Chizi Fureshi
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 1,718
- 463
Kupitia kituo cha Television cha ITV, kazi ya kuagwa kwa gwiji la Sheria na Siasa ndo imeanza muda huu. Tufuatilie...
Marehemu Sengondo Mvungi 1952 - 2013
-----------------------------------------
Marehemu Sengondo Mvungi 1952 - 2013
-----------------------------------------
Nami nipo hapa Karimjee kumuaga mwalimu wangu, rafiki yangu...alikuwa mtu mwema na mwenye upendo wa kweli. RIP Dkt. Sengondo Mvungi.
Mwanadamu kumbuka kuwa u-mavumbi wewe na mavumbini utarudi. Ni maneno yaliyoko katika wimbo unaoendelea sasa... Pumzika kwa amani - Dr. Edmund Sengondo Mvungi.
profesa costa mahalu: DR MVUNGI NI SHUJAA NDIO MWASISI WA SERIKALI TATU
Akitoa salamu kutoka UB University of Bagamoyo amesema Dk. Mvungi ni shujaa yeye ndio aalipigania uwepo serikali tatu pia alipewa jina la utani yaani 'nguto' means leopard au chui.
Source ITV news
Waraka wa Mh. Rais Dr. J.M.Kikwete unsomwa kwa niaba yake na Makamu wa Rais. ...Dr. E.S.A.Mvungi alikuwa mzalendo wa kweli na mahili katika fani, ndo maana sikusita kumteuwa kuwa mjumbe wa tume...
Sala fupi ya Buriani inatolewa na Padri Mvungi...
MBATIA - Tukishampumzisha Dr. E.S.A. Mvungi kwa nguvu hiyohiyo tuitumie kulinda uhai wa wananchi wetu. Mh.Mbatia.
Mvua nayo inanyesha hapa kusindikiza mwili wa mpendwa Mvungi
JK: "...ni msiba wetu sote, majonzi yenu ni yetu sote...sote tumshukuru Mungu kwa fursa ya kuishi na marehemu..."
Ujumbe wa padri Kabla ya kulala hakikisha umelala baada ya kutubu makosa(dhambi) kwa Mungu kqma kuna mtu kakuudhi/kakukosea msamehe nawe kama umemkosea omba akusamehe ili ulale na Amani yaeezekana ukawa ni mlalo wako wa mwisho hapa duniani
Wadau,
Nimeipenda hii kauli ya Prof Costa Mahalu,Ametutaka watanzania tumuenzi Dk Sengondo Mvungi kwa kukubali kuwa na serikali tatu katika katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema, Dk Mvungi alisimamia sana suala hilo na kutetea msimamo wake huo,
my take:
Je wale wanaopinga mfumo huu wa serikali tatu watamuenzi kweli Dk Mvungi au itakuwa ni chanzo cha mifarakano na kupotea kwa amani katika nchi yetu? Nawaomba wenzangu CCM tumuenzi mjumbe huyu ambaye sasa tunakwenda kumzika.
Prof: Lipumba Dr. Sengondo Mvungi alitutetea sisi Marais tuliochakachuliwa
Prof, Akitoa salamu za rambimbi katika shuhughuli za kuaga Mwili wa Marehemu Dk. Sengondo Mvungi.
Amekiri kumfahamu 1995 wakati walikuwa wanataka kufungua kesi kupinga uchakachuaji wa kura mwaka huo na kuendelea.
Mwaka 1995 walishindwa kuendelea na kesi kwa kuwa Mwenzao Lamwai aliingia mitini.
Amekiri kuwa wao ni Marais waliochakachuliwa kura zao.
Naomba kuwasilisha
Wanajamvi
Mhe. Mwingulu akitoa salamu za Chama kuaga Mwili wa Marehemu Dk. Mvungi.
Amekiri katika Salamu kuwa mambo ya ukatili yanayotokea Tanzania Serikali ichukue hatua.
Lakini yeye anaona, "Roho ya mauti na Mapepo"
Ndo yanafanya haya.
Dr. Mvungi alikuwa tayari kwenda kutetea Rasimu ya Katiba katika Bunge la Katiba - Alfred Masako.
Mkuu ata mimi sijamwelewa Masako alikuwa anamaanisha nini apo?
Kwani bunge lililopita si wamekubaliana kuwa ukomo wa tume ya mabadiliko ya katiba ufike kabla ya kuanza bunge la katiba? Sasa hapo napata kigugumizi kuwa angetetea vp hiyo rasimu?
Shuhuli za kuuaga mwili zimeisha na jeneza limefungwa na mvua imekatika kabisa, Itv nao wanafunga kipindi kurusha hii shuhuli live. Mimi pia nalog off.
MUNGU ALITOA NA SASA KATWAA JINA LAKE LIBARIKIWE
Shughuli imekamilika, asanteni Watanzania. Mtetezi wa Serikali tatu katangulia sisi nyuma yake. Asanteni wana JF na hasa mods kwa kuboresha post #1 .