joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Mimi wasiwasi wangu ni neno "kisiasa", sijui hili neno linaingiaje. Tatizo kama ulilosema la kuwa na base ndogo la walipa kodi, hilo ndio tatizo kubwa la TRA ambalo Magufuli amekuwa akiwapigia sana kelele TRA, amekwenda mbali hadi kuanzisha vitambulisho vya wamachinga na kuanzisha Masoko ya madini ili kupanua"tax base".Upo sahihi lakini hata hicho kiwango TRA inakusanya .. unakusanya kutoka base ndogo sana kwa sababu unatoza kodi kubwa.
Mfano
KRA: Capital Gain Tax ni 5%
TRA : Capital Gain Tax ni 10%
Ndio maana tunasema makusanyo ya TRA yamebeba risk kwa sababu yapo kisiasa.
Kama TRA watatoza kodi sahihi kwa wafanya biashara maana yake hatuwezi kufikia hata kiwango cha sasa hadi watakapo kuza base ya walipa kodi na kufikia walau 80% ya wanao stahili kulipa kodi.
Kuna maeneo mengi sana ambayo hayaja guswa na kama yakiguswa TRA inaweza kuwa na nafasi kubwa sana katika maendeleo ya nchi hii.
Kushindwa kwa TRA kupanuo tax base ndiko kunakowafanya kutoza kodi kubwa Kama hiyo uliyosema, sasa unaposema wanafanya kazi kisiasa unamaanisha nini?. Lakini tusisahau kwamba wananchi wakenya ndio raia wanaolipishwa kodi nyingi kuliko raia wa nchi yoyote hapa mashariki na kusini mwa Afrika.