Ndugu, nina maoni tofauti na kauli ambayo kadiri yangu inaakisi woga usio na msingi wala uthibitisho. Hivi tunapokalia kusema CHADEMA haijajipanga kuchukua uongozi wa nchi tuna maana gani? Je, tunataka tumuone mtu akifanya kazi ya waziri mkuu wakati hajawa bado? Je, lini kikwete, kabla ya kuapisha aliwahi kuonyesha umahiri katika uraisi hata ikawa ndio kigezo cha kumchagua? Na kama ccm inayoongoza sasa ndiyo ilijipanga vizuri kwa kushika dola, kwa hali ilivyo sasa, basi sioni kwanini tuseme chadema haijajipanga. Upo msemo unasema, kanzu haimfanyi mtu kuwa padri au shehe, hawa wanajulikana kanisani au msikitini kwa shughuli zao katika mahali wanapofanyia kazi. Utendaji huu wa akina Mulugo, Pinda, Ngeleja, ndio tuseme ccm ilijipanga jamani? Mimi nadhani katika mabadiliko suala la kuthubutu pia ni la muhimu sana, hatuwezi kusubiri mpaka tuwe na uhakika wa 100% , ambayo haitapatikana, eti ndio tuseme chama kimejipanga. Tuache woga, tuthubutu, kwani hata hiyo chadema ikifanya vibaya, haitakaa hapo milele. Kutafuta evidentia rei kutatugharimu sana na kufanya maisha yetu kuwa magumu zaidi. Twende na hii evidentia credibilitatis, kwasababu nafasi ya kubadili tunayo. Tena basi sasa tunao mchakato wa mabadiliko ya katiba tujilinde kwa kupendekeza kuwa wananchi wapewe fursa ya kuitathmini serikali yao ndani ya kipindi cha utawala wake kwa njia ya kura ya maoni. Hapa atakayeleta gozi gozi anatolewa wakati wowote. Kwa pamoja tutashinda. Naomba kuwakilisha.