KRA vs TRA: Kwanini Kenya inakusanya kodi mara 3 ya Tanzania

Naton Jr

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
6,091
2,000
Njoo na data mkuu,porojo nyingi hazitoshi lete ushahidi
unataka data ipi sasa? Zaidi ya hii?


2487631_tapatalk_1584017659452.jpeg
 

big-diamond

JF-Expert Member
May 23, 2009
407
500
1. TRA imekaa kisiasa, inaendeshwa kwa maslahi ya chama na sio Watanzania.

2. Wanasiasa wanatuambia tukiwachagua wao watatuletea maendeleo kwa kutumia pesa zao.

3. Wananchi wanachukia kulipa kodi kwa kuwa hawana haki kwenye maamuzi ya matumizi ya kodi zao.

4. Wanasiasa wanatumia umasikini wetu na matatizo yetu kama mtaji wa kututawala.

NB: SIKU AMBAYO SERIKALI ITAANZA KUSEMA WAZI WAZI KUWA MAENDELEO HAYALETWI NA WANASIASA BALI NI KODI ZETU, NDIYO SIKU AMBAYO MAENDELEO YA KWELI YATAONEKANA
 

tuusan

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
13,098
2,000
Hata hiyo yako mara mbili bado ni aibu.
Mara mbili bado haifiki pia,huwezi kukadiria pesa.Makusanyo siyanaendana na shughuli za uzalishaji mali katika eneo husika. Mfano hapa Tanzania kuna wafugaji wenye Ng'ombe kwa maelfu hao wakipata soko wanalipia kodi wapi? Kwa siku moja zinauzwa Ng'ombe, mbuzi kondoo ngapi ambazo hazilipiwi kodi?Bado serikali inamtambua mfugaji kama choka mbaya wakati huingiza fedha nyingi sana kuliko watu wengi wa kawaida. Kwann basi wasitengeneze utaratibu wa kukusanya walau 5% kwa kila Ng'ombe atakaeuzwa, pesa zipo nyingi zinazunguka hazisomeki kwenye mfumo.
 

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,524
2,000
Hata 1% inatosha..
Mara mbili bado haifiki pia,huwezi kukadiria pesa.Makusanyo siyanaendana na shughuli za uzalishaji mali katika eneo husika,Mfano hapa Tanzania kuna wafugaji wenye Ng'ombe kwa maelfu hao wakipata soko wanalipia kodi wapi?kwa siku moja zinauzwa Ng'ombe, mbuzi kondoo ngap ambazo hazilipiwi kodi?Bado serikali inamtambua mfugaji kama choka mbaya wakati huingiza fedha nyingi sana kuliko watu wengi wa kawaida.. Kwann basi wasitengeneze utaratibu wa kukusanya walau 5% kwa kila Ng'ombe atakaeuzwa ,Pesa zipo nyingi zinazunguka hazisomeki kwenye mfumo
 

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
20,292
2,000
Mara mbili bado haifiki pia, huwezi kukadiria pesa. Makusanyo siyanaendana na shughuli za uzalishaji mali katika eneo husika,Mfano hapa Tanzania kuna wafugaji wenye Ng'ombe kwa maelfu hao wakipata soko wanalipia kodi wapi?kwa siku moja zinauzwa Ng'ombe, mbuzi kondoo ngap ambazo hazilipiwi kodi?Bado serikali inamtambua mfugaji kama choka mbaya wakati huingiza fedha nyingi sana kuliko watu wengi wa kawaida. Kwann basi wasitengeneze utaratibu wa kukusanya walau 5% kwa kila Ng'ombe atakaeuzwa, Pesa zipo nyingi zinazunguka hazisomeki kwenye mfumo.

Ina maana uliambiwa wafugaji Kenya ndio wanalipa kodi? Jamii za wafugaji zinamiliki maelfu ya mifugo na hakuna huhangaika kuwafuatilia. Tungekua na namna ya kukusanya kila shilingi iliyo kwenye mizunguko huku kwetu yaani sijui tungekua wapi.
 

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,524
2,000
Na hiyo ya makadirio wanaoenda kwa sababu huwezi kukadiriwa bila kutoa chai.
TRA imejaa wapigaji wengi, nakumbuka kuna video ambayo Magufuli aliita kikao na wana biashara, wakamfungukia ukweli wote namna huwa wanababaishwa, mtu una biashara yenye mtaji wa Tshs 10,000,000 unapotaka ulipe kodi jamaa wanapiga mahesabu wanakuambia una deni la TRA la Tshs 200,000,000

Unaambiwa ufanye maamuzi, uwape kitita fulani wakurekebishie au ukapambane mbele huko, haya yote aliambiwa rais wenu sijui kama kuna lolote la maana mlilifanya au ile ilikua show tu, tatizo mnapenda maonyesho maonyesho ya kisiasa halafu utendaji zero.

Pia Watanzania hamna desturi ya kupenda kulipa kodi, nilishangaa sana nikiwa Bongo kuona hamna mtu huhangaika kuagiza risiti ya EFD. Sasa hapo mnataka mshindane na sisi kiuchumi, pengo baina yetu litazidi kuongezeka mpaka basi.
 

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,989
2,000
Tabutupu,

Taasisi za Tanzania zimeachana na weledi wa kitaaluma na kucheza midundo ya wanasiasa, TRA ikiwemo. Bila kutoa rushwa mlipa kodi Tanzania utatumia na kuiacha biashara. Hawana ubunifu wa kuwaza vyanzo vipya vya mapato. Kila mwaka ni kuwaongezea Kodi wafanya biashara walewale. Kwa logic ipi TRA wamediriki kuwaongezea wafanya biashara Kodi mwaka huu wenye janga la mvua ya muda mrefu na corona? Wakapimwe akili.
 

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
18,532
2,000
We mbwa umetoa wapi hiyo? 14T?

Unabwabwaja tu na fake data zako, KRA na TRA hazina tofauti kubwa ya kutisha kwenye ukusanyaji mapato, KRA haijatupita hata mara 1,achilia mbali mara 3!

View attachment 1572013
Hili ndio tatizo tulilonalo, badala ya mtu kuweka uzi kwa kutumia data za kweli na kutumia maneno ya kuwatia wachangiaji hamasa ili wachangie, wao wanaanza kujenga chuki.

Tafadhalini sana wenzetu toka Kenya, punguzeni tabia ya kupenda kujikweza haiwasaidii badala yake inawatengenezea maadui zaidi. Ingefaa kusema KRA inakusanya kodi nyingi kulikoeTRA, ingetosha, au kama ulitaka kuonyesha ni kiwango gani, basi ungekusanya taarifa za kweli ambazo ni up to date kuliko kuweka taarifa za zamani.
 

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,524
2,000
Huu mjadala ni wa kuelimishana na siyo kutafuta nani mkubwa kwa sababu huu ndio ukweli ambao hata Rais wako anaujua.

Tuisaidie TRA .. TRA ikikusanya vizuri ni mafanikio kwa Tanzania.

Tuweke utoto pembeni. JF ni kwa big minds siyo pororojo, porojo huko facebook.
Tumekubaliana tupunguze mivutano isiyokuwa kuwa na tija. Lengo ni kuonyesha ni maeneo gani nchi ipi inafanya vizuri ili nchi nyengine ijifinze kutoka nchi nyingine.

Katika huu uzi na ule unaohusu bandari ya Dar na Mombasa, watu wamejaribu kuchangia bila ushabiki wa kujisifu au kujaribu kushusha nchi nyingine.

Jambo la kushangaza, wewe umeanza kujisifu na kutoa kashfa kwa Tanzania, jaribu kuwa na busara kidogo. Ukweli ni kwamba, niliomba tupunguze malumbano baada ya kuona wakenya mumezidiwa katika mijadala mbalimbali, jana yote wakenya mlipotea kabisa.

Punguza chuki na wivu, kila nchi ina mapungufu yake na mazuri yake, lengo ni kujifunza na kubadilishana uzoefu, sasa wewe unataka kuendeleza malumbano ambayo tayari Kenya mlishaanza kuzidiwa, jaribu kubadilika mkuu.
 

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
18,532
2,000
Watanzania tuko nyuma kwa mambo mengi, kitu tunachokijua ni mdomo tu.

Maneno mengi na ujuaji mwingi
Tafadhali hili sio lengo la huu mjadala, lengo ni kuonyesha mapungufu ili watu wajifunze, wacha kutoa conclusions ambazo huna uhakika nazo, hadi sasa tumezungumzia maeneo mawili tu, ya bandari za Mombasa vs Dar.na TRA vs KRA, subiri kuna maeneo mengi yanakuja, sijui kama hutofuta hii kauli yako.
 

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,524
2,000
Leta data za kweli.. 14 TR ndio makusanyo ya TRA.

Achana na huyo mpuuzi kachukua bajeti ya serikali anadhani ndio makusanyo ya TRA.

Pia hajui kwamba kuna mapato yasiyo ya kodi ambayo hayapiti TRA.

JF ya miaka hii mbona imejaza vilaza na wanabfacebook?
Hili ndio tatizo tulilonalo, badala ya mtu kuweka uzi kwa kutumia data za kweli na kutumia maneno ya kuwatia wachangiaji hamasa ili wachangie, wao wanaanza kujenga chuki.

Tafadhalini sana wenzetu toka Kenya, punguzeni tabia ya kupenda kujikweza haiwasaidii badala yake inawatengenezea maadui zaidi. Ingefaa kusema KRA inakusanya kodi nyingi kulikoeTRA, ingetosha, au kama ulitaka kuonyesha ni kiwango gani, basi ungekusanya taarifa za kweli ambazo ni up to date kuliko kuweka taarifa za zamani.
 

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,524
2,000
Kabisa.. magufuli kajitahidi kuwapa elimu juu ya kuongeza base ya walipa kodi hadi akadiriki kutengeneza vitambulisho vya wamachinga lakini TRA bado wamelala..

Kwa kweli TRA inalakujifunza kutoka KRA.
Taasisi za Tanzania zimeachana na weledi wa kitaaluma na kucheza midundo ya wanasiasa, TRA ikiwemo. Bila kutoa rushwa mlipa kodi Tanzania utatumia na kuiacha biashara. Hawana ubunifu wa kuwaza vyanzo vipya vya mapato. Kila mwaka ni kuwaongezea Kodi wafanya biashara walewale. Kwa logic ipi TRA wamediriki kuwaongezea wafanya biashara Kodi mwaka huu wenye janga la mvua ya muda mrefu na corona? Wakapimwe akili.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom