KRA vs TRA: Kwanini Kenya inakusanya kodi mara 3 ya Tanzania

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,493
2,000
Upo vizuri sana mkuu.. naoenda unavyo leta fact.
Kama nilivyosema, hadi sasa TRA inakusanya 15% ya GDP badala ya 24% bado TRA ipo mbali sana kufikia 24% ya GDP, japo lengo sio kufikia 24%, wastani mzuri duniani ni kufikia 20%. Kikwete aliacha tunakusanya 11% ya GDP, kwahiyo tunapiga hatua taratibu.

KRA bado ina matatizo mengi, kinda see ni kutotanua base ya kukusanya kodi, matumizi ya tehama na ubunifu mdogo wa uongozi wa TRA.

Ila kama tunataka kulinganisha na KRA. Hatupaswi kulinganisha kiwango cha pesa zinazokusanywa kwasababu uchumi wa Kenya na Tanzania ni tofauti.

Mfano ni nchi ya Botswana ambayo makusanyo yao kwa mwaka hayafiki hata 6trl, lakini katika ukusanyaji kodi, ndio nchi inayofanya vizuri zaidi Africa, wanakusanya 22% ya GDP yao, hivyohivyo kwa Rwanda.
 
big-diamond

JF-Expert Member
May 23, 2009
408
500
Kaka upo nje kabisa ya mada, wewe ndiye unayezungumza siasa, TRA ipo na matatizo ya kiutendaji kama ilivyo KRA.

Kawaida huwezi kulinganisha makusanyo ya nchi mbili zenye uchumi tofauti kwa kuangalia kiwango kilichokusanywa, badala yake unaangalia ni asilimia ngapi ya GDP ya hiyo nchi imewezwa kukusanywa, hapo ndio unaweza kupima ufanisi wa makusanyo ya kodi.

Kawaida nchi inapaswa kukusa 24% ya GDP yake kama kodi, Kama nchi ikifanikiwa kukusanya 24% ya GDP, hiyo ndio 100% ya ukusanyaji kodi, lakini hakuna nchi ambayo imeshafikia huko, nchi nyingi zinazofanya vizuri zipo kati ya 18 to 21%.

Kwa mara ya mwisho data za BoT zilionyesha Tanzania tunakusanya 15% na Kenya 16 %(sikumbuki vizuri). Kwahiyo hatupaswi kulinganisha kiwango badala yake tulinganishe % ya ukusanyaji wa mapato
Nimekusoma kaka, lakini hebu tuangalie pale Mamlaka yetu hii ingejikita katika maboresho ya utendaji na kuachana na siasa..

Maono yangu mimi, kuna kuna sababu ndogo ndogo na huwa kuna sababu mzizi, ambao ukifanikiwa kuujua ukaung'oa basi ule mti wa tatizo utanyauka.

TRA wanajitahidi, lakini tunaangushwa na viongozi wetu.

KUMBUKA: Hao TRA kwa sasa wanacheza kulingana na mdundo wa wakuu wa serikali na sio kulingana na maelekezo ya taaluma zao au mahitaji ya soko.

TRA itengwe na siasa, ipewe nguvu ya kukemea pale inapoingiliwa na wanasiasa.
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,493
2,000
Well said..

Mkuu Mr zero brain naomba nikukunbushe bapa sio facebook
We level yako ni kina Lissu zero brain wenzio, sio unakuja kuleta uzumbukuku wako hapa utegemee utakutana na wapiga lami deki na watanua vidole kama kule kwenye jukwaa la siasa, wewe ni zero brain sababu hata kusoma hujui
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
17,739
2,000
Hakuna anaependa kulipa kodi hata ingekua ndogo kiasi gani!! Hapa agenda kuu ni kwnn KRA wanakusanya zaidi ya TRA,Hata izo fedha zilizokusanywa hazijatolewa kwa dhati ni kwasababu ya sheria kanuni na taratibu za nchi.
Kwasababu Kenya uchumi wao ni mkubwa, kumbuka kodi inatozwa kutokana na % ya mapato ya nchi, mapato yakiwa makubwa hiyo % inakua ni pesa nyingi.

Muhimu ni kulinganisha ufanisi kati ya TRA na KRA, sio kiwango cha jumla ya fedha kilichokusanywa, hilo ni kosa.

Tujiulize KRA inakusanya % ngapi ya GDP ya Kenya, na TRA inakusanya % ngapi ya GDP ya Tanzania?
 
big-diamond

JF-Expert Member
May 23, 2009
408
500
Kosa kubwa TRA, unaulizwa unauza ngapi kwa siku!! KRA unaulizwa unapata faida gani kwa siku na hiyo faida ndio mnagawanya kwa kodi mbalimbali ikiwemo KRA. Ni pesa kidogo ila watu hawakwepi kwani wanatendewa haki. Tz unakadiriwa kwa kukomolewa na watu wanakwepa. Kinachokwepwa ndicho KRA wanatuzidi nacho
Nasema kila siku, TRA ni adui wa wafanya biashara.

Wafanyabiashara ni adui wa TRA.

Wakati wenzetu wanaona sifa kulipa kodi, sisi tunaona sifa kukwepa kodi.

Chanzo cha yote haya ni SIASA kuingizwa kwenye UKUSANYAJI na MATUMIZI YA MAPATO.
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,493
2,000
Naton Jr,

Soma hapa.
20200917_092539.jpeg
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
17,739
2,000
[mention]joto la jiwe [/mention] huyu shemegi yangu [mention]MK254 [/mention] anapenda ugomvi sana sijui ana matatizo gani watu tunasimama kukuza mawazo ili Afrika mashariki tusonge mbele yeye analeta utani
Hata mimi ninamshangaa sana, ukweli lazima niuseme, huyu jamaa amechangia sana kunifanya niishambulie Kenya, anapenda sana kutengeneza chuki badala ya maelewano.
 
Naton Jr

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
4,992
2,000
Nasema kila siku, TRA ni adui wa wafanya biashara.

Wafanyabiashara ni adui wa TRA.

Wakati wenzetu wanaona sifa kulipa kodi, sisi tunaona sifa kukwepa kodi.

Chanzo cha yote haya ni SIASA kuingizwa kwenye UKUSANYAJI na MATUMIZI YA MAPATO.
Siasa imeingizwaje kwenye mfumo wa kikodi?
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,493
2,000
Upo sahihi lakini hata hicho kiwango TRA inakusanya .. unakusanya kutoka base ndogo sana kwa sababu unatoza kodi kubwa.

Mfano

KRA: Capital Gain Tax ni 5%
TRA : Capital Gain Tax ni 10%

Ndio maana tunasema makusanyo ya TRA yamebeba risk kwa sababu yapo kisiasa.

Kama TRA watatoza kodi sahihi kwa wafanya biashara maana yake hatuwezi kufikia hata kiwango cha sasa hadi watakapo kuza base ya walipa kodi na kufikia walau 80% ya wanao stahili kulipa kodi.

Kuna maeneo mengi sana ambayo hayaja guswa na kama yakiguswa TRA inaweza kuwa na nafasi kubwa sana katika maendeleo ya nchi hii.
Kwasababu Kenya uchumi wao ni mkubwa, kumbuka kodi inatozwa kutokana na % ya mapato ya nchi, mapato yakiwa makubwa hiyo % inakua ni pesa nyingi.

Muhimu ni kulinganisha ufanisi kati ya TRA na KRA, sio kiwango cha jumla ya fedha kilichokusanywa, hilo ni kosa.

Tujiulize KRA inakusanya % ngapi ya GDP ya Kenya, na TRA inakusanya % ngapi ya GDP ya Tanzania?
 
tonnylee

Member
Aug 11, 2013
22
45
Kuna vitu vinatia aibu.. mtu unatoka huko unatafuta ulipe kodi haraka unadhani kuna namna rahisi unakutana na menu ambazo hazina hata mashika.

Kuna tatizo kwa wanao ongoza kitengo cha ICT TRA.. inawezekana yupo busy sana kiasi kwamba vitu vidogo kama hivi hajawahi kuwaza kwamba vina impact kubwa sana kwenye kazi za TRA.

TRA inahitaji mabadiriko makubwa kwenye matumizi ya tehama na siku wakilijua hilo watashangaa kazi zao zilivyo rahisi na makusanyo yatakavyo kua kwa haraka japo tunatambua tehama itaua mapato yao binafsi yale ya pembeni..
We unadhani hawalijui hili wanajua sana ila wamejawa na tamaa tu, kupenda kuwanyonya walipa kodi.

TRA amkeni amkeniiiiii
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
17,739
2,000
Nimekusoma kaka, lakini hebu tuangalie pale Mamlaka yetu hii ingejikita katika maboresho ya utendaji na kuachana na siasa..

Maono yangu mimi, kuna kuna sababu ndogo ndogo na huwa kuna sababu mzizi, ambao ukifanikiwa kuujua ukaung'oa basi ule mti wa tatizo utanyauka.

TRA wanajitahidi, lakini tunaangushwa na viongozi wetu.

KUMBUKA: Hao TRA kwa sasa wanacheza kulingana na mdundo wa wakuu wa serikali na sio kulingana na maelekezo ya taaluma zao au mahitaji ya soko.

TRA itengwe na siasa, ipewe nguvu ya kukemea pale inapoingiliwa na wanasiasa.
Kaka katika kitu kinachomuumiza kichwa Magufuli ni TRA na Wizara ya mambo ya ndani na BoT, wewe mwenyewe umemsikia mara kadhaa Magufuli akichanganyikiwa kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa TRA, katika kipindi cha uongozi wake wa miaka 5. amebadilisha makamishina wakuu 5, wastani wa kamishna mkuu mmoja kila mwaka , hii ni dalili kwamba hakuna utendaji mzuri TRA.

Kaka tatizo la TRA lipo kwa wetendaji kuwa na uwezo mdogo, kukosa ubunifu na kutokuwepo na uongozi imara, bado wafanyakazi wengi wa TRA ni mangi meza, sidhani Kama kuna siasa.
 
ipyax

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,622
2,000
Shida kubwa ya TRA ni kwamba sio taasisi huru ambayo inajiendesha yenyewe bila kuingiliwa na wanasiasa . Nafasi ya bosi wa TRA ilifaa iwe inatangazwa watu wanaomba kuajiriwa kwa mkataba wa muda fulani huku wakija na mbinu za kuiboresha hii taasisi ili iende na waakati. Pale ambapo TRA inacheza mziki wa wanasiasa iwe Rais,Waziri, RC, DC au mbunge basi hiyo taasisi haiwezi kujiendesha kwa weledi.

Tutalia na kupiga kelele lakini wanasiasa (viongozi) Hawaii tayari kuichia TRA ijiendeshe yenyewe kwa sababu inatumika kama fimbo kuwachapia wasiowapenda,kupata cheap political milage nk. Mungu ibariki Tanzania.
 
Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
32,489
2,000
Kaka katika kitu kinachomuumiza kichwa Magufuli ni TRA na Wizara ya mambo ya ndani na BoT, wewe mwenyewe umemsikia mara kadhaa Magufuli akichanganyikiwa kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa TRA, katika kipindi cha uongozi wake wa miaka 5. amebadilisha makamishina wakuu 5, wastani wa kamishna mkuu mmoja kila mwaka , hii ni dalili kwamba hakuna utendaji mzuri TRA.

Kaka tatizo la TRA lipo kwa wetendaji kuwa na uwezo mdogo, kukosa ubunifu na kutokuwepo na uongozi imara, bado wafanyakazi wengi wa TRA ni mangi meza, sidhani Kama kuna siasa.
Hivi mirahaba na kodi za madini hukusanywa na TRA au huenda directly Hazina? maana hili gap la kuzidishwa mara tatu ni kubwa!
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,049
2,000
Kama nilivyosema, hadi sasa TRA inakusanya 15% ya GDP badala ya 24% bado TRA ipo mbali sana kufikia 24% ya GDP, japo lengo sio kufikia 24%, wastani mzuri duniani ni kufikia 20%. Kikwete aliacha tunakusanya 11% ya GDP, kwahiyo tunapiga hatua taratibu.

KRA bado ina matatizo mengi, kinda see ni kutotanua base ya kukusanya kodi, matumizi ya tehama na ubunifu mdogo wa uongozi wa TRA.

Ila kama tunataka kulinganisha na KRA. Hatupaswi kulinganisha kiwango cha pesa zinazokusanywa kwasababu uchumi wa Kenya na Tanzania ni tofauti.

Mfano ni nchi ya Botswana ambayo makusanyo yao kwa mwaka hayafiki hata 6trl, lakini katika ukusanyaji kodi, ndio nchi inayofanya vizuri zaidi Africa, wanakusanya 22% ya GDP yao, hivyohivyo kwa Rwanda.
Kumbe JPM kwa miaka 5 ameongeza 4% kutoka pale tulipo achwa na JK, pamoja namajigambo bado makusanyo ya TRA yako chini yakiwango, kazi nimoja kwa CCM tenganisha siasa na uchumi wa nchi ndomtaweza kuona performance ya sector ya fedha
 
Naton Jr

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
4,992
2,000
2019-2020
Zimejumuisha maduuli yote ya serikali kutoka maeneo kama national parks, wizara ya kilimo, wizara ya nishati na agencies nyingine za serikali ambayo mifumo yake kikodi haiintercept na TRA?

Ya Kenya ulioweka hapo ukasema imetuzidi mara 3 imejumuisha hayo yote, sasa na kuuliza na ya Tanzania imejumuisha? 🚮🚮🚮🚮
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom