Kuagwa kwa Marehemu Dk. Mvungi - ITV

Kuagwa kwa Marehemu Dk. Mvungi - ITV

Mvungi atakumbukwa kwa katiba mpya. Yafaa tumuenzi kwa mambo yafuatayo
1.0 Waziri kutokuwa mbunge,
2.0 Viti maalumu kutokuwepo,
3.0 Kupunguza baraza la mawaziri
4.0 Viongozi wote waliwahi kushika nafasi basi wasiishi nje ya nchi baada ya ukomo wa uongozi wao
5.0 Serikali ihakikishe katika kila rasilimali ya ardhi basi inamiliki japo 20% ikiwemo gesi na madini.

umesahau kidogo, serikali 3
 
Docta mvungi alikuwa mjumbe wa tume, kila mjumbe ana nafasi yake,lakini mvungi alikuwa ni zaidi ya mjumbe...
 
Eliuter aliuliwa, profesa mwakusi aliuliwa, dk Mvungi ameuliwa! Hawa wote ni WAKRISTO. Dk Ulimboka aliteswa, Absalom aliteswa, Mwangosi aliuliwa. Hawa wote na wengine niliowasahau wamefanyiwa hayo na nchi! WAKRISTO HAWA WAMEKOSA NINI? Je ni kwa sababu ya kuwa watetezi wa wanyonge?

Naona unataka kubadilisha hali ya hewa
 
Naomba kurudia tena, twamwomba mwenyezi Mungu, awape familia ya marehemu moyo wa uvumilivu..Warioba anaonyesha kulia.. anaona kabisa kifo chake ni cha kupangwa tu!
 
kama tutakuwa kimya basi wengi tutwapoteza yatupasa tuamke usingizini maana hali inatisha kwa kweli
 
Kuna maamuzi ya kifisadi ameyafanya ndio yamemfanya asishiriki chakula cha bwana, ama sivyo angedondoka mbele ya kadamnasi !!!

dhambi ya wapigwe tu inamtafuna na huyu anaweza kuwa ni mmoja wa watuhumiwa kwa kauli yake ya wapigwe tuuuu,shame on him
 
Mvungi atakumbukwa kwa katiba mpya. Yafaa tumuenzi kwa mambo yafuatayo
1.0 Waziri kutokuwa mbunge,
2.0 Viti maalumu kutokuwepo,
3.0 Kupunguza baraza la mawaziri
4.0 Viongozi wote waliwahi kushika nafasi basi wasiishi nje ya nchi baada ya ukomo wa uongozi wao
5.0 Serikali ihakikishe katika kila rasilimali ya ardhi basi inamiliki japo 20% ikiwemo gesi na madini.

umesahau kidogo, serikali 3
 
Mh.dr.Bilali anatoa salamu za serikali sasa,anasema amemwakilisha rais na anasoma barua alioiacha JK kabla ya kwenda Srilanka,Colombo.
 
Waraka wa Mh. Rais Dr. J.M.Kikwete unsomwa kwa niaba yake na Makamu wa Rais. ...Dr. E.S.A.Mvungi alikuwa mzalendo wa kweli na mahili katika fani, ndo maana sikusita kumteuwa kuwa mjumbe wa tume...

Sala fupi ya Buriani inatolewa na Padri Mvungi...
 
Kabla ya Mauti kumkuta Dr. Mvungi siku ya Ijumaa alipewa jukumu la Kufanya utafiti wa jambo ambalo lilikuwa linahitaji umakini na alikamilisha kazi hiyo na kukabidhi na hiyo ndiyo kazi yake ya mwisho ndani ya tume. Swali Je ni huo utafiti alioufanya ndiyo umechangia Mauti yake?
 
Sengodo kweli umekwendaa!!kapumzike kwa amani Dr!inaumiza na kusikitisha na kuhuzunisha sana
 
JK: "...ni msiba wetu sote, majonzi yenu ni yetu sote...sote tumshukuru Mungu kwa fursa ya kuishi na marehemu..."
 
Back
Top Bottom