Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,710
- 40,777
Kiwira bado kuzalisha megawati 200
2007-06-24
Na Radio One Habari
Mgodi wa Makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya, bado haujaanza kuzalisha megawati 200 za umeme licha ya awamu ya kwanza ya mradi huo kupangwa kukamilika mwezi ujao.
Kwa mujibu wa mkataba wa miaka 20 wa kuzalisha umeme wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 340 awamu ya kwanza ya umeme wa megawati 50 ulipangwa kukamilika mwezi ujao.
Hii ni kwa mujibu wa mkataba huo kati ya serikali, Mgodi huo na Shirika la Umeme hapa Nchini TANESCO ambapo mgodi ulikuwa uanze awamu ya pili ya kuzalisha megawati zingine 100 za umeme mwezi Novemba mwaka huu.
Hata hivyo ujumbe wa TANESCO ulipotembelea mgodi huo wataalamu walisema kwa mwendo uliopo, huenda mradi huo ukachukua miaka mingi kukamilika kinyume na matarajio ya serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi Bw. Evance Mapundi amesema mchakato wa kuwatafuta wakandarasi umekamilika na kwamba awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo wa kuzalisha megawatt 50 utaanza Mwezi Septemba na kukamilika baada ya miezi kumi na nane.
SOURCE: Radio One
My take:
We need to know who did what and where are they now!? Kama watu walidhania IPTL na RDC kuwa ni majinamizi ya mikataba, here comes Mchuchuma na Kiwira!!