Serikali iwahamasishe wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa na makazi bora

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,141
Lindi na Mtwara ni miongoni mwa mikoa ambayo wananchi wake wana uhakika wa kupata fedha za pamoja tofauti na baadhi ya mikoa.

Kuna msimu wa ufuta, vijana hupata mamilioni, msimu wa korosho wazee pamoja na vijana hupata mamilioni, msimu wa mbaazi pia huwapa mamilioni wakulima baadhi. Ila makazi ya wananchi wengi kusini (home land) ni duni.

Kipaumbele chao ni pikipiki. Fahari yao ni kila mtu awe na pikipiki yake. Million 2.5-3 inayoweza kununua pikipiki Moja inaweza kumfanya mtu aanze ujenzi wa nyumba ya wastani kijijini na msimu unaofuata akamalizia nyumba yake vizuri.

Makazi bora ndio ustawi wa jamii yoyote. Kila msimu mtu akipata pesa kusini huko mtu hununua pikipiki mpya au gari. Baada ya muda anafulia. Serikali ina sauti kubwa, ihamasishe watu wajenge nyumba bora.
 
Back
Top Bottom