha LAW & ORDER

Richmond na EPA , kila kukicha mlitaka kutuaminisha kuwa mwenye makosa ni ROSTAM na LOWASSA lakini ukweli waliotuingiza hapo ni wanasheria wetu akina MKONO, akina MAAJAR & CO na wanasheria wengine ambao ni wasomi zaidi walioko Tanesco, wizarani, wizara ya sheria na kwingineko

Mie sina hiyo degree, kisomo changu ni form 6 lakini najua siku zote contracts zina pande 2 sasa iweje leo tunaaminishwa kuwa wahindi, wairan, akina mkono ndio wabaya wakai serikali hii ina mijitu ina degree 3 tutu?

mimi nakushairi. acha kutuletea hizo articles ndefu as if sisi ni wajinga na hatujui tatizo liko wapi. Lete article ya paragraph 2 max kisha waache hawa so called great thinkers waumize kichwa.

Mimi naona bora kama unapata ugali wako wewe endelea tuu lakini hii system imeoza, hao the so called wapinzani wameoza zaidi. Kila mmoja ale kwake

Eti LAW & ORDER...labda Law and order ya tv series na hata ile wahalifu wanakamatwa.

mimi nishachoka na naskia kichefu chefu nikisoma hizi habari eti kusoma kusoma sasa hao wasomi wametufikisha wapi?
HAKUNA KOSA KUBWA KWA BINADAMU KAMA KUKATA TAMAA!! be careful!! Hasa ukiwa kijana!!
 
Na wale wasomi wa Havard na viingereza vingi nao sio wasomi? Mbona ndio vinara wa ku compromise mikataba?
 
Ndio wamesoma wamepata ma PHD lakini hawajaelimika

Indeed those guys have learned and get all the certificates the universities in the world could offer...but majority never developed educated minds...ndio vinara wa kufanya mambo ya kimagumashi kutumia usomi wao....Chenge, Balali, Dr. Rashid, Dr.......
 
Hivi kwa nini msiseme tu kuwa tatizo ni wizi? Hii: elimu, ubinafsi, kukosa uzalendo si ni lugha za kistaarabu kwa watu walioamua kuweka ustaarabu pembeni na kuwa majizi aka majambazi? Manake wamefikia hatua ya kuua na kujeruhi wanaotishia mustakabali wao binafsi na wa mfumo wa kimafia walioujenga. It is futile to try to explain this phenomenon in any other way than plain thievery by state machinery that has only a political solution.
 
Tatizo ni kusomea mtihani na baada ya kuchukua ganda erosion takes place!

Umemaliza yote kiongozi

Ukikaa na msomi wa kitanzania mkajadili jambo la kawaida kabisa ambalo lipo nje ya taaluma yake....utashangaa!!!

Hata kufanya analysis ya masuala ya kawaida tu... inakuwa tatizo...nafikiri kuna umuhimu wa kufumua mfumo wa elimu yetu na kuutengeneza upya....

Hili la kuongeza idadi ya wahitimu wa shahada wasio na uwezo na tunawapa majukumu makubwa kitaifa na kimataifa ni tatizo kubwa sana
 
Back
Top Bottom