KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 86
KWA HIYO UNASEMA MWANAKIJIJI KAOLEWA ?? mi nauliza tu. unajua wazungu/weusi hata kama mwanamme anakwambia am married !
Halafu huu ujeuri wa kusema kama mnaona tumekosea NENDENI mahakamani.......haya nimatusi kwa wanachi wa tanzania wanaotaka kuelewa YANAYOJIRI
Mbona mna kiherehere? chuki nyingine za ajabu sana watu badala ya kujadili anachosema mnajadili lahaja na lafidhi ya waziri. Naona mnashindana nani mpondaji zaidi... JF usanii tu
Gamba la nyoka
usalama wa nchi unauchukuliaje ndg yangu......................TRUST ME, pamoja na kazi zingine za ulinzi, classified information zozote ambazo zaweza kuleta utata ndani ya jamii kama ilivyo sasa...........ni moja ya kazi zao kuhakikisha hizi classified inf hazi-leak.
Maan nenda ktk Intelligence Unit yeyote ulimwenguni kuprotect nyaraka za serikali ni moja ya kazi muhimu kwao
yaani mbaya sana unawaambia watu wasikilize radio saa 7 mchana saa za marekani halafu wee mwenyewe huonekani ! mie nilizidisha sauti ya computer hadi mwisho, sikusikia kitu, kuna mtu akanipigia simu nikawa simsikii vizuri akauliza wee maskio yako mazuri kweli, nikasema labda nimekuwa kiziwi maana radio ya mwanakijiji sisikii kitu ukizingatia sauti maxima halafu mtu mwingine ananiuliza kama maskio yangu mazuri, i was wild ! kumbe kosa lako wee bana wa shambani !
God Bless you Geeque & MKJJ kwa kutupa nafasi hii nyingine
Siku ya Jumamosi kwenye matangazo yetu ya moja kwa moja (live) nilipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Tanzania Mhe. Mohammed Seif Khatib (MB).
<p> Makubwa tuliyozungumza ni suala zima la tuhuma zilizotolewa na ushirika wa wapinzani tarehe 15 Septemba pale Jijini Dar. Pamoja na hayo tulizungumzia kuhusu suala la Buzwagi na jinsi mwitikio wa wananchi ulivyokuwa na hasa ziara ambazo zimefanywa wiki iliyopita na Mawaziri na Manaibu wao kwenye mikoa mbalimbali.</b>
<p>Je, hoja za wapinzani zina msingi? Je serikali ina msimamo gani kuhusu kuvuja kwa mkataba wa Buzwagi na kama ina mpango wa kuwachukulia hatua za kisheria wale watakaokutwa nao? </b>
Hayo na maswali mengine mengi yanajibiwa na Mhe. Khatib. Lakini majibu yake yanajibu maswali niliyomuuliza? Sikiliza uamue... Kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kusikiliza mahojiano yangu na Mhe. Khatib, unaweza kusikiliza kupitia KLH News...
Katika Mahojiano yake na Mwanakijiji Jumamosi Waziri wa Habari na Utamaduni,Seif khatib alidai kuwa si kweli kwamba Viongozi wanazomewa huko Mikoani,naomba mumuonyeshe article hii ya kuzomewa kwa Dr. Ngasongwa na kule Mbeya Bwana Tyson(Waziri Wasira) alipozomewa!!!,Kitendo cha kuzomea kinaonyesha kuchoshwa.
ZIARA ZA MAWAZIRI MIKOANI NI BALAA.
2007-10-08 09:27:14
Na Waandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw. Henry Daffa Shekifu, amelazimika kuingilia kati na kuwasihi wananchi wa wilaya ya Hanang wasimzomee Waziri wa Mipango Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa, anaripoti Zillipa Joseph wa PST kutoka Hanang.
Bw. Shekifu aliwataka wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko mjini Katesh kutoa nafasi kwa viongozi kujieleza badala ya kuzomea.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya Dk. Ngasongwa kujibu maswali ya baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
`Tufautishe mikutano. Mkutano huu sio wa kampeni ni wa serikali, tutoe nafasi kwa viongozi, tusitunishiane misuli tukapoteza amani, na amani ikivunjika kuirudisha ni kazi. Kama kuna mwananchi anataka kubadilisha mkutano huu uwe wa kampeni nitamdhibiti kwa nguvu za serikali,` alionya Bw. Shekifu.
Baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wananchi hao ni kutaka kufahamu ni kwa sababu? gani serikali inawasambaza mawaziri na manaibu wao mikoani kuelezea bajeti, na kudai kuwa huo ni ubadhirifu wa fedha za walipa kodi, wakati wananchi wanataabika na bei za bidhaa kupanda.
Swali lingine lilihoji uhalali wa kumsimamisha mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe, kuhudhuria vikao vya Bunge huku wananchi hao wakidai kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Akijibu maswali hayo, Dk. Ngasongwa alisema Bw. Zitto, anajitafutia umaarufu na kuongeza kuwa alitoa lugha ya matusi bungeni ndio sababu ya kusimamishwa kuhudhuria vikao.
Tehe tehe ! patamu hapo,maana hiyo mechi itaitwa CCM vs Wananchi. Kwa kujikomba,Tambwe na Akwilombe watataka kumuonyesha bosi wao walivyo jasiri kwa kusaidia kumshushia kipigo mwananchi huyo.Zomeazomea hii kuna siku Makamba ataamua kutoka jukwaani na kumkimbiza mwananchi halafu amdunde live....hoohoo?