KIWIRA na MCHUCHUMA: A Campaign To Reclaim...

KIWIRA na MCHUCHUMA: A Campaign To Reclaim...

Binafsi sipendi kuambiwa na Ngeleja nani mmliki wa Kiwira kwasababu tayari tunajua nani ni mmliki wa Kiwira,katika hili nadhani nitapata na wengine wa kuniunga mkono.Tunajua Mkapa na Yona wanamiliki Kiwira,sasa kama wameamua kupachika majina ya watoto wao hakuwezi kuwaondoa wao kumiliki mgodi wa Kiwira.
Ningefurahi kusikia serekali ikituambia hatua gani imepanga kuzichukua iwapo itabainika Mkapa na Yona walitumia madaraka yao vibaya au kwa manufaa yao na familia.
 
Alipaswa kuitoa taarifa hii Bungeni katika kikao kilichopita lakini hakufanya hivyo, kwa nini? Ngeleja, tafadhali achana na cheap politics. Ulikutana na hao waandishi kwa nini ukuitoa hiyo taarifa? Kumbuka ilishanenwa kuwa Watanzania si mabwege tena
 
Tunaomba hili swala lisiwe SIASA!maanake kwa sasa kitu nashindwa kukielewa katika hili swala la kufichua uozo ndani ya serikali.INAWEZEKANA NI MBINU T.hasa inapozingatiwa kuwa mwakani tuna uchaguzi

AMKENI WATANZANIA
 
Ngeleja anasubiri nini "kufichua siri ya Kiwira"? 😕
 
Bongo noma kweli yaani hata wizi unatumika kwa ajili ya manufaa ya kisiasa. Ngereja umeamua kufanya siasa katika kodi zetu zilizoibiwa na mafisadi. Brela wametuambia nani ni mmiliki wa Kiwira siri gani hiyo mpya uliyonayo????.Tunashukuru sana kwa kutufanya mabwege ila ipo siku tutapata uhuru wa kweli kutoka kwenu wakoloni wa ndani na kwa taarifa yako siku zenu zinahesabika hata na mtoto wa miaka miwili.

Issue iko wazi miaka kibao inajulikana unawaita waandishi wa habari na kuwapotezea muda wao kwa mashairi yako yasiyoukuwa na maana bila sababu. Anyway basi tufanyeni sisi wote wajinga ila kama nilivyosema siku zetu zinahesabika. Ahsante.
 
Mradi wa Kiwira wafukuzisha wanafunzi

2009-03-08 11:38:33
Na Thobias Mwanakatwe, Mbeya
​

Wafanyakazi wa Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira uliopo mkoani hapa wameanza kuonja machungu ya kutolipwa mishahara yao, kufuatia wanafunzi 102 ambao ni watoto wao wanaosoma katika Shule ya Sekondari ya Kiwira Coal Mine iliyopo Wilayani Kyela kufukuzwa shule kutokana na wazazi wao kushindwa kuwalipia ada.

Wafanyakazi wa mgodi huo hawajalipwa mishahara yao kwa miezi nane sasa ambayo imefikia zaidi ya shilingi bilioni mbili ambapo wamiliki wa mgodi wanapotafutwa kujua ni lini watalipa simu zao zimekuwa zikiita bila ya kupokelewa.

Wanafunzi hao walianza kufukuzwa shuleni tangu wiki iliyopita kwa awamu na uongozi wa shule hiyo kutokana na kutolipa ada kwa muda mrefu hali iliyosababisha shule kushindwa kununua mahitaji muhimu ya shule.


Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (Tamico) tawi la Kiwira, Kibona amemwandikia barua Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mashimba Mashimba kumjulisha hali hiyo ikiwa ni pamoja na kumuomba wanafunzi hao warejeshwe shule wakaendelee na masomo wakati wazazi wao wanatafuta pesa za ada.

Kibona alisema kimsingi siyo kwamba wafanyakazi wa Mgodi wa Kiwira Coal Mine wanakataa kulipa ada hiyo lakini ukweli ni kwamba hawana fedha kwa sababu wamiliki wa mgodi huo hawajawalipa mishahara kwa zaidi ya miezi nane sasa.

Alisema wafanyakazi wa mgodi huo wamepewe muda kidogo kwa ajili ya kutafuta ada hiyo lakini wakati huo wanafunzi warejeshwe shuleni kwani kuwafukuza kunakosesha haki yao ya msingi ya kusoma na wala wao hawana kosa lolote kwani wazazi wao hawajalipwa mishahara na wamiliki wa mgodi.


Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mashimba akizungumza na Nipashe kwa simu alikiri kupokea barua kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Migodi Kiwira Coal Mine ikielezea kusudio la kufukuzwa wanafunzi hao kutokana na wazazi wao kutolipa ada.

Mashimba alisema hata hivyo kitendo cha kufukuzwa wanafunzi hao kwa sababu wazazi wao hawajalipa ada ni kinyume cha agizo la serikali ambayo iliagiza wanafunzi wasifukuzwe shule kwa sababu ya ada na badala yake kinachotakiwa kufanywa ni wazazi kuitwa na kupewa mkakati wa jinsi nya kulipa ada hiyo.

Mapema mwezi Januari 17 mwaka huu Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembela katika mgodi huo, wafanyakazi waliwaeleza wabunge kuwa kutokana na kutolipwa mishahara hali za maisha zimekuwa mbaya sana ambapo baadhi yao wanalazimika kuwaweka rehani wake zao ili wapate fedha za kuwalisha watoto wao.
SOURCE: Nipashe
 
Nadhani imefika wakati wa sisi kuamka jamani, tunapochagua rais lazima tuangalie alifanya nini siku za nyuma, sio anatuambia nini leo!

Kikwete alishashindwa zamani sana wizara ya nishati tangu alipokuwa waziri wa wizara hiyo, leo tungetegemea basi baada ya kuingia ikulu athibitishe kuwa alishindwa nyakati zile kwa sababu hakuwa rais! leo anaweza kwa sababu rais! lakini sivyo!!

Kikwete anawaza kuingia ikulu tena 2010, mgao wa umeme, kiwira, ufisadi, shauri zenu kafieni mbali na watoto wenu!

Tatizo sisi nadhani wala sio viongozi tunaowachagua wallah! maana viongozi wetu wanaelezea sisi tulivyo! sitaki kuamini, lakini may be ""NDIVYO TULIVYO"(NG 2009).
 
Wakuu,

Ni kweli wafanyakazi wa mgodi wa Kiwira wana hali mbaya sana. Mgodi wao unazidi kufa
kwasababu ya malumbano ya siasa.

Nafikiri sasa tunawaadhibu hawa wafanyakazi badala ya kuwaadhibu mafisadi. Serikali ichukue uamuzi wa haraka wa kuutaifisha huu mgodi na kuufufua kabla ya kutafuta wawekezaji wa maana kwa faida ya nchi nzima na wananchi wa Kyela ambao walikuwa wanautegemea sana huu mgodi.

Mali kadhaa za mgodi zimeanza kuibiwa na kadri serikali inavyochukua muda mrefu kutoa maamuzi, ndivyo jinsi uharibifu unavyozidi kuongezeka.

Viongozi wa wilaya pia walipigie kelele hili jambo. Huu mgodi ukifa, itakuwa ni hasara kubwa sana kwa taifa na kwa wananchi wa Kyela.

Kama hatuna mpango wa kusimamia huu mgodi basi hata ilikuwa afadhali kumwachia fisadi Mkapa kuliko kuuachia ufe kama ilivyo sasa.

Ukiona hao wafanyakazi mpaka wanashindwa kulipia wanao shule jua hali ni mbaya sana. Ada ya hiyo shule ni kama laki mbili kwa mwaka, sio pesa nyingi, kama wanafunzi wanafukuzwa, hiyo ni ishara tosha kwamba wazazi wao wana hali mbaya sana kifedha.
 
What really happened kwa KIWIRA...mpaka kufikia hali hii

Au ndio ile systematic subotage inayoendelea ili ku-justify......mambo fulani
 
Unajua Mwanakijiji ukiamua kushinda uoga kuthubutu kurudi nyumbani na ukaendeleza hizi kampeni zako katika mikakati rasmi utalisaidia sana Taifa.....

Huu utamaduni wa kubwekea nje ya uzio wa nyumba ni mojawapo ya upotevu wa RESOURCES adimu tulizonazo katika kusukuma gurudumu la DEMOKRASIA nchini.

omarilyas
 
Mwezi umekatika sasa tangu Ngeleja atuahidi 'kufichua siri ya Kiwira' hapo February 18, 2009. Hii ni ushahidi mwingine kwamba Ngeleja kazi imemshinda

Ngeleja kufichua siri ya Kiwira

na Kulwa Karedia
Tanzania Daima~Sauti ya watu
​

SERIKALI imesema imejiandaa kuanika ukweli na hatima ya mgodi wa mawe wa Kiwira, wakati wowote kuanzia sasa kwa maslahi ya taifa.

Akitoa taarifa ya serikali kwa waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana kuhusu kuuzwa kwa asilimia 75 za kampuni ya Williamson Diamond, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema serikali imekamilisha kukusanya taarifa za mgodi huo ambao majibu yake yanasubiriwa na Watanzania wengi.

"Napenda kuwaambia kwamba kila kitu juu ya mgodi huu kimekamilika, ni matumaini yangu kwamba wakati wowote kuanzia sasa tutaanika ukweli na hatima ya mgodi huu ambao umezua mambo mengi katika siku hivi karibuni," alisema Waziri Ngeleja.

"Hatuna sababu ya kuchelewesha suala hili, tuko tayari kufafanua mambo yote yaliyofanyika na yale ambayo tunaona yana faida kwa taifa katika siku zijazo," alisema Waziri Ngeleja.

Serikali haitakaa kimya kwani katika mkutano wa 14 wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita mjini Dodoma, suala hili lilikuwa limewekwa kwenye orodha ya kujadiliwa lakini ilishindikana kutokana na muda.

"Baada ya suala hili kutojadiliwa bungeni, watu wanaweza kusema tumeingia ‘mitini'…nasema ndugu zangu hapana…tupo pamoja kwa nia ya kujenga taifa letu," alisema Ngeleja.

Katika hatua nyingine, Ngeleja alisema serikali imeridhia uuzaji wa asilimia 75 za kampuni ya Williamson Daimonds Limited zilizokuwa zinamilikiwa na kampuni ya Willcroft Limited.

Alisema baada ya uchunguzi wa kina kufanyika, serikali imeridhia kuuza kiasi hicho kwa kampuni ya Petra Diamond ambayo iliingia mkataba wa kununua kampuni ya Willcoft Limited.

"Baada ya kupokea ushauri wa kamati ya wataalamu wa kisekta ya serikali na ule wa kamati ya ushauri ya Jaji Mark Bomani na kujiridhisha kuwa mbia, Petra Diamond ina uwezo wa kuendesha mgodi wa almasi, serikali imeona kampuni hiyo haina kikwazo, hivyo kukabidhiwa mgodi," alisema Ngeleja.

Masharti yaliyowekwa na serikali ni pamoja na Petra Diamond itambue mikataba iliyopo kati ya serikali na Willcroft na kuendeleza majadiliano ya kurekebisha hali ya mgodi huo ili uweze kuleta manufaa zaidi kwa taifa.

Alisema serikali itaendelea na majadiliano na mbia wake huyo kupitia upya mkataba wa wanahisa ili uendane na wakati uliopo kwa manufaa ya pande zote.

"Majadiliano yatahusu pia mradi wa upanuzi wa shughuli za uzalishaji wa almasi ili mgodi uweze kuzalisha kati ya karati 500,000 na 1,000,000 kwa mwaka badala ya 200,000 zinazozalishwa hivi sasa," alisema Ngeleja.

Serikali itahakikisha maslahi ya wafanyakazi wa mgodi huo yanalindwa na Petra itaendeleza miradi na huduma za kijamii zilizokuwa zinatolewa na kampuni ya De Beers na mradi wa Mwadui Community Diamonds Partenership (MCDP), unaohusu kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa eneo la Mwadui.
 
..hatuchelewi kusikia kaja Hosea na kusema kila kitu kilifata utaratibu uliotakiwa na Kiwira ni swaaafi!
 
Unajua Mwanakijiji ukiamua kushinda uoga kuthubutu kurudi nyumbani na ukaendeleza hizi kampeni zako katika mikakati rasmi utalisaidia sana Taifa.....

Huu utamaduni wa kubwekea nje ya uzio wa nyumba ni mojawapo ya upotevu wa RESOURCES adimu tulizonazo katika kusukuma gurudumu la DEMOKRASIA nchini.

omarilyas
Mmh!, yana ukweli haya!, au iwe rahisi kumziba mdogo kama hawa wengine waliopo?
 
Tanzania earned only $17.4 over five-year price boom

home+sub+2+pix.jpg

Prof Oim Ajakaiye of Africa Economic Research Consortium displays the report by experts on exploitation of minerals by African governments as mobilisation for internal resources for development. Photo/ANTHONY KAMAU​

By KEVIN KELLEY
THE EAST AFRICAN

Posted Saturday, March 28 2009 at 00:53

Tanzania has collected only $1 million in income tax from foreign mining companies even though they exported nearly $3 billion worth of gold over a four-year period, a new report has revealed.

As at the end of last year, AngloGold Ashanti was the sole mining company operating in Tanzania to have paid any corporate income tax, says the report by Action Aid and other advocacy groups.

The company made a $1 million payment in 2007 on its Geita gold mine operation, which provided Johannesburg-based AngloGold Ashanti with gross profits of $93 million between 2002 and mid 2007.

According to the report, Canada-based Barick Gold, another large mining company doing business in Tanzania, reported a net income of $97 million between 2004 and the first half of 2007 but paid no corporate income tax to the Tanzanian government.

Between 2002 and 2006, mining companies exported around $2.9 billion worth of gold. During that time, the government earned around $17.4 million in royalties, charged at 3 per cent of the market value minus transport and transaction costs.


"If royalties were charged at 5 per cent as it has now been recommended by a presidential commission, the government revenue would have increased to $145 million over the next five years," says the report titled: "Breaking the Curse: How Transparent Taxation and Fair Taxes can Turn Africa's Mineral Wealth into Development."

"Mining companies operating in Africa are granted too many tax subsidies and concessions," says the report, which also covers Congo, Ghana, Malawi, Sierra Leone, South Africa and Zambia. "There is high incidence of tax avoidance by mining companies conditioned by such measures as secret mining contracts, corporate mergers and acquisitions, and various ‘creative' accounting mechanisms."

Tanzania negotiates from a position of weakness in its dealings with multinational mining corporations, says Peter Kafumu, the country's Commissioner for Minerals.

He says: "The companies are holding a panga by the handle and we are getting the sharp end."

Foreign governments also lobby in Tanzania on behalf of the mining companies, the report says.

It says that in June last year, the staff of the Canadian High Commission in Tanzania tried to influence parliamentarians to reject the recommendations of the Bomani Commission which had been appointed by President Jakaya Kikwete to review the country's mining contracts and legal framework.

The companies further try to take advantage of weaknesses in Tanzania's legal structure, the report adds

It quotes Mr Kafumu as saying: "We have no capacity to look at their books. The companies can write the books so that third world countries cannot regulate. Even the contracts are difficult. I think the mining companies exploit our weaknesses in law and capacity."

The companies have used their negotiating leverage to gain exemptions from local government taxes and fuel levies, the report adds.


It notes that under negotiated agreements, the mining companies do not pay local government taxes in excess of $200,000 a year. And even that sum, which is much lower than standard tax rates, is not fully collected.

Royalties account for the largest source of revenues that the Tanzanian government is able to collect from the companies.

It earned about $17 million in royalties per year during a five-year period. The figure is the product of a 3 per cent charge on the market value of gold exports, minus the cost of transportation and transactions.

Meanwhile, mining companies in Tanzania are expected to make their formal response to the accusations contained in the report.

Industrial sources told The EastAfrican that think the companies and the chamber for energy and minerals would be making a formal response to what is contained in the report.

"It is not good for the industry or the country," said the sources.

Additional reporting by Joseph Mwamunyange
 
Nimepata sketchy report kwamba Waziri Mkuu amesema kuwa hisa za Kiwira zitarudishwa serikalini na kuwa kosa hilo la Mkapa (kwamba ni "kosa moja") lisitufanye tumhukumu vikali.

Kama habari itakuwa ndivyo ilivyo itakuwa ni kutimiza ile kampeni yetu ya kureclaim Kiwira..
 
ngoja tuwasikilize wabunge, sijui ni wabunge wepi wataomba nafasi ya kuchangia. Hon. Zitto, Cheyo and Slaa, please mtuwakilishe, you know a lot about Kiwira.
 
Nziku.. sidhani kama kuna mjadala.. uamuzi umeshachukuliwa. Kiwira inarudishwa serikalini. HIvyo ndivyo nilivyoipata sijui technicalities zake.
 
oh! sasa ile agenda ya bungeni itafutwa nini? siku Dr. Slaa anatoa hoja ya upinzani bungeni aliamriwa asiongelee Kiwira kwakuwa ipo kwenye agenda za bunge hili.
 
Nziku.. sidhani kama kuna mjadala.. uamuzi umeshachukuliwa. Kiwira inarudishwa serikalini. HIvyo ndivyo nilivyoipata sijui technicalities zake.

Deni lililopo atalipa nani kati ya serikali na Mkapa?.

Mgodi unarudi serikalini ama serikali inaununua upya mgodi huo toka kwa Mkapa?
 
Back
Top Bottom