KKKT na mtego kwenye msiba wa Mengi

KKKT na mtego kwenye msiba wa Mengi

Si unasikia kwenye matangazo ya ndoa kuna wale wanaoambiwa kama wana pingamizi la haki?
Baadhi ya mapingamizi ya haki ni
Kifo cha mwenza... Kuwe na death certificate
Ugonjwa wa akili kwa mwenza (ithibati ya cheti cha hospital)
Talaka (ithibati ya hati ya talaka)
Haya Unayosema Kiongozi Ni Tofauti Na Wanachosema Hao Wengine
Wao Wanasema Iwapo Umemchoka Kwa Namna Mbalimbali Unamuacha Unachukua Talaka Unafunga Nyingine.
 
Naona hawafuati misingi ya kanisa,au labda kunakuwa na sababu.
Hata Joyce Kiria baada ya kuachana na mumue wa kwanza na yupo hai walifungiwa ndoa na kileo huko kimara, sasa kaivunja tena sijui akipata mwingine atafungishwa tena, some times KKKT bora wangekuja na mitaala yao maana mhhh..
 
Hata Joyce Kiria baada ya kuachana na mumue wa kwanza na yupo hai walifungiwa ndoa na kileo huko kimara, sasa kaivunja tena sijui akipata mwingine atafungishwa tena, some times KKKT bora wangekuja na mitaala yao maana mhhh..
Haa🤣😃😁
Hao Viongozi Wa Dini Wana Yao Iwapo Ni Kweli
 
Mkuu KKKT haina TAABU taabu ni baadhi ya VIONGOZI, kukimbia kanisa hukufanya jema maana hata huko kwa WALOKOLE si ndio wako kina KAKOBE ( tunakula mema ya nchi ikulu) kina LUSEKELO ( wanao tukana majirani wakiwa wamelwa kabisa) na wengine wengi.. Simama na BIBLIA ijue kweli nayo itakuweka huru.
Kiongozi KIPOFU akimuongoza mwenzake WOTE wantumbukia shimoni;
 
Kweli kabisa mkuu., yaani kuna mambo ya ajabu ajabu sana kwa baadhi yao.
Waumini Wanaumizwa Sana Na Mambo Kama Hayo Hasa Wanapoona Watu Wanapewa Stahiri Kwa Nyadhifa Zao Siyo Kwa Kufuata Misingi Ya Dini
 
Hata Joyce Kiria baada ya kuachana na mumue wa kwanza na yupo hai walifungiwa ndoa na kileo huko kimara, sasa kaivunja tena sijui akipata mwingine atafungishwa tena, some times KKKT bora wangekuja na mitaala yao maana mhhh..
Ndoa ya pili ya Joyce ifungiwa kwa mkuu wa wilaya jamani hii nakumbuka
 
Waumini Wanaumizwa Sana Na Mambo Kama Hayo Hasa Wanapoona Watu Wanapewa Stahiri Kwa Nyadhifa Zao Siyo Kwa Kufuata Misingi Ya Dini
Inaumiza sana mkuu, haswa umepata msiba una hitaji msaada wa kanisa halafu wanakujia na vikwazo vyao kuhusu marehemu, huko rombo kuna marehemu waligoma kumzika kisa tu ALIKUWA MLEVI...halafu unaambiwa wanafanya hivyo na walevi wengine wajifunze waache ulevi, hovyo kweli kweli.
 
Ndoa ya pili ya Joyce ifungiwa kwa mkuu wa wilaya jamani hii nakumbuka
Ilifungwa na mkuu wa wilaya baada ya muda ikafungwa kanisani mkuu, fuatilia tena akasema kabisa WALIOKUWA WANANINANGA KANISA NITALISIKIA MKO WAPI? , ilfungwa na shela akavaa ila akasema HAFANYI SHEREHE TENA..alishafanya.
 
kuhusu kuoa wake wengi au la...nadhani yesu alinukuliwa ndivyo sivyo
 
Karibuni Mengi alionekana KKKT msasani na akaaidi kutoa vifaa vya matarumbeta kwa ajili ya huduma(Sina hakika kama ametoa) sasa usishangae ukaambiwa alirudishwa kundini msasani na maana kama ni kweli alirudishwa Sawa kama sio kweli basi mchungaji atazongwa mpaka azikwe na KKKT kama walivyofanya ya mtoto wa Mwakasege (ila Mungu anawaona ujue) Mtoto wa Mwakasege alizikwa kwa heshima zote za KKKT ingawa hakuwa ameandikishwa. Makapuku mlie tu mtaa mbulia kuzungushwa na kanisa mpaka mkome yetu macho
 
Sokoine alizikwaje?
Mengi ana mchango mkubwa kitaifa na kimataifa.
Na ni mshiriki mzuri wa kabisa.

Mussa alioa wake wengi
Ibrahimu alioa wake wengi.
Isaka alioa wake wengi.
Yakobo alioa wake wengi.
Daud alioa wake wengi.
Suleimani alioa wake wengi.
Mtume Mohammed alioa wake wengi.
Nani miongoni mwetu mkubwa na mwenye imeni kubwa kuliko hao manabii walioongea mpaka na Mungu?

Kuhudhuria ibada kwa Viongozi wa kabisa ni muhimu mana Mengi amekua ni mshirika mzuri sana kwa kabisa na makanisa . Hiya ya familia yake hayatuhusu.
HERI WENYE MOYO SAFII WATAKWENDA... dini ya kweli ni Kutoa sadaka..Kusaidia wajanee na yatima na wote wenye Uhitaji.. Mengi ametoa zaidi ya Sadaka na Kanisani Hakuacha kwendaa... Leo kanisa linaanzia wapi kumkataa???[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15] Suala la kufunga ndoa mara mbili ni zambi kama dhambi zinginee tu ni kutubu tu maana ulitaka mzee wa watu aendelee kuishi maisha ya Upwekee na uzinzi wa kimya kimyaa.. Na biblia inaruhusu mwanaume kumuacha mkewe kwa Dhambi ua uzinzi sasa wewe unajua sababu ya Mengi na mkewe kuachana?? acheni kuwa Miungu watu
Samehe mara 7x70; wapi uzinzi hausameheki hata mara zote hizo, Acha kupotosha watu, kaa chini ufundishwe.
Mke mmoja hata kifo kiwatenganishe; hilo ndio NENO na halijipingi wewe ndio hujui.
 
kama walivyofanya ya mtoto wa Mwakasege (ila Mungu anawaona ujue) Mtoto wa Mwakasege alizikwa kwa heshima zote za KKKT ingawa hakuwa ameandikishwa.

hakuwa ameandikishwa maana yake nini? Hakuwa mlutheri?
 
Kama inavyofahamika katika kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania ,ndoa inayotambulika ni moja tu hadi kifo kitakapowatenganisha.

Mzee Mengi ambaye alikuwa ni muumini wa kanisa la kilutheri Tanzania na katika uhai wake inasemekana alifunga ndoa nyingine na Jack wakati huo huo Mama Mercy Mengi alikuwa bado yupo hai.

Je Mengi atazikwa na kanisa la kilutheri ,kikristo? Je kanisa litamtambua Jack kama mke wa marehemu? Kiukweli huu ni mtego na nightmare kwa kanisa la kilutheri.


Mungu hamfichi mnafiki, viongozi wa KKKT ni wanafiki waliopitiliza, wanajiita kanisa la matengenezo wakidai kule kwingine kulikuwa na vikaratasi vya utakaso, kwakweli wao ndiyo wamekuwa wa vikaratasi vya utakaso mara 10 ya hao waliowakimbia, kuna sababu gani ya kuandika sadaka ya mtu kwenye kadi maalumu wakati Mungu aliagiza sadaka kuwa ya siri?

Sidhani kama watakwepa mazishi kwasababu hata vigogo wao wana small houses kibao!!!
 
Back
Top Bottom