KRA vs TRA: Kwanini Kenya inakusanya kodi mara 3 ya Tanzania

Well said mkuu..
Tafadhali hili sio lengo la huu mjadala, lengo ni kuonyesha mapungufu ili watu wajifunze, wacha kutoa conclusions ambazo huna uhakika nazo, hadi sasa tumezungumzia maeneo mawili tu, ya bandari za Mombasa vs Dar.na TRA vs KRA, subiri kuna maeneo mengi yanakuja, sijui kama hutofuta hii kauli yako.
 
Tabutupu,

Hapa mataga wa lumumba kwa Humphrey Polepole hawawezi kuelewa hata kidogo, tufike mahala kama taifa tujifunze, hii tabia ya kushangilia upuuzi unaofanywa na ccm hautatusaidia, matatizo ni mengi sana kwenye uendeshaji wa serikali chini ya CCM mambo ni hovyo kabisa.
 
Kuna vitu vinatia aibu. Mtu unatoka huko unatafuta ulipe kodi haraka unadhani kuna namna rahisi unakutana na menu ambazo hazina hata mashika.

Kuna tatizo kwa wanao ongoza kitengo cha ICT TRA.. inawezekana yupo busy sana kiasi kwamba vitu vidogo kama hivi hajawahi kuwaza kwamba vina impact kubwa sana kwenye kazi za TRA.

TRA inahitaji mabadiriko makubwa kwenye matumizi ya tehama na siku wakilijua hilo watashangaa kazi zao zilivyo rahisi na makusanyo yatakavyo kua kwa haraka japo tunatambua tehama itaua mapato yao binafsi yale ya pembeni.

Niliwahi kujiuliza ile vacancies pale ya kazi gani. Umetisha mkuu!
 
Tabutupu,

bishana na takwimu

Screenshot_2020-09-17-09-03-33.jpg
Screenshot_2020-09-17-09-03-40.jpg
 
1. TRA imekaa kisiasa, inaendeshwa kwa maslahi ya chama na sio Watanzania.

2. Wanasiasa wanatuambia tukiwachagua wao watatuletea maendeleo kwa kutumia pesa zao.

3. Wananchi wanachukia kulipa kodi kwa kuwa hawana haki kwenye maamuzi ya matumizi ya kodi zao.

4. Wanasiasa wanatumia umasikini wetu na matatizo yetu kama mtaji wa kututawala.

NB: SIKU AMBAYO SERIKALI ITAANZA KUSEMA WAZI WAZI KUWA MAENDELEO HAYALETWI NA WANASIASA BALI NI KODI ZETU, NDIYO SIKU AMBAYO MAENDELEO YA KWELI YATAONEKANA
Kaka upo nje kabisa ya mada, wewe ndiye unayezungumza siasa, TRA ipo na matatizo ya kiutendaji kama ilivyo KRA.

Kawaida huwezi kulinganisha makusanyo ya nchi mbili zenye uchumi tofauti kwa kuangalia kiwango kilichokusanywa, badala yake unaangalia ni asilimia ngapi ya GDP ya hiyo nchi imewezwa kukusanywa, hapo ndio unaweza kupima ufanisi wa makusanyo ya kodi.

Kawaida nchi inapaswa kukusa 24% ya GDP yake kama kodi, Kama nchi ikifanikiwa kukusanya 24% ya GDP, hiyo ndio 100% ya ukusanyaji kodi, lakini hakuna nchi ambayo imeshafikia huko, nchi nyingi zinazofanya vizuri zipo kati ya 18 to 21%.

Kwa mara ya mwisho data za BoT zilionyesha Tanzania tunakusanya 15% na Kenya 16 %(sikumbuki vizuri). Kwahiyo hatupaswi kulinganisha kiwango badala yake tulinganishe % ya ukusanyaji wa mapato
 
Kwa uelewa wangu kama TRA iliweka lengo la kukusanya trillion 5 robo ya Oct -Dec 2019 na ikafanikiwa kukusanya 4.972 Trillions Sawa na 97% ni dhahiri kwamba hata wangekusanya kwa 100% bado isingezidi makusanyo ya KRA ,Malengo tofauti vyanzo tofauti ufanisi umeongezekena kulingana na lengo walilokua wamejiwekea.

Nadhan waibue vyanzo vipya vya kukusanya Mapato Huwezi kuwalaumu kwasababu wamefikia lengo Lao walilojiwekea
 
Upo sahihi lakini Je matatizo tunayo yajadili unaya onaje..

Ina maana kama tunakudanya kiwango sahihi kulingana na GDP tungeweza kufanya vizuri zaidi..

Japo siamini kwa sababu baada ya Rais Magufuli kuwa mkali nankubadilisha CG kila mara mapato yakapanda..

Hii ina maana kwamba bado Tanzania kuna room kubwa sana ya kufanya vizuri.

Sikuoni kama defensive ila najaribu kutoa mawazo.
Kaka upo nje kabisa ya mada, wewe ndiye unayezungumza siasa, TRA ipo na matatizo ya kiutendaji kama ilivyo KRA.

Kawaida huwezi kulinganisha makusanyo ya nchi mbili zenye uchumi tofauti kwa kuangalia kiwango kilichokusanywa, badala yake unaangalia ni asilimia ngapi ya GDP ya hiyo nchi imewezwa kukusanywa, hapo ndio unaweza kupima ufanisi wa makusanyo ya kodi.

Kawaida nchi inapaswa kukusa 24% ya GDP yake kama kodi, Kama nchi ikifanikiwa kukusanya 24% ya GDP, hiyo ndio 100% ya ukusanyaji kodi, lakini hakuna nchi ambayo imeshafikia huko, nchi nyingi zinazofanya vizuri zipo kati ya 18 to 21%.

Kwa mara ya mwisho data za BoT zilionyesha Tanzania tunakusanya 15% na Kenya 16 %(sikumbuki vizuri). Kwahiyo hatupaswi kulinganisha kiwango badala yake tulinganishe % ya ukusanyaji wa mapato
 
Kosa kubwa TRA, unaulizwa unauza ngapi kwa siku!! KRA unaulizwa unapata faida gani kwa siku na hiyo faida ndio mnagawanya kwa kodi mbalimbali ikiwemo KRA. Ni pesa kidogo ila watu hawakwepi kwani wanatendewa haki. Tz unakadiriwa kwa kukomolewa na watu wanakwepa. Kinachokwepwa ndicho KRA wanatuzidi nacho
 
Leta data za kweli.. 14 TR ndio makusanyo ya TRA..

Achana na huyo mpuuzi kachukua bajeti ya serikali anadhani ndio makusanyo ya TRA.

Pia hajui kwamba kuna mapato yasiyo ya kodi ambayo hayapiti TRA.

JF ya miaka hii mbona imejaza vilaza na wanabfacebook?
Hatugombani tunaeleweshana, tunaomba ushahidi wa hiyo 14trl. na hiyo 34trl ili tujue ni mwaka gani? Tafadhali tumia reliable sources za nchi zote mbili.
 
Kuna vitu vinatia aibu.. mtu unatoka huko unatafuta ulipe kodi haraka unadhani kuna namna rahisi unakutana na menu ambazo hazina hata mashika.

Kuna tatizo kwa wanao ongoza kitengo cha ICT TRA. Inawezekana yupo busy sana kiasi kwamba vitu vidogo kama hivi hajawahi kuwaza kwamba vina impact kubwa sana kwenye kazi za TRA.

TRA inahitaji mabadiriko makubwa kwenye matumizi ya tehama na siku wakilijua hilo watashangaa kazi zao zilivyo rahisi na makusanyo yatakavyo kua kwa haraka japo tunatambua tehama itaua mapato yao binafsi yale ya pembeni.
Kabisa mkuu
 
Hiyo 1.9 ndio the highest in history of TRA.

Haya tufanye ndio average pengine tuongeze iwe 2tr .. kwa mwaka si utakusanya just 24tr.

Hapo KRA wanakusanya 34 tr.

Leta story nyingine.
Nmeshaifafanua hii kwenye comment iliofuata
 
Kosa kubwa TRA, unaulizwa unauza ngapi kwa siku!! KRA unaulizwa unapata faida gani kwa siku na hiyo faida ndio mnagawanya kwa kodi mbalimbali ikiwemo KRA. Ni pesa kidogo ila watu hawakwepi kwani wanatendewa haki. Tz unakadiriwa kwa kukomolewa na watu wanakwepa. Kinachokwepwa ndicho KRA wanatuzidi nacho
Hakuna anaependa kulipa kodi hata ingekua ndogo kiasi gani!! Hapa agenda kuu ni kwnn KRA wanakusanya zaidi ya TRA,Hata izo fedha zilizokusanywa hazijatolewa kwa dhati ni kwasababu ya sheria kanuni na taratibu za nchi.
 
TRA imejaa wapigaji wengi, nakumbuka kuna video ambayo Magufuli aliita kikao na wana biashara, wakamfungukia ukweli wote namna huwa wanababaishwa, mtu una biashara yenye mtaji wa Tshs 10,000,000 unapotaka ulipe kodi jamaa wanapiga mahesabu wanakuambia una deni la TRA la Tshs 200,000,000

Unaambiwa ufanye maamuzi, uwape kitita fulani wakurekebishie au ukapambane mbele huko, haya yote aliambiwa rais wenu sijui kama kuna lolote la maana mlilifanya au ile ilikua show tu, tatizo mnapenda maonyesho maonyesho ya kisiasa halafu utendaji zero.

Pia Watanzania hamna desturi ya kupenda kulipa kodi, nilishangaa sana nikiwa Bongo kuona hamna mtu huhangaika kuagiza risiti ya EFD. Sasa hapo mnataka mshindane na sisi kiuchumi, pengo baina yetu litazidi kuongezeka mpaka basi.
Nafikiri tatizo TRA hawajawekeza kwenye elimu ya mlipa kodi, yawezekana hawataki kwa sababu watu wakielewa watashindwa kupiga.
 
Nmeshaifafanua hii kwenye comment iliofuata
Nadhani unachanganya makusanyo ya TRA na makusanyo ya serikali vs bajeti..

Nadhani kabla ya kupewa elimu ya mlipa kodi tunahitaji elimu jinsi serikali inavyo zipata fedha kwa ajili ya maendeleo na matumizi.mengine.

Ukweli.lazima tuuseme na hili lipo wazi juu ya utendaji wa TRA na ndio maana Rais Magufuli amekuwa karibu sana na TRA hata kufukuza CG kama watano ndani ya miaka 5.
20200917_092539.jpeg
 
Upo sahihi lakini Je matatizo tunayo yajadili unaya onaje..

Ina maana kama tunakudanya kiwango sahihi kulingana na GDP tungeweza kufanya vizuri zaidi..

Japo siamini kwa sababu baada ya Rais Magufuli kuwa mkali nankubadilisha CG kila mara mapato yakapanda..

Hii ina maana kwamba bado Tanzania kuna room kubwa sana ya kufanya vizuri.

Sikuoni kama defensive ila najaribu kutoa mawazo.
Kama nilivyosema, hadi sasa TRA inakusanya 15% ya GDP badala ya 24% bado TRA ipo mbali sana kufikia 24% ya GDP, japo lengo sio kufikia 24%, wastani mzuri duniani ni kufikia 20%. Kikwete aliacha tunakusanya 11% ya GDP, kwahiyo tunapiga hatua taratibu.

KRA bado ina matatizo mengi, kinda see ni kutotanua base ya kukusanya kodi, matumizi ya tehama na ubunifu mdogo wa uongozi wa TRA.

Ila kama tunataka kulinganisha na KRA. Hatupaswi kulinganisha kiwango cha pesa zinazokusanywa kwasababu uchumi wa Kenya na Tanzania ni tofauti.

Mfano ni nchi ya Botswana ambayo makusanyo yao kwa mwaka hayafiki hata 6trl, lakini katika ukusanyaji kodi, ndio nchi inayofanya vizuri zaidi Africa, wanakusanya 22% ya GDP yao, hivyohivyo kwa Rwanda.
 
@joto la jiwe huyu shemegi yangu @MK254 anapenda ugomvi sana sijui ana matatizo gani watu tunasimama kukuza mawazo ili Afrika mashariki tusonge mbele yeye analeta utani
 
Back
Top Bottom