Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Kocha wa makipa simba mbaroni kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.

Sambamba na boss wa Cambiaso

================


Kocha huyo, Mwalami Sultan ni kati ya watuhumiwa 9 akiwemo Mmiliki wa Kambiaso Sports Academy, Alhaj Kambi Zubeir Seif wanadaiwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin zenye Kilo 34.89.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), Gerald Kusaya Kusaya amesema watuhumiwa wote wamekamatwa katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi katika Operesheni iliyofanyika Oktoba, mwanzoni na Novemba 2022.

K1.PNG
K2.PNG


Pia soma:
 
Kamishna Jenerali wa DCEA Bw. Gerald Kusaya ametangaza watuhumiwa 9 wakiongozwa na Mmiliki wa Kambiaso Sports Academy, Alhaj Kambi Zubeir Seif pamoja na Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Mwalami Sultan kuhusika kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye Kilo 34.89.

Mwalami.jpg

Mwalami Sultan​
 
#HABARI Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imewakamata watuhumiwa 9 wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin kg 34.89 ambapo miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na Muharami Sultan ambaye ni kocha wa magolikipa wa timu ya @SimbaSCTanzania
pamoja na Kambi Zuber Seif maarufu kama Cambiasso.

#EastAfricaRadio
https://t.co/JtJMiS3ulE
 
Juzi nilipohudhuria Live band hapo DSM na kuona sijui Mapendeshee yanatajwa Tena kwenye nyimbo zile nilianza kuhisi hii biashara ya Madawa Haina muda mrefu inaanza.

Hongereni Mamlaka kuweza kuwakamata hao Wahusika ila muhimu wasije kuhonga pesa na kuachiliwa.
 
Kwaio star hapo ndio wa simba, bila kumtaja huyo habari haiuziki, na pia sababu ya chuki kubwa sana iliyojengwa miaka ya karibuni kati ya simba na yanga, basi kuna watu wataitumia hii habari kuichafua simba, bila kujua hata wa gsm nae ni wale wale tu sema wao ndio washika mpini ( mapapa) hawa wanaokamatwa ni dagaa tu.
 
Kamishna Jenerali wa DCEA Bw. Gerald Kusaya ametangaza watuhumiwa 9 wakiongozwa na Mmiliki wa Kambiaso Sports Academy, Alhaj Kambi Zubeir Seif pamoja na Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Mwalami Sultan kuhusika kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye Kilo 34.89.

View attachment 2417341
Mwalami Sultan​
Nimeumia sana kama Mwanasimba kindakindaki
 
Kamishna general wa mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Gerrad Kusaya ametangaza Watuhumiwa 9 wakiongozwa na mmiliki wa Kambiaso sports academy Alhaj Kambi Zubeir Seif pamoja na Kocha wa Makipa wa Simba Mwalami Sultan kuhusika kukamatwa na madawa
20221115_112613.jpg
20221115_112744.jpg
 
Back
Top Bottom