KWANZA NIKUPONGEZE KWA MJADALA HUU! MIMI NAJIKITA KATIKA KUNDI LA WAFANYAKAZI KADA YA AFYA: Hawa ndugu zetu (wafanyakazi katika kada ya afya) mara nyingi wamekuwa wakifanya kazi masaa ya usiku na BUNGE lilipitisha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6 ya mwaka 2004 iliyotoa haki ya mfanyakazi kulipwa japo 5% ya mshahara wa saa kwa kila saa aliyofanya kazi usiku (kuanzia saa 2.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri) lakini Serikali hii ya CCM inawazungusha na kuwanyima maskini watumishi hawa haki hiyo.
Ushauri wangu kwa CCM ni huu, kama kweli wanataka wapate kurejea mbele ya watanzania mwaka 2015 ajili ya kuwaomba tena ridhaa, basi makovu madogo madogo kama haya yaepukwe. Naomba Viongozi wa Serikali wajiulize, mfanyakazi wa umma anayefanya kazi usiku na ambaye mshahara wake ni Tsh. 400,000.00 kwa mwezi, mshahara wa saa utakuwa Tsh. 2,308.00. Asilimia 5 ya mshahara huo ni Tsh. 115.40. Kama Mtumishi huyu ameingia kazini usiku kwa siku 16 kwa mwezi na kila siku alifanya kazi masaa 10 kwa usiku mmoja, atakuwa na haki ya kulipwa 115.40 x 16 x 10 = 18,463.00 kwa mwezi! Je, hii ni ngumu kwa Serikali kulipa? hata kama tunadai kuwa hali ya uchumi ni mbaya kiasi hiki ni kidogo sana! Tuheshimu sheria zetu tunazoridhia wenyewe. Let's be Serious, otherwise 2015 will be a night mare! it will be a ':israel:' to CCM