Dar: Watu watatu Wakamatwa wakiwa na kilo 15.19 za dawa za kulevya aina ya Heroin

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Washirika wa mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma wakamatwa na kilo 15 za dawa za kulevya aina ya heroin.

Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imewakamata watuhumiwa watatu ambao ni washirika wa mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zuberi Seif (40) wakiwa na kilo 15.19 za dawa za kulevya aina ya heroin.

Akizungumza jijini Dar es Salam leo Desemba 7, 2022 Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya amesema watuhumiwa waliokamatwa ni Suleiman Thabit mkazi wa Salasala.

Wengine ni Sharifa Suleiman Bakari mkazi wa Maji matitu na Farid Hamis Said mkazi wa Maji matitu jijini Dar es Salaam.

=====

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

UKAMATAJI WA KILO 16.643 ZA DAWA ZA KULEVYA

Dar es Salaam, 07 Disemba, 2022
Katika kipindi cha mwishoni mwa mwezi Novemba 2022, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ilifanikiwa kukamata jumla ya kilo 16.643 za dawa ya kulevya zikijumuisha kilo 15.19 za heroin, gramu 655.73 za cocaine na gramu 968.67 za Methamphetamine zilizowahusisha jumla ya watuhumiwa saba.

Ukamataji wa kilo 15.19 za dawa za kulevya aina ya heroin zilizowahusisha watuhumiwa watatu ni mwendelezo wa operesheni zilizopita.

Watuhumiwa hawa ni washirika wa Kambi Zuberi Seif na wenzake waliokamatwa wakiwa na kilo 34.89 za heroin katika operesheni ya mwanzoni mwa mwezi Novemba 2022.

Watuhumiwa hao watatu ni Suleiman Thabit Ngulangwa (36), mfanyabiashara na mkazi wa Salasala, Sharifa Seleman Bakar (41), mkazi wa Maji matitu - Mbagala na Farid Khamis Said (22) mkazi wa Maji matitu – Mbagala, wote ni wakazi wa Dar es Salaam.

Watuhumiwa wengine wanne (4) walikamatwa wakiwa na gramu 655.75 za cocaine na gramu 968.67 za Methamphetamine. Walikamatwa wakiwa kwenye harakati za kusafirisha dawa hizo za kulevya kwenda nje ya nchi.

Watuhumiwa hao wanne ni Hussein Rajab Mtitu (28) anayejulikana pia kama Chodri Mohamed mfanyabiashara na mkazi wa Kibonde maji, Mbagala, Jaalina Rajab Chuma (31) anayejulikana pia kama Jaalina Mohan mjasiriamali na mkazi wa Tandika, Shabani Abdallah Said (36) mkazi wa Kilimahewa, Tandika, hawa pia ni wakazi wa Dar es Salaam, pamoja na Irene Dickson
Mseluka (39) mfanyabiashara na mkazi wa Ndala Shinyanga.

Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kiupelelezi kukamilika.

Kutokana na kuimarika kwa udhibiti wa dawa za kulevya nchini, wahalifu wa dawa za kulevya wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali ili kufanikisha uhalifu wao. Hata hivyo, Mamlaka iko macho na inaendelea kukabiliana na mabadiliko ya mbinu hizo.

Aidha, tunashirikiana na makampuni ya usafirishaji wa vifurushi, vyombo vyote vya ulinzi na usalama na wadau wengine katika udhibiti na mapambano dhidi ya dawa za kulevya ili kukabiliana na mbinu mpya za usafirishaji na uuzaji wa dawa za kulevya.

Imetolewa na,

Florence Khambi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya
 
Hapo mtandao unasakwa kimyakimya kama kuna walio baki wakazimimine hizo dawa vyooni tu maana watatajwa na mahala wanako zihifadhi
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata kilo 16.643 za dawa za kulevya zikiwamo kilo 15.19 za heroin. Dawa hizo aina ya heroin zimekamatwa kwa watuhumiwa watatu ambao ni washirika wa Kambi Seif na wenzake waliokamatwa mwanzoni mwa Novemba wakiwa na kilo 34.89 za heroin.

Kiwango hicho kinafanya jumla ya dawa za kulevya zilizokamatwa kwa Kambi na washirika wake kufikia kilo 50.08.

Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Gerald Kusaya amewataja watuhimiwa hao ni Suleiman Ngulangwa (36), Sharifa Bakar (41) na Farid Said (22) wote wakazi wa Dar es Salaam.

Watuhumiwa wengine wanne walikamatwa na gramu 655.75 za cocaine na gramu 968.67 za metamphetamine, kulingana na Kusaya hawa walikamatwa wakiwa kwenye harakati za kusafirisha dawa hizo.

Waliokamatwa katika operesheni hiyo ni Irene Mseleku (39) mkazi wa Shinyanga, Hussein Mtitu (28), Jaalina Chuma (31) na Shaban Said (36) wote wakazi wa Dar es Salaam.

“Kutokana na kuimarika kwa udhibiti wa dawa za kulevya nchini, wahalifu wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali ili kufanikisha uhalifu wao. Hata hivyo mamlaka iko macho na tunaendelea kukabiliana na mbinu hizo.

“Tunashirikina na kampuni za usafirishaji wa vifurushi, vyombo vya ulinzi na usalama na wadau wengine katika kudhibiti ili kukabiliana na mbinu mpya za usafirishaji na uuzaji wa dawa za kulevya,” amesema Kusaya.

Katika hatua nyingine Kusaya amewaonya wasanii wanaotunga nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya na kueleza kuwa hatua zitachukuliwa dhidi yao endapo itathibitika wanafanya hivyo.

MWANANCHI
 
Sijadanganya.
Nilichosema ni kweli

Kwenye hiyo list wanafika jumla ya watu 11 na wote ni dini moja

Angalia madanguro yote wengi ni hao hao

Nenda Temeke wote ni hao hao, tena Temeke ndo kuna danguro la mashoga na wote ni Ijumaa

Nenda madanguroni asilimia 90 ni Ijumaa

Vibaka, Majambazi wengi wao

Matajiri wakubwa pia ni wao

Viongozi wakubwa Tanzania ni wao

Walalamikaji kuonewa ni wao
Umeanzisha vita!!
 
Back
Top Bottom