Usihalalishe UOVU kwa waliotenda uovu; MKE MMOJA MUME MMOJA hadi kifo kiwatenganishe; MUNGU ANACHUKIA KUACHANA, hilo ndilo neno la Bwana.
Mungu hana Upendeleo, Biblia unaweza kutafsiri unavyotaka wewe lakini DHAMIRA yako inakuambia sivyo.
Ingekuwa RUKSA wake wengi Adam angepewa na MUNGU wake kadhaa. Mengine yaliandikwa ili tujifunze tusifanye kama wao.
Hao WOTE uliowataja ni wanadamu, hatuna cha kujifunza kwao na wao walitenda dhambi kama wanadamu wengine.
Huko KKKT huwezi kufundishwa hayo, huko pombe, nyumba ndogo uzinzi hawadhubutu kukemea.
NENO la Mungu walishatia MAJI siku nyingi.
Karibu katika familia ya WALOKOLE.