Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Ninaamini nyumba bora huboresha afya ya mwili na akili. Mahitaji ya msingi ya binadamu ni hewa safi na kuishi sehemu isiyosababisha maradhi mfano baridi na unyevu unyevu. Nyumba bora huleta fahari kwa mwenye nyumba hata kukaribisha wageni na humjengea heshima katika jamii.
Watanzania wengi wanaishi kwenye nyumba za udongo na nyasi. Baadhi ya nyumba hizi zina ubora duni kiasi cha kwamba mvua zikinyesha wakazi wananyeshewa na maji kuingia ndani na kuleta hali ya unyevu nyevu. Pia nyingi hazina madirisha makubwa ya kuingiza hewa ya kutosha.
JamiiForums kama jumuiya ya jamii inaweza kuanzisha mchakato wa kujenga kijiji cha mfano. Wengine watakaopenda muundo wa kijiji hiki wataiga. Kijiji kichaguliwe katika Tanzania. Wanakijiji washirikishwe katika mpango na kama wakiridhia mchakato uendelee.
Ipatikane idadi ya wanakijiji, wenye uwezo wa kufanya kazi, vipato vyao nk. Wenye vipato wawe tayari kuchangia gharama za ujenzi. Wazee na walemavu wapatiwe msaada kutokana na michango ya jamii ikiwemo diaspora.
Wapatikane wabunifu watakao buni ramani ya kijiji na majengo. Majengo ya vyumba viwili na sebule pia vyumba vitatu na sebule kutokana na ukubwa wa familia. Nyumba ziwe sa saruji na kuwezekwa kwa mabati. Kuwe ná ceiling board pamoja na madirisha yanayoingiza hewa ya kutosha.
Vyoo viwe vya shimo vyenye sahani ya Indian toilet. Kila nyumba iwe na gutters za kuvunia maji pia kuwe na simtank.
Wanakijiji wanaweza kupatiwa majiko ya gesi pia kuhamasishwa kupanda miti. Hii ni katika harakati za kuokoa matumizi ya misitu na kuepuka jangwa siku zijazo.
Haya yakifanikiwa tuiombe serikali kujenga shule, zahanati, soko na ikiwezekana kituo cha polisi kijijini.
Katika kuchagua kijiji kiwe wapi ni lazima kuwe na vigezo vitakavyo washawishi wachangiaji kuchangia.