Kuanguka kwa CCM: Kutimilika kwa Unabii...

  • Thread starter Mzee Mwanakijiji
  • Start date

Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,202
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,202 2,000
chama kilichojiandaa kuchukua nchi kikoje? wajipange vipi? wape mkakati waweze kujipanga. Ni rahisi kumhukumu mchezaji aliyepo uwanjani. Ingia mchezoni tuone kaka!!
Siyo wote wachezaji
 
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
33,774
Points
2,000
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
33,774 2,000
Yanayotokea nchi za uarabuni ndio yatakayotekea hapa bongo tofauti itakuwa ni njia ya mapinduzi,wakati uarabuni wanapigana vita sisi bongo itakuwa ni kwenye sanduku la kura.Kila zama na mwisho wake.Yu wapi leo Gaddafi,Mubaraka,waliokuwa maraisi wa Yemen na Tunisia?Sidhani kama walitarajia kuwa kuna siku wangetoka madarakani tena kwa aibu na kudhalilishwa kama ilivyotokea.

Wawaulize KANU kilichotokea ni nini,wawaulze waliokuwa watawala wa Zambia na kwingineko.Ni vigumu kuzuia mabadiliko hata kwa mtutu wa bunduki.
 
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,492
Points
1,500
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,492 1,500
Bravo Mwanakijiji kwa makala nzuri!

Kwa muda mrefu tumekuwa na tatizo la wananchi kushindwa kuhusisha matatizo yao yanayowakabili na utawala uliopo madarakani...mara nyingi wamekuwa wakihusisha shida zao na "bahati mbaya", "mipango ya Mungu", "haikuwa riziki" n.k.

Kwa mara ya kwanza wananchi sasa wanaamka na kuwahoji watawala kwanini hali zao bado ni mbaya wakati wao viongozi wanazidi kunenepa, wananchi wanapanda ghadhabu wanaposikia hizi hadithi za miaka nenda rudi za wizi na ufisadi wa kutisha huku wao wakiwa hawana uhakika wa mlo wa siku. Shida ikizidi sana huwa inaamsha watu aisee....na usicheze na mwananchi aliyefulia na kupigika!

Hakika anguko kuu la CCM linakuja!
 
mbogo31

mbogo31

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2008
Messages
698
Points
225
mbogo31

mbogo31

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2008
698 225
MM nakala yako imeniacha natetemeka kwa hisia za ukombozi wa nchi yetu, kwa yeyote mwenye frikra sahihi hawezi kupinga kwamba nchi hii inahitaji ukombozi na unatakiwa uwe mwaka 2015, shukrani kwa makala bora tutajitahidi tu durufu ili hata wale wasisoma mitandao na magazeti tuwafikishie ujumbe huu.
 
U

Unstoppable

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Messages
1,048
Points
1,195
U

Unstoppable

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2011
1,048 1,195
Sheikh Yahaya mwengine well tukuulize umetumwa ? Kila la kheri we shall see mie sina chama ila nadhani CCM kuanguka ni ngumu sana. Zaidi kwasababu Chadema ni chama hakijajipanga kuchukua nchi hata kidogo. Sana sana kutatokea machafuko tu hasa ya kidini mark my words......
Hapo penye blue (Ivi kwani awamu hii ilijipanga kuchukua nchi?) Mimi ninavyoona mambo yanavyokwenda anybody can be a president in Tz i.e. nafasi ya uraisi haina heshima tena kama ilivyokuwa. Infact kikitokea kikundi fulani cha jeshi chenye udhubutu kinaweza kuongoza hii nchi ya TZ- its very sad.
 
Henge

Henge

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
6,876
Points
1,250
Henge

Henge

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
6,876 1,250
Hilo la kutokea machafuko limekuwa linatumiwa sana na ccm, kwa bahati mbaya kipindi hiki habari zinapatikana kwa urahisi zaidi hivyo upotoshaji watu eti kwa kisingizio cha kuwepo machafuko upinzani ukipewa madaraka hauna mashiko!
mkuu tatizo la ccm wako nyuma sana na muda!
 
Nyunyu

Nyunyu

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2009
Messages
4,369
Points
1,250
Nyunyu

Nyunyu

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2009
4,369 1,250
Sheikh Yahaya mwengine well tukuulize umetumwa ? Kila la kheri we shall see mie sina chama ila nadhani CCM kuanguka ni ngumu sana. Zaidi kwasababu Chadema ni chama hakijajipanga kuchukua nchi hata kidogo. Sana sana kutatokea machafuko tu hasa ya kidini mark my words......
Mdondoaji, umesema vema. Lakini upenpo wa mabadiliko umeshavuma tena kwa kasi!! Nachooona tutakuwa kama Malawi au Zambia. Kwamba CCM itakwenda na bado matatizo yatakuwa pale pale!!!
 
Ruhazwe JR

Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2011
Messages
3,411
Points
1,195
Ruhazwe JR

Ruhazwe JR

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2011
3,411 1,195
mwanakijiji,kuna vitu unaweza andika na watu wakachukulia rahs tu.kiukweli uzi huu una ujumbe mzite na unatupa moyo sisi wapenda mageuzi.mimi nakupa pongez maana umekwa mbele bila woga.mungu akutie nguvu
 
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
4,837
Points
2,000
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
4,837 2,000
MM,
Agreed to a man.

Wishes aside, there's a head of steam gathering. It's peaked and its momentum is felt. The wind of change simply hasten it even to blow any obstacle in its wake. Phew!
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,202
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,202 2,000
Kinachonitisha zaidi - hasa baada ya kuamka leo - ni kuwa CDM inaweza ikajikuta nyuma ya mwamko wa mabadiliko. Kuna zaidi ya kufanya mikutano na watu kuhamia kwa wingi CDM.
 
Nyunyu

Nyunyu

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2009
Messages
4,369
Points
1,250
Nyunyu

Nyunyu

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2009
4,369 1,250
Kinachonitisha zaidi - hasa baada ya kuamka leo - ni kuwa CDM inaweza ikajikuta nyuma ya mwamko wa mabadiliko. Kuna zaidi ya kufanya mikutano na watu kuhamia kwa wingi CDM.
I hope there is a team of strategists who think all these through in CDM to make sure, they wont let wananchi down!!
 
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Messages
21,836
Points
1,250
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2008
21,836 1,250
Labda nikwambie kitu kimoja tu MMM, ccm ya sasa haiwezi kujipanga

labda useme kitu kingine
 
Parata

Parata

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Messages
3,110
Points
1,225
Parata

Parata

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2011
3,110 1,225
wana jamvi ktokana na hali inayoendelea hapa nchini tanzania nathubutu kutabiri kuwa ccm ndo imefika mwisho na mwenye macho haambiwi tizama
 
Constantine Akitanda

Constantine Akitanda

Member
Joined
Feb 15, 2012
Messages
29
Points
20
Constantine Akitanda

Constantine Akitanda

Member
Joined Feb 15, 2012
29 20
[FONT=&amp]TAARIFA YA DP KUHUSU UNYAMA DHIDI YA DR. ULIMBOKA[/FONT]
[FONT=&amp]Tarehe 30/6/2012[/FONT]​
[FONT=&amp]NI ISHARA YA KUANGUKA KWA UTAWALA![/FONT]

[FONT=&amp]Tumeamua kuvunja ukimya kuhusu mpango wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wa mauaji ya kinyama ya Daktari Steven Ulimboka na wenzake. Kwanza kabisa tunatoa pongezi kwa vyombo vya habari kwa uzalendo na uhanga wenu, wa kuweka wazi unyama wa kutisha, ambao dunia yote sasa imeshuhudia jinsi ulivyotoa makucha yake na tutaendelea kuipasha.[/FONT] [FONT=&amp]Sasa inakumbukwa ile kauli ya Rais Kikwete kwamba yeye akisema "No" ni "No" tu, na kwamba hao watakaoshughulikiwa hata wakienda kumlalamikia kwa taasisi za Haki za Binadamu haitawasaidia kitu!

Inakumbukwa pia kauli yake aliyoitoa Dodoma katika kikao kilichopita cha halmashauri kuu ya chama chao, akiuhakikishia mkutano huo kwamba kamwe CCM haitafia mikononi mwake yeye, bali atahakikisha kuwa kinashinda mwaka 2015 kwa gharama yoyote, labda kifie mikononi mwa hao atakaowaachia! [/FONT] [FONT=&amp]Mpango umefichuka, nao ni kuizimisha taaluma ya habari, ambayo ndiyo inayotumiwa kukiinua chama cha Chadema na kuiteketeza CCM, kwa kuwateka nyara na kuwaua kinyama waandishi mahiri wa habari, kama walivyomfanya Daktari Ulimboka lakini Mungu akawafedhehesha kwa kuidhibiti mauti kwa uweza wake! [/FONT] [FONT=&amp]Na sasa wauwaji wa serikali wanajaribu hila za kila aina ili wamalize kabisa uhai wa Dr. Ulimboka pale Hospitalini MOI, lakini wanakutana na ulinzi mzito wa madaktari wenzake pamoja wahanga wengine, chini ya mkono wa Mungu ambaye amekusudia kulipa kisasi! [/FONT] [FONT=&amp]

Maharamia wa serikali sasa wanahaha kumtafuta Daktari Deo Michael ambaye aliwashuhudia wauwaji wote wa serikali waliohusika na unyama wa kutisha uliofanyika, wameazimia kumwua kwa kudhani kuwa watakuwa wanaharibu ushahidi, lakini kila kilichofanyika sasa kinaeleweka bayana, na wote waliohusika na unyama huu wa kutisha wanajulikana, ni makachero wa Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa! [/FONT] [FONT=&amp]UZALENDO ULIO NDANI YA MGOMO WA MADAKTARI WETU[/FONT] [FONT=&amp]Wananchi wengi wamepotoshwa kwa sababu ya ufinyu wa ufahamu wao, kutokana na upofusho wa kifikra wa CCM, kiasi cha kutoelewa kwamba mgomo wa madaktari wao unawatetea zaidi walalahoi, ambao ndio wanaokufa na kumalizika kwa kutoweshwa kwa makusudi na watawala wa CCM vitendea kazi muhimu vya utabibu katika Hospitali, wakati watawala pamoja na familia, na ndugu, na rafiki zao wakiamka na chunusi tu wanapeana mabilioni ya fedha ya walalahoi wakatibiwe na kustarehe nje ya nchi! [/FONT] [FONT=&amp]Madaktari wetu wanakosea wapi, ikiwa huduma bora za tiba wanazodai leo kwa migomo zilitolewa bure kwa raia wetu, kutokana na uchumi wa Taifa lao uliotegemea kilimo na mashirika ya umma ambao haukugusa kabisa hazina yetu ya madini, leo baada ya wananchi kuachwa bila kitu wanaambiwa walipie matibabu na elimu, wakati tani za dhahabu na raslimali zingine zote zinakombwa usiku na mchana bila kukaguliwa? Madaktari wetu wanatetea huduma kuu ya Taifa letu ya uhai wa raia!

[/FONT] [FONT=&amp]Isitoshe, duniani kote hata huko wanakoenda kutibiwa hawa watawala wa CCM, malipo ya madaktari yako juu kuliko fani zote, kwa sababu ya thamani ya uhai wa binadamu wanaouhudumia. Udaktari unasomewa kwa miaka 21 na ubingwa wa kitabibu ni miaka 25, lakini daktari wetu anakwenda kulipwa shilingi laki sita, wakati afisa wa TRA au Benki Kuu anakwenda kulipwa zaidi ya shilingi milioni mbili, Mbunge ndiyo usiseme, urais wa matanuzi kama wa Kikwete ni wa matrilioni ya fedha! [/FONT] [FONT=&amp]Magonjwa yote yanayowamaliza wananchi weanatupiwa wao, lakini posho wanayolipwa haiwezi hata kuwapa chakula bora cha kuzilinda afya zao.

Tunamkufuru Mungu kwamba wafe tu na njaa kwavile eti kazi yao ni ya wito! Fani zote ni vipawa, na vipawa vyote hutoka kwa Mungu, kwahiyo vyote ni wito ila tunatofautiana kuheshimu huo wito. Ni agizo la Mungu kwamba "Kila mtendakazi astahili ujira wake, hata ahudumuye madhabahuni imempasa ale madhabahuni". [/FONT] [FONT=&amp]Madaktari wa nchi yetu ni wavumulivu sana kutokana na uzalendo wao, tatizo la wagonjwa ni unyama wa watawala wa CCM, kama unyama waliomfanyia Daktari wetu. [/FONT] [FONT=&amp]Walengwa wa unyama huu ni pamoja na wanasiasa (bilashaka siyo Chadema) na raia wenye ushawishi katika jamii watakaozidi kuupinga utawala wa Jakaya Kikwete, wataanza kutekwa kwa mabavu kisha hawataonekana tena, miili yao isipookotwa msitu wa Pande! [/FONT] [FONT=&amp]Walengwa wengine wa unyama huu ni viongozi wa vyama vya wanafunzi hususan wa vyuo vikuu, na wafanyakazi ambao ni pamoja na Waalimu, ambao hawatafungika modomo yao kwa rushwa au vitisho, ambao katika kuwafanyia unyama wa jinsi hii watasingiziwa kujihusisha na upinzani, ingawa wanasagiwa meno hata mahasimu walio ndani ya CCM yenyewe! [/FONT] [FONT=&amp]

Mpango huu wa unyama unawakusudia pia viongozi wa kidini, wale watakaothubutu kuupinga ushetani wa utawala huu. Watatumika Waislamu watakaojifanya wa imani kali, pamoja na Wakristo ambao wanaonunuliwa kwa vipande thelathini vya fedha. [/FONT] [FONT=&amp]Kikwete na wauwaji wake wametangaza vita hii wakisahau kwamba hata wao ni damu na nyama na mifupa! Wote wamezaliwa na wazazi, na wote wana wake na watoto na ndugu. Kwahiyo kama wanyama hawa watawafanya wenzao wawe wanazika, wajue kwamba na wao lazima watakuwa wanazika au wanazikwa, kwa sababu imeandikwa, "Kipimo kile kile mtakachowapimia wenzenu ndicho mtakachopimiwa na ninyi." [/FONT] [FONT=&amp]

Wanahabari na walengwa wengine wote wa unyama huu, fahamuni kwamba Watanganbyika wote wapo pamoja na niyi, na zaidi sana Mwenyezi Mungu, hivyo unyama huu ni ishjara ya kwisha kabisa CCM, Chama cha Majambazi. [/FONT] [FONT=&amp]Dawa yas usalama ni kujiuzulu Bwana Kikwete nha kuwafikisha wote waliohusika na unyama huu mbele ya sheria maramoja, kwa sababu wote wanajulikana. Saa ya ukombozi ni sasa![/FONT]

[FONT=&amp]Democratic Party [/FONT]


[FONT=&amp]Mch. C. Mtikila[/FONT]
[FONT=&amp]MWENYEKITI [/FONT]
 

Attachments:

M

Malipo kwamungu

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Messages
575
Points
195
Age
58
M

Malipo kwamungu

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2012
575 195
Napita tu huyu mtumishi bado yupo!!
 
Mangaline

Mangaline

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2012
Messages
1,051
Points
0
Age
54
Mangaline

Mangaline

JF-Expert Member
Joined May 19, 2012
1,051 0
Ulimwenguni dola nyingi zimeanguka. Dalili za kuanguka dola huwa zinaonekana miaka miwili, au hata mitatu kabla ya hitimisho la anguko lenyewe. Dalili kuu za kuanguka kwa dola huwa ni pamoja na:-
1. Viongozi kuonekana kama wana masikio, angawa huwa hawasikii (Viziwi)
2. Viongozi kuonekana kama wana macho, ingawa huwa hawaoni (Vipofu)
3. Viongozi kuonekana kama wana midomo, ingawa huwa hawawezi kusema (Bubu)
4. ......................................................................................................................
5. ....................................................................................................................
6. .....................................................................................................................
Tafadhali endeleza dalili nyingine, na ukiweza bashiri dola zinazo onesha dalili za kuanguka.
 

Forum statistics

Threads 1,285,456
Members 494,621
Posts 30,862,989
Top