Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 63,594
- 107,547
Katika miaka 65 ya utawal wake sifa na majivuno ya CCM haikupaswa kuwa kumiliki dola na majeshi yake na kuwapakiza wanachama wake masikini kwenye mabasi kuhudhuria mikutano ya chama chao.
Katika miaka 65 ya kuwepo madarakani wastani wa kipato cha Watanzania ni duni sana kwa wastani wa $1,300
CCM inajivunia nini ikiwa zile nchi zote zilizokuwa sawa na Tanzania kiuchumi miaka ya 1960 kama Korea Kusini, Malysia, Singapore na Vietnam leo ni nchi tajiri zinazotupa msaada na teknolojia tena zikiwa zimepigana vita kubwa au kuwa na misukosuko mikubwa ya siasa ?
CCM inajivunia nini kumiliki dola ikiwa nusu ya raia wa nchi ni masikini na waliobaki wengi wao bado wanaishi maisha ya kuungaunga na wengine hadi watoke kila siku ndio wale!
CCM inajivunia nini ikiwa pamoja na mito yote na maziwa tuliyo nayo maji safi ya bomba sehemu kubwa ya nchi ni tatizo kubwa na ndoto na walichobaki nacho CCM sasa hivi ni kuweka takwimu za uongo tu kuhusu hali ya upatikanaji wa maji!
Miaka 65 ya CCM ajira kubwa za raia mijini ni vibarua, bodaboda, wapiga debe, wamachinga huku kukiwa na uhaba mkubwa wa wataalamu kila sekta kuanzia madaktari mpaka walimu.
CCM kumiliki dola wala haina maana yoyote kwa raia wengi wa Tanzania kwa zaidi ya 80%, wanufaika halisi wa dola kumilikiwa na CCM ni kakikindi kadogo tu cha watawala, matajiri wa tenda na rasilimali za nchi na network yao ya wabeba mikoba na machawa. Raia wengine wote CCM haijawa na msaada kwao au zaidi sana imewaumiza tu.