KIWIRA na MCHUCHUMA: A Campaign To Reclaim...

KIWIRA na MCHUCHUMA: A Campaign To Reclaim...

Kiwira mine workers protest, point fingers at Mkapa

THISDAY CORRESPONDENT
Mbeya

SCORES of workers of Kiwira Coal and Power Company Limited rallied outside the plant over the weekend to protest over delayed salary payments, blasting former President Benjamin Mkapa for his dubious involvement in the privatization of the formerly state-run mine.

Employees of the coal mine located in Mbeya Region staged a protest demonstration, seeking President Jakaya Kikwete’s intervention in the matter.

They criticized the Mkapa administration in the controversial privatization of the mine in 2005, and blamed the ex-president for the current predicament facing the workers.

They carried placards with messages blasting the mine’s shareholders and urging the government of the day to take definitive steps to end the turmoil.

The workers said they have gone without salaries for at least five months, and accused the management of the troubled mine of ignoring their grievances.


Among other things, the workers questioned Mkapa’s involvement in the privatization of the coal mine, which was sold under dubious circumstances to a company formed by the ex-president and the then Minister for Energy and Minerals, Daniel Yona.

’’JK you are our only hope. What is Kiwira’s fate? Why have you forsaken us?’’ stated some of the placards carried by the workers.

The workers demanded a final decision on the fate of the factory, saying they were angered at the way it is being run.


They furthermore criticized shareholders for failing to make any significant capital injection and vehemently questioned the $271m (approx. 350bn/-) deal between the company and the state-owned Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO).

While the 20-year contract calls for Kiwira coal mine to supply up to 200MW to the national power grid, the said loss-making company can now manage to supply just 1-2MW of electricity to TANESCO.


The opposition camp in parliament has been demanding action from the government on the privatization of the Kiwira coal mine, asserting that the national constitution does not grant any ex-president absolute immunity from criminal prosecution.

Debating this year’s (2008/09) budget estimates of the Prime Minister’s Office, opposition legislators openly questioned the sale of the coal mine to TANPOWER Resources Limited, a private company jointly set up by Mkapa, Yona and immediate family members in 2004 while both were still in public office.

Several months ago, the government promised to make a formal statement to the National Assembly on the controversial privatization of the Kiwira coal mine.

However, the statement by incumbent Energy and Minerals Minister William Ngeleja has not been made to date.

About 85 per cent of shares in Kiwira Coal and Power Ltd are currently owned by TANPOWER Resources Ltd. The government currently retains just 15 per cent of shares in Kiwira.


Investigations by THISDAY have already uncovered that TANPOWER Resources swiftly assumed ownership of the previously state-owned Kiwira coal mine after being registered by then president Mkapa and senior minister Yona, with very few other people in government actually aware of what was actually going on.

According to THISDAY findings, Tanpower Resources was officially registered on December 29, 2004, and within just six months had succeeded in acquiring most of the majority shares in the renamed Kiwira Coal and Power Ltd.

Tanpower Resources was the joint brainchild of Mkapa and Yona, formed during the later stages of the third phase government when one was still serving as president of the United Republic and the other as minister for energy and minerals, respectively.

At the time of the company’s establishment in 2004, its first listed directors were the then first lady Mrs Anna Mkapa; the then minister for energy and minerals Daniel Yona; Nicholas Mkapa (the president and Mrs Mkapa’s son); Joseph Mbuna (Nicholas Mkapa’s father-in-law); and Evans Mapundi.
 
Mpaka Wafanyakzi wagome na kuanza kusema hovyo ndiyo Ngeleja anaona umuhimu wa kutwambia Watanzania kuhusu ripoti ya Kiwira ambayo ilitolewa April 2008. Kazi kweli kweli!!

Ngeleja: Tuko tayari kutoa taarifa ya Kiwira bungeni

2008-12-18
Na Joseph Mwendapole

Wizara ya Nishati na Madini, imeahidi kupasua jipu hivi karibuni kuhusu nani mmiliki wa mgodi wa wa makaa ya mawe wa Kiwira, ambao unahusishwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Akizungumza na Nipashe jana, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema kwa kuwa suala hilo liliibuliwa bungeni, basi jibu hilo watalitoa huko huko bungeni.

Alipoulizwa Wizara yake inatarajia kutoa jibu hilo katika mkutano upi wa Bunge, Ngeleja alisema hilo linategemea zaidi ratiba itakayopangwa na Bunge.

Alisema tayari wizara yake ina taarifa ya kutoa kuhusu mgodi huo na kwamba wanachosubiri ni kusoma taarifa hiyo watakapopewa muda.

Mgodi huo umekuwa ukihusishwa na aliyekuwa Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.
Kwa pamoja wanadaiwa kujiuzia mgodi huo kwa Sh. milioni 700 wakati thamani halisi ya mgodi huo ni Sh. bilioni nne.

Inadaiwa kuwa licha ya kujimilikisha mgodi huo kwa bei hiyo ya kutupa na kumiliki asilimia 80 kwa kutumia Kampuni yao ya TanPower Resources Limited, kiasi walicholipa ni Sh. milioni 70 tu kati ya Sh. milioni 700.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), nayo ilikaririwa siku chache zilizopita ikisema kuwa itatoa taarifa ya uchunguzi wa mgodi wa Kiwira hivi karibuni, ambapo DPP, Elieza Feleshi, alisema ofisi yake bado inalifanyia uchunguzi suala hilo.

Alipoulizwa kwanini uchunguzi huo unachukua muda mrefu, Feleshi alisema wanafanya uchunguzi huo kwa umakini ili kutenda haki kwa pande zinazohusika.

``Bado tunalifanyia kazi ila halitakaa sana kila kitu kitawekwa hadharani hivi karibuni msiwe na haraka tuacheni tufanye kazi kwanza,`` alisema Feleshi.

Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), alikuwa wa kwanza kuibua tuhuma katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwaka huu, alipowataja bungeni Mkapa na Yona kuwa wanamiliki mgodi huo na walijiuzia kwa bei ya kutupa na kupendekeza kuwa wanastahili kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua.

Kimaro alisema mwaka 2004, Mkapa kwa kushirikiana na Yona, walianzisha Kampuni ya TanPower Resources Ltd na mwaka mmoja baadaye wakauziwa machimbo ya Kiwira kimya kimya.

Alisema katika mauziano hayo ya siri, TanPower Resources Limited, ilikuwa iilipe serikali Sh. milioni 700 katika mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh. bilioni 4.

Hata hivyo, Kimaro alisema cha kushangaza ni kwamba, kampuni hiyo ilifanya malipo ya awali ya Sh. milioni 70 tu.


Kimaro alisema mwaka 2006, Mkapa na Yona, waliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa ajili ya kufua umeme kwa makubaliano ya kulipwa `capacity charge` (gharama za uwekezaji bila kujali kwamba wamefua umeme au la) ya Sh. milioni 146 kila siku (dola 3.6 milioni kwa mwezi) pasipo kufuata utaratibu.

SOURCE: Nipashe
 
Kwa nini Serikali isiwanusuru wafanyakazi wasio na hatia kama ilivyofanya kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Reli?
 
Ngeleja: Tuko tayari kutoa taarifa ya Kiwira bungeni

2008-12-18 12:35:30
Na Joseph Mwendapole


Wizara ya Nishati na Madini, imeahidi kupasua jipu hivi karibuni kuhusu nani mmiliki wa mgodi wa wa makaa ya mawe wa Kiwira, ambao unahusishwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Akizungumza na Nipashe jana, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema kwa kuwa suala hilo liliibuliwa bungeni, basi jibu hilo watalitoa huko huko bungeni.

Alipoulizwa Wizara yake inatarajia kutoa jibu hilo katika mkutano upi wa Bunge, Ngeleja alisema hilo linategemea zaidi ratiba itakayopangwa na Bunge.

Alisema tayari wizara yake ina taarifa ya kutoa kuhusu mgodi huo na kwamba wanachosubiri ni kusoma taarifa hiyo watakapopewa muda.

Mgodi huo umekuwa ukihusishwa na aliyekuwa Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.
Kwa pamoja wanadaiwa kujiuzia mgodi huo kwa Sh. milioni 700 wakati thamani halisi ya mgodi huo ni Sh. bilioni nne.

Inadaiwa kuwa licha ya kujimilikisha mgodi huo kwa bei hiyo ya kutupa na kumiliki asilimia 80 kwa kutumia Kampuni yao ya TanPower Resources Limited, kiasi walicholipa ni Sh. milioni 70 tu kati ya Sh. milioni 700.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), nayo ilikaririwa siku chache zilizopita ikisema kuwa itatoa taarifa ya uchunguzi wa mgodi wa Kiwira hivi karibuni, ambapo DPP, Elieza Feleshi, alisema ofisi yake bado inalifanyia uchunguzi suala hilo.

Alipoulizwa kwanini uchunguzi huo unachukua muda mrefu, Feleshi alisema wanafanya uchunguzi huo kwa umakini ili kutenda haki kwa pande zinazohusika.

``Bado tunalifanyia kazi ila halitakaa sana kila kitu kitawekwa hadharani hivi karibuni msiwe na haraka tuacheni tufanye kazi kwanza,`` alisema Feleshi.

Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), alikuwa wa kwanza kuibua tuhuma katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwaka huu, alipowataja bungeni Mkapa na Yona kuwa wanamiliki mgodi huo na walijiuzia kwa bei ya kutupa na kupendekeza kuwa wanastahili kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua.

Kimaro alisema mwaka 2004, Mkapa kwa kushirikiana na Yona, walianzisha Kampuni ya TanPower Resources Ltd na mwaka mmoja baadaye wakauziwa machimbo ya Kiwira kimya kimya.

Alisema katika mauziano hayo ya siri, TanPower Resources Limited, ilikuwa iilipe serikali Sh. milioni 700 katika mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh. bilioni 4.

Hata hivyo, Kimaro alisema cha kushangaza ni kwamba, kampuni hiyo ilifanya malipo ya awali ya Sh. milioni 70 tu.

Kimaro alisema mwaka 2006, Mkapa na Yona, waliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa ajili ya kufua umeme kwa makubaliano ya kulipwa `capacity charge` (gharama za uwekezaji bila kujali kwamba wamefua umeme au la) ya Sh. milioni 146 kila siku (dola 3.6 milioni kwa mwezi) pasipo kufuata utaratibu.

SOURCE: Nipashe
 
Ni vizuri hii taarifa ikatolewa bungeni ili tusikie mengi, maana hawa viongozi wetu ni vichwa maji. wanadhani Wa TZ ni Mabwege miaka yote
 
Sitta: Ngeleja lete hoja ya Kiwira

2008-12-19
Na Joseph Mwendapole



Spika wa Bunge la Muungano, Samwel Sitta, amesema suala la mgodi Kiwira linaweza kujadiliwa katika mkutano ujao wa Bunge endapo Wizara ya Nishati na Madini itasema iko tayari kutoa taarifa hiyo.

Akizungumza na Nipashe jana, Sitta alisema endapo wizara hiyo italiarifu Bunge kuwa imekamilisha taarifa yake ni wazi Kamati ya Uongozi ya Bunge itaipa nafasi ya kuwasilisha bungeni ripoti yake.

``Kwa utaratibu Bunge linapoipa kazi serikali, yenyewe inatakiwa kusema tuko tayari na hapo ndipo wanapopangiwa muda wa kuwasilisha wanachotaka kusema,`` alisema Sitta.

Alisema kuna masuala mengi yanayosubiri kujadiliwa kwenye vikao vya Bunge hivyo lazima wizara husika iseme kama imekamilisha kazi iliyotumwa na Bunge.

``Unajua kuna mambo mengi ya kujadiliwa bungeni kama mkataba wa TICTS, TRL, Nyumba za Serikali na utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu mkataba tata wa kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond, hivyo kila kitu kikiwa tayari lazima kipangiwe siku,`` alisema Sitta.

Juzi Wiraza ya Nishati na Madini, iliahidi kupasua jipu hivi karibuni kuhusu nani mmiliki wa mgodi wa Kiwira, ambao unahusishwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini, Daniel Yona.

Akizungumza na Nipashe, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema kwa kuwa suala hilo liliibuliwa bungeni basi jibu hilo watalitoa huko huko bungeni.

Alipoulizwa wizara yake inatarajia kutoa jibu hilo katika mkutano upi wa Bunge, Ngeleja alisema hilo linategemea zaidi ratiba itakayopangwa na Bunge.

Alisema tayari wizara ina taarifa ya kutoa kuhusu mgodi huo na anachosubiri ni muda wa kusoma taarifa hiyo watakaopewa.

Mgodi huo ambao umekuwa ukihusishwa na Mkapa na Yona, kwa pamoja wanadaiwa kujimilikisha kwa Sh. milioni 700 wakati thamani yake halisi ni Sh. b
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), nayo ilikaririwa hivi karibuni ikisema kuwa itatoa taarifa ya uchunguzi wa mgodi wa Kiwira hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Mashitaka, Elieza Feleshi, alisema ofisi yake bado inalifanyia uchunguzi suala hilo.

Alipoulizwa kwanini uchunguzi huo unachukua muda mrefu, Feleshi alisema wanafanya uchunguzi huo kwa umakini ili kutenda haki kwa pande zinazohusika.

``Bado tunalifanyia kazi ila halitakaa sana kila kitu kitawekwa hadharani hivi karibuni msiwe na haraka tuacheni tufanye kazi kwanza,`` alisema Feleshi.

Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), alikuwa wa kwanza kuibua tuhuma katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwaka huu, alipowataja bungeni Mkapa na Yona kuwa wanamiliki mgodi huo na walijiuzia kwa bei ya kutupa, hivyo wanastahili kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua.

Kimaro alisema mwaka 2004, Mkapa kwa kushirikiana na Yona, walianzisha Kampuni ya TanPower Resources Ltd na mwaka mmoja baadaye wakamilikishwa machimbo ya Kiwira kimya kimya.

Hata hivyo, Kimaro alisema cha kushangaza ni kwamba, kampuni hiyo ilifanya malipo ya awali ya Sh. milioni 70 tu.

``Wakauziwa kwa Sh. milioni 700 bila kutangazwa na wao wakalipa down payment (malipo ya awali) ya Sh. milioni 70,`` alisema Kimaro.

Kimaro alisema mwaka 2006, Mkapa na Yona, waliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa ajili ya kufua umeme kwa makubaliano ya kulipwa `capacity charge` (gharama za uwekezaji bila kujali kwamba wamefua umeme au la) ya Sh. milioni 146 kila siku (dola 3.6 milioni kwa mwezi) pasipo kufuata utaratibu.


SOURCE: Nipashe
 
Isijekuwa mgodi umeshauzwa kwa wamiliki wengine halafu ndo mtuambie kuwa mgodi ni wa wamiliki hao wapya. Sisi tunawajua Mkapa na Yona na walijiuzia mgodi kwa milioni 70 yaani walituibia.
 
Kwani taarifa ya mkaguzi mkuu wa serikali inasemaje kuhusu taratibu za manunuzi ya huo mgodi? Mbona sikusikia cho chote kuhusu hili? Nani alifanya tathmini ya milioni 700? Nani alifanya tathmini ya bilioni 4?

Mimi napenda sana wazalendo wauziwe rasimali hizi lakini utaratibu utumike. Kama utaratibu haukutumika basi sheria ichukue mkondo wake. Kama utaratibu ulitumika basi tukae kimya itakuwa ni wivu sasa. Maana wazalendo wataogopa kununua rasilimali.
 
Patamu hapo....Leteni mambo wajameni twaweza kuweka kahistoria Tz na sisi kiranja mkubwa nae akatupwa korokoloni kama masikhara ati...Let's wait...
 

Akizungumza na Nipashe jana, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema kwa kuwa suala hilo liliibuliwa bungeni, basi jibu hilo watalitoa huko huko bungeni.

Mgodi huo umekuwa ukihusishwa na aliyekuwa Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.

Sasa wasipowataja watuhumiwa wetu tunaowajua, tumejiandaa vipi kukabiliana na hili? Maana Tanzania bwana, lolote laweza kutokea kama vile nchi isiyo na serikali. Hapa ndipo karata za upinzani zinatakiwa zichangwe vizuri
 
Hili la Kiwira ni either mkulu wa zamani anafikishwa pamoja na yona kutumia madaraka vibaya na kujiuzia kwa bei ya kutupwa Kiwira Coal Mine au hakuna kesi.Lakini hakuna namna anaweza kupelekwa mtu mwingine badala ya hao kama kesi hii itafunguliwa mahakamani.Nafikiri wakati mwingine tuna-underestimate uwezo wa kufikiri wa serikali yetu.

Kwamba asimame X & Y kwenye kesi inayomhusu Yona na mkulu wa awamu ya tatu? hilo haliwezekani.
 
Wakati wanapiga danadana za kisiasa, wananchi wa hayo maeneo wanahangaika kwa kukosa ajira. Wale wenye ajira hawajalipwa.

Nchi ina matatizo ya umeme lakini mgodi wa Kiwira unachechemea shauri ya kuuziana bila mpango na kuwapa watu wasio na uwezo.

Tuna safari ndefu sana.
 
TUCTA yahimiza serikali kuwalipa wafanyakazi Mgodi wa Kiwira

Na Joachim Nyambo, Mbeya
Mwananchi
12/20/2008

RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Ayoub Omary Juma ameitaka serikali kuingilia mgogoro wa malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, ili waweze kulipwa ili kuepusha hujuma zinazoweza kufanywa mgodini hapo.

Juma alisema hayo jana wakati wa kufunga mafunzo ya sheria mpya za kazi kwa wafanyakazi wa taasisi na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi yaliyofanyika katika Chuo cha Wafanyakazi Mbeya.

Alisema serikali inapaswa kuhakikisha wafanyakazi Kiwira wanalipwa malimbikizo yao kama ilivyofanya kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC),

Juma alisema kwa vile serikali imeshindwa kumtaja moja kwa moja mmiliki wa mgodi wa Kiwira na bado inaendelea kutafakari ni vyema ikaheshimu uvumilivu wa wafanyakazi hao kwa kuwalipa malimbikizo yao ya mishahara na stahili nyingine.

Aliongeza kuwa serikali inatakiwa kulichukulia kwa umuhimu wa pekee suala la wafanyakazi wa Kiwira ili kuwaondolea kero ya kuishi maisha duni na ya kubabaisha.

“Sisi hatuamini kama kweli serikali yetu inashindwa kuwalipa wafanyakazi hao tena kwa kiwango kizuri,tatizo hapa ni fedha nyingi kuwa mikononi mwa watu wachache,”alisema Juma.

Alisema shirikisho hilo lina imani kubwa na juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika vita dhidi ya ufisadi anayoendelea nayo hali ambayo imeendelea kurudisha imani kwa wananchi.

Wiki moja iliyopita jumla ya wafanyakazi 500 wa mgodi wa Kiwira waliandamana mkoani hapa kushinikiza kulipwa malimbikizo yao ya miezi mitano ya mishahara wanayodai, pamoja na kutaka kujulishwa mmiliki halali wa mgodi huo.

Hivi karibuni serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini iliahidi kutoa jibu la nani mmiliki wa mgodi wa Kiwira, ambao umekuwa ukihusishwa na rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa na aliyekuwa waziri wake wa Nishati na Madini, Daniel Yona.
 
Hali ya hatari mgodi wa Kiwira

MENEJIMENTI ya mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya imethibitisha kuwepo hatari ya kuripuka makaa ya mawe katika mgodi huo na kuiomba serikali kuingilia kati kunusuru hali iliyopo.

Wakati menejimenti hiyo ikitoa kauli hiyo kupitia kwa meneja wa mgodi huo Bw. Adam Abdul, wajume wa kamati ya bunge ya madini na nishati wapo mkoani humo pamoja na mambo mengine wanatarajia kuzuru mgodi huo ili kujionea hali halisi iliyopo.

Kwa mujibu wa meneja huyo Bw. Abdul hali za wafanyakazi ni mbaya kimaisha wengi wao wanadai mwekezaji mishahara ya miezi saba ambapo ametoa wito kwa serikali ichukue hatua kuwalipa wafanyakazi hao kama iliyofanyika kwa wafanyakazi wa kampuni ya reli ya kati TRL.

Akizungumzia hoja ya ni nani mwekezaji kwenye mgodi huo Bw. Abdul amekanusha madai ya kuhusishwa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin Mkapa kwamba menejimenti inawatambua watu watatu kwa kuwa ndio mara kwa mara wamekuwa wakihangaikia uwekezaji katika mgodi huo.

Amewataja watu hao kuwa ni mabwana John Mbuna, Evance Mapundi na Wilfred Malekia ambao kwa pamoja wanamiliki asilimia 85 ya hisa zote huku serikali ikimiliki asilimia 15 ya hisa na kwamba madai ya kuhusishwa kwa Mh. Mkapa ni uzushi kwa kuwa hayawezi kuthibitishwa.

Hata hivyo ameshindwa kufafanua ni kwa nini wamiliki wa hisa hizo wamekaa kando na kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi ambao wapo mbioni kugoma hadi walipwe haki zao, amesema suala hilo ni la kisera linatakiwa kujibiwa na wahusika kwa kuwa nayeye ni mwajiriwa.Miongini mwao hakuna aliyepatika kuzungumzia sakata hilo.

Aidha kuhusu hali ya mitambo na uendelezaji wa mgodi huo Bw. Abdul amesema mitambo mingi imechakaa na kwamba hakuna uwezo wowote wa kuzalisha umeme uliotarajiwa na serikali wa mega wati 200 na kwamba vyuma vingi vimeuzwa kama chakavu hali ambayo inaongeza shaka ya kuwepo uwekezaji endelevu.

Haikuweza kufahamika mara moja lengo mahususi la ziara ya wajumbe wa kamati ya bunge ya madini na nishati lakini taarifa zimeeleza kuwa walitarajia kukutana na wakuu wa wilaya za Rungwe, Kyela na Ileje mahali ulipo ngodi kabla ya kwenda katika eneo la mgodi Kiwira kukutana na menejimenti ya mgodi huo.

Mwishoni mwa mwaka jana wafanyakazi mdogi hapo waliandamana jijini Mbeya kushinikiza mwekezaji awalipe mishahara yao na kuiomba serikali iingilie kati kutatua tatizo lililopo
 
Wenye mgodi wao fisadi Mkapa na Yona wako wapi watatue matatizo ya Kiwira!? 😕
 
Jamani wameuziwa bei rahisi kuliko bado wanawatesa wafanyakazi.....au nao wanataka kuuza kama Dowans?
 
Ufisadi wa kutisha wagundulika Kiwira
​

• Shellukindo: Tutaonana na Ngeleja Dodoma
​


na Christopher Nyenyembe, Kyela
Tanzania Daima
​

WIMBI la ufisadi linaendelea kuiandama Serikali ya Awamu ya Nne, baada ya kugundulika matumizi mabaya ya sh bilioni 13 kwenye mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, uliopo mkoani Mbeya.

Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe (CCM), ndiye aliyeibua tuhuma hizo nzito alipotaka kujua fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kukarabati mgodi huo zilivyotumika kutokana na matatizo katika mgodi huo kuzidi kushamiri siku hadi siku.

Mapendazoe ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo ipo mkoani hapa chini ya Mwenyekiti wake,William Shelukindo, alihoji hayo kwenye kikao kilichowakutanisha wakuu wa wilaya za Ileje, Kyela na wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama kama wamewahi kusikia au wana taarifa kwamba serikali ilitoa sh bilioni 13 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya mgodi huo.

"Ndugu Mwenyekiti, ninachofahamu kupitia ripoti ya Jaji Mark Bomani, sh bilioni 13 zilitolewa kwa ajili ya ukarabati wa mgodi wa Kiwira, tunaambiwa mpaka sasa hivi hakuna chochote kilichofanyika, je, fedha hizo zilifikishwa au zimeishia wapi?" alihoji Mpendazoe.


Huku wajumbe wengi kwenye kikao hicho wakishangazwa na uwepo wa fedha hizo, inadaiwa kuwa serikali ina hisa asilimia 20 na mwekezaji Kampuni ya Kiwira Cool and Power (KCP) ina asilimia 80, hawajui kiasi hicho kikubwa cha fedha kilivyotumika.

Kauli ya mbunge huyo kuhoji mahali zilipoishia fedha hizo huku hakuna hata mbunge mmoja kwenye kamati hiyo aliyewahi kuuona mkataba wa ubinafsishaji uliowekwa kati ya serikali na mwekezaji, hoja hiyo nzito ilionekana kumshtua Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Shellukindo, ambaye alitaka uchunguzi ufanyike kwanza mara moja.

Kwa kuonyesha kuwa alichokisema ni sahihi, Mpendazoe aliinuka na kufuata kitabu chenye taarifa ya Jaji Bomani kuwa alitoa ushauri akiitaka serikali ichunguze kwa kina mahali zilipopelekwa fedha hizo mwaka 2006 kwa ajili ya ukarabati wa mgodi huo.

"Naomba muangalie ukurasa wa 119 wa taarifa ya Jaji Bomani, alishauri serikali ichunguze uhalali wa matumizi ya sh bilioni 13 za ukarabati, haiwezekani kiasi kikubwa cha fedha kama hizo zifikishwe katika mgodi huo leo hii, wawekezaji wanashindwa kununua hata baruti, hatuwezi kuridhika na hali hii," alisema Mpendazoe.

Baada ya hoja hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Shelukindo, aliwageukia wakuu wa wilaya za Kyela, Hussein Mashimba na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Esther Wakali, kama serikali kuu imewahi kuwaeleza kuwa imewekeza kiasi hicho cha fedha kwenye mgodi huo na wamewahi kuuona mkataba wa serikali na mwekezaji.

Swali hilo lilionekana kuwa gumu baada ya wakuu hao huku kila mmoja akijibu anavyoelewa kwamba hawajawahi kusikia wala kuambiwa kama kuna mabilioni ya fedha yamewahi kumwagwa Kiwira na hawajawahi kuona mkataba uliosainiwa kati ya serikali na mwekezaji.

"Ndugu mwenyekiti mimi kama mkuu wa wilaya kazi yangu kwa kushirikiana na Kamati yote ya Ulinzi na Usalama tumekuwa tukifanya kazi ya kuzuia migomo ya wafanyakazi ili kuepusha hujuma na hilo tumefanikiwa, lakini hatujui chochote wala Wizara ya Nishati na Madini haina mawasiliano na sisi kuhusu Kiwira," alisema Mashimba.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Wakali alisema kuwa hajui chochote kuhusu mkataba au fedha zilizowahi kutolewa, kwani halmashauri ya wilaya hiyo ndiyo inayolipwa ushuru lakini nayo inadai fedha za ushuru bila mafanikio, huku shughuli za uzalishaji zikiwa zimeshuka kwa kiasi kikubwa.

Baada ya majibu hayo, Shelukindo alimgeukia ofisa wa Madini kutoka makao makuu, Dar es Salaam, aliyetumwa kuongozana na kamati hiyo, alipoulizwa kama aliwahi kuuona mkataba wa serikali na mwekezaji, alijibu hajui kitu chochote.

Swali hilo lilionekana kuwa mwiba mkali kwa ofisa huyo, Jerad Remmy, ambaye alikiri wazi kutokufahamu chochote kuhusu mkataba wa Kiwira na serikali na kwamba hajawahi kuuona na hafahamu mambo mengi yanayoihusu serikali kupitia wizara hiyo na KCP.


" Mwenyekiti sifahamu chochote wala sijawahi kuuona mkataba wa serikali na mwekezaji, hilo swali linaweza kujibiwa na waziri mwenye dhamana, kwa kuwa ndiye anayeweza kuwa na jibu sahihi kwa upande wa serikali, kweli sijui chochote wakati mkataba unasainiwa sikuuona," alisema Remmy.

"Wapo watu wanaosema kuwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imefadhiliwa na wawekezaji ili isifanye kazi vizuri na waandishi wa habari wamekuwa wakitupigia simu, nawaambia huyo atakaye kuja kutuhonga ndio mwisho wake, wote tunajitosheleza, kazi tuliyonayo sasa ni kusaka mafisadi tu, huyu Waziri wa Nishati na Madini tutaonana naye bungeni," aliongeza.


Mbali ya madai hayo, kamati hiyo ya Bunge ilihoji mambo mbalimbali yanayokwamisha shughuli za uzalishaji katika mgodi huo, na sababu zilizochangia mwekezaji ashindwe kujenga mtambo wa kuzalisha umeme wa megawati 200 kama walivyowekeana mkataba na TANESCO.

Kusimimama kwa shughuli za uzalishaji kumewafanya zaidi ya wafanyakazi 500 katika kiwanda hicho wakose mishahara tangu Agosti mwaka jana na maofisa wa juu inadaiwa kuwa wengi hawajalipwa mishahara yao tangu mwezi Mei mwaka jana na haieleweki wanaishije.

Kamati hiyo ya Bunge ikiwa na Makamu Mwenyekiti wake, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela, aliwaomba wafanyakazi hao kuwa na subira wakati kazi inayofanywa na wabunge hao itakapowasilishwa bungeni na kuishauri serikali kuhusu hali halisi waliyoiona.
 
Yaani haya mambo ni kama mtu anaangalia picha ya Rambo. How this can happen wakati ukienda hospitali hakuna dawa, machine ndogo tu za kupima kisukari nu tabu, ukienda Mwananyamaala, Amana na Temeke watu wanalala mpaka chini achilia mbali vianda watatu watatu. Ni lazima tuchukue hatua mwafaka kwa mafisadi ili resources za nchi ziwekwe kwenye matumizi sahihi. Hii pia aligundua NAO ama? Nafikiri upo ufisadi mdogomdogo na mkubwa kwenye wizara na halimashauri ni vizuri watu wakauanika na kuweka mambo sawa. Tumechoka jamani. It is enough....
 
Back
Top Bottom