Wewe kuwa mkisto unataka ulazimishe watu wote waamini ktk ukristo wako? Dini ya Mayaudi hawanaamini ktk kristo kwanini unataka wamwamini Yesu? Ni imani ya madhebu ya kikiristo tu wanaomwani Yesu siyo dini nyinginezo.Kabla sijaenda mbali, kwanza nikiri mimi ni Mkristo, ila Ukristo wangu sio sababu ya kutohoji hata kama mtasema imani yangu ni ndogo.
Tukirudi kwenye mada, huku kwetu ukimpinga Kristo, hutaeleweka na utachakuliwa kuwa ni mwenye dhambi na unastahiili kuombewa.
Hata hivyo, cha kushangaza, wakati sisi tunaodai Israel ni Taifa telule la Mungu, Wayahudi wenyewe hawamkubali Yesu, na wameukataa kabisa Ukristo.
Kwa kifupi, jambo hili linaweza kuwa ni ushahidi tosha kuwa katika hizi dini, kuna mambo ya kutunga katika hivi tunavyovitta vitabu vitakatifu na huenda ni maandiko/aya zote ni uongo au baadhi ya maandiko/aya ndio za uongo .
Pia, nawaza,Tulia watanzania wengi hawamkubali, lakini huko nje ya nchi wamemkubali na kumpa cheo kikubwa tu. Je, ndio yale yale ya Wayahudi kumkataa Yesu na sisi huku kumkubali kama Mwana wa Mungu?
Hakika maswali ni mengi kuliko majibu.