Kuanguka kwa CCM: Kutimilika kwa Unabii...

  • Thread starter Mzee Mwanakijiji
  • Start date

mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Messages
3,393
Points
1,250
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2013
3,393 1,250
na CCM wametumia swala la kuwatishia wananchi kwa kudhani watanzania ni wa mwaka arubaini na saba(1947 )baada ya vita vya pili vya dunia maana dunia yote ilikuwa inaogopa vita na something that relating to that
Mbona mimi sijawahi kutishwa wewe unazungumzia watanzania gani wanaotishwa?

tumia akili vizuri watanzania wao ndiyo wanajua chama kipi kinawafaa na siku wakitaka kubadili chama wenyewe ndiyo wataamua siyo wewe mtu wa bavicha.
 
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Messages
3,393
Points
1,250
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2013
3,393 1,250
Jitahidini kuweka kumbukumbu zenu sawa ili siku ikifika tuweze kukumbushana mtapata aibu kweli siku ikifika msijifike.
Polisi siyo wepesi kiasi hicho na vyombo vya dola kwa ujumla viko imara wewe kama umetumwa kufanya fujo tutakuzika mapema sana.
 
N

notradamme

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
2,012
Points
1,195
N

notradamme

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2010
2,012 1,195
HATA MWINGIRA NAYE NI NABII..
NA HATA NENO LAKE LINAWEZA KUITWA UNABII...
Huu unabii una sauti tamu sana na yenye kupumbaza haswa kwa wale wasio na fikra pevu na wanaoishi kwa kujidanganya.
naapa na mungu yu shahidi yangu"" NI LAZIMA ITAFIKA SIKU CCM ITASHINDWA NA NINA HAKIKA ITASHINDWA KWA AIBU NA HUENDA KUSHINDWA KWAKE KUKAWA NDIO MWISHO KABISA WA CHAMA HICHO""
Lakini je ukweli huo ninaoukiri unatosha kunipumbaza kiasi cha kujidanganya kuwa ETI ULE MUDA NDIO UMESHAWADIA??!!! Je ninahaja ya kujitia upofu wa kiakili kiasi cha kujipa tumainikuwa kiasi cha miezi NANE ijayo inatosha kuutimiza huu unabii wa MM!!!???
NASEMA HAPANA.. HAPANA SI KIDOGO BALI NI HAPANA YA KWELI NA DHATI.
Huenda wajinga walio wengi wanaoishi kwa kujidanganya, wanaweza wakadhani matokeo ya uchaguzi uliopita hivi punde wa serikali za mitaa ni dalili tosha la anguko la ccm, lakini wameshindwa kabisa kufanya SCIENTIFIC ANALYSIS ya jinsi ambavyo CCM bado inakubalika na na inahitaji nguvu kubwa na kutokata tamaa ili kuiondoa madarakani.
pamoja na udhaifu mkubwa kabisa wa kiutendaji wa chama na serikali yake iliyoko madarakani, lakini bado watanzania wana imani kubwa sana kwa CCM na hii inadhihirishwa na kiwango cha ushindi katika huo uchaguzi husika.
ESCROW..
MFUMUKO WABEI..
NGUVU KUBWA ILIYOTUMIWA NA WAPINZANI KATIKA KUWAFIKIA WANANCHI..
BUNGE LA KATIBA na mengineyo, yamechangia kwa kiasi kikubwa sana matokeo kuwa vile na kwa ushindi ule, ccm inadhihirisha jinsi ambavyo ina nguvu isiyomithilika.
kikubwa kinacho/kitakacho uumiza upinzani ni KUISHI KWA DHANA HUKU WAKIEPUKA HALI HALISI. huenda hata huu uzi wa MM ni mkakati wa government agents wa kuupunguza nguvu upinzani kwa kujaribu KUWAVISHA KILEMBA CHA UKOKA KWA KUWAAMINISHA KUWA sasa mumeiva na mko tayari kuchukua nchi wakati hali halisi haiko hivyo.hii itapelekea upinzani kubweteka na kudhani kazi iliyo mbele yako ni ndogo isiyohitji nguvu na akili nyingi.
niko vijiweni kila siku na hili nitakalosema hapa kila mmoja wetu anaweza akawa shahidi kama atasimamia ukweli.
na jambo lenyewe ni kwamba" tunapojadili wagombea watarajiwa kutoka CCM, hata wafuasi wa upinza wanaonyesha kwa dhati kabisa kupitia maongezi yao kuwa Raisi ajaye atatoka CCM(NDANI YA MIOYO YAO WANAAMINI HIVYO)
NINADHANI WOOTE TUNGEFUATA USHAURI WA ZZK kuhusu systematic growth.
kwamba upinzani kama block moja ingejipa projections kwa uchaguzi ujao kwa kufanya intensive analysis nchi nzima ya kutambua tunakubalika wapi na kwa kiasi gani then kujipanga kuchukua majimbo kiasi gani katika maeneo gani na tuwe na uhakika wa kupata asilimia ngapi za kura za uraisi. baada ya analysis hiyo ufuate mkakati wa kuhakikisha PROJECTIONS zinasimamiwa na kufikia asilimia sio CHINI YA 95%. BAADA YA HAPO NI KUJIPANGA KUICHUKUA NCHI BAADA YA MIAKA MINGINE 5 AU KUMI.
Bila mikakati ya kiutu uzima namna hii na mkabaki na mikakati ya kuombea kudra toka kwa mungu, naapa sio mwaka huu bali hata baada ya miaka 50 CCM itaendelea kututawala. HATUNA HAJA ya kujipa matumaini hewa ambayo mwishowe yatawafanya hata wenye mioyo migumu kukaa mbali kabisa na siasa
 

Forum statistics

Threads 1,284,731
Members 494,236
Posts 30,837,859
Top