greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 781
- 1,211
MAKALA YA 2
Karibuni tena katika Makala yenye kutoa elimu juu ya mambo muhimu kwenye ujenzi wa Majengo (madogo) I.e. Nyumba, Maduka, Darasa, Zahanati n.kLeo tunatazamia katika Halijoto ndani ya jengo.Hili suala linawasumbua wakazi wa mikoa ya ukanda wa Pwani, Longido, Loliondo, Simanjiro, Mwanza n.k
1. Halijoto ni moja katika kitu kinachofanya mtu uone Jengo uone ni zuri pindi unapokuwa ndani.
Nje ya jengo, joto ni 30⁰C lakini ukiingia ndani joto linakuwa 36⁰C,hauwezi ukasema hilo jengo ni zuri.
Kwa upana wa Wilaya au Mji,joto usababishwa na;
I)Ukaribu wa Mji na Bahari,Ziwa au Bwawa
ii)altitude ya mji
iii)Mpango mji mbovu
iv)Ukosefu wa Uoto na mvua
2. Kuna miji ambayo ina halijoto kavu,yani inajoto kali lakini kiwango cha unyevu katika hewa ni chini ya 50%
Mfano;Longido,Loliondo,Simanjiro,Dodoma na Same.
Kwenye hii miji ,joto kali lakini jasho kidogo
Kuna miji ambayo ina halijoto lenye unyevu,yaani ina joto halafu na unyevu kwenye hewa unazidi 50%.
Kwa mfano;Dar,Tanga mjini,Zanzibar,Mtwara na Bagamoyo na Mwanza.
Kwenye hii miji joto kali na jasho la kutosha
3. Mambo yanayosababisha joto ndani ya Jengo.(Kabla ya ujenzi)
I) Umbo la Jengo : Kwa mikoa iliyo na joto ,inashauriwa jengo liwe na umbo la mstatili kuliko mraba. Umbo hili linaipa uraisi upepo kuingia na kutoka ndani ya jengo ukiwa bado una kasi.
Mfano.Majengo ya wakoloni mkoani Dar I.e. ikulu
II) Uelekeo wa jengo: Mapana ya jengo yanatakiwa yaelekee mstari wa jua kuliko marefu yake.
Mf.Kota za polisi Oysterbay
III) Nafasi kati ya jengo na jengo:Angalau kuwe na kuwa na nafasi isiyopungua mita 3,ili kuruhusu mzunguko wa upepo.
4. Visababishi vya joto (kipindi cha Ujenzi )
I) Urefu kati ya Sakafu na Dari;joto huwa ni hewa nyepesi kwahiyo itakaa karibia na dari. Hakikisha urefu wa Dari katika Chumba chenye makutano ya watu wengi kinazidi mita 2.5
II)Idadi ya Madirisha pale itakapowezekana hakikisha kila chumba kuna madirisha mawili
III)Ukubwa wa madirisha: Kadri dirisha linavyokuwa kubwa ndipo unaporuhusu upepo mwingi kuingia
iv) Madirisha yawekwe uelekeo wa upepo
Na
Panapowekwa dirisha:Madirisha ambapo hewa huingia yaanzie angalau 0.8m kutokea kwenye sakafu,hewa baridi huwa nzito so huwa chini.
V ) Ukubwa wa vyumba : watu hutaka kujaza vyumba vingi kwenye Majengo Yao na nafasi ikiwa ndogo, hutaka vyumba vipunguzwe vipimo .
VI) Milango mingi : kutoka jikoni kwenda sebreni mlango, kutoka sebreni kwenda korido ya chumbani kuna mlango,kwenda sehemu ya kula mlango:hewa haizunguki hapo.