Daily News;
June 03, 2008
Kampuni ya Makaa ya Mawe na Nishati ya Kiwira (KCP), imetamba kuwa umeme wake utakuwa wa bei nafuu ambao utalipa faida kubwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
KCP pia imesema mkataba wake ambao wameingia na Tanesco kamwe hautakuwa mzigo kwa shirika hilo na kwa serikali. Akizungumza na gazeti mwishoni mwa wiki, Mtendaji Mkuu wa KCP, Francis Tabaro alisema mkataba walioingia na Tanesco ni kuliuzia shirika hilo uniti moja kwa senti tano, kiasi alichodai kuwa ni kidogo ikilinganishwa na bei za umeme wa kampuni nyingine.
Kiwango hicho si tu kwamba ni cha chini, bali ni cha chini hata kwa Afrika Mashariki na Kati, alisema Tabaro wakati akijibu swali aeleze namna ambavyo wameingia mkataba na Tanesco. Alisema kiwango hicho cha bei ya umeme kilipendekezwa na serikali yenyewe wakati huo Waziri wa Nishati na Madini, akiwa Dk. Ibrahim Msabaha.
Sisi tuliwapa kile ambacho serikali ilitaka, maana Dk. Msabaha alisema kama tusipokubaliana na bei hiyo, asingeruhusu mkataba na Tanesco kusainiwa, alisema. Mtendaji huyo alisema umeme wa makaa ya mawe gharama zake ni rahisi kama ulivyo wa maji ndiyo maana kampuni yao inaona ni vyema ikaiuzia Tanesco kwa bei hiyo ili shirika hilo litakapouza lipate faida.
Ninavyojua mimi umeme wa gesi na umeme wa dizeli ni aghali na Tanesco inalazima kupata ruzuku kutoka serikalini ili imudu kununua kwa kampuni zinazozalisha umeme wa namna hiyo, alisema. Tanzania kwa sasa inatumia umeme wa maji ambao unaelezwa kuwa ni rahisi kuliko umeme mwingine. Pia inatumia umeme unaotokana na gesi na dizeli.
Kampuni ya IPTL inazalisha umeme wa dizeli, wakati Songas, Aggreko na Dowans wanazalisha umeme wa gesi. Licha ya kuwa na utajiri wa makaa ya mawe, Tanzania haikuwahi kufaidi nishati ya madini hayo. Tabaro alisema Tanesco itapata faida kubwa kampuni yake itakapoanza kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kwani itakuwa mara ya kwanza kununua umeme wa bei ya chini na kuuza kwa faida.
Alisema wanatarajia kuanza kuzalisha megawati 50 ifikapo Aprili mwaka 2010. Alisema Oktoba mwaka huo huo, kampuni yake itazalisha megawati 150 hivyo kufanya jumla ya megawati zitakazokuwa zinazalishwa na kampuni hiyo kufikia 200, umeme ambao utaingizwa kwenye gridi ya taifa.
Alisema kuanzia mwaka 2012 itaanza kuzalisha megawati zingine 200 hivyo kufanya umeme utakaotoka Kiwira kuwa megawati 400. KCP inamilikiwa na Tanpower kwa asilimia 85 na serikali ina hisa 15 tu mgodi huo uliuzwa kwa kampuni hiyo kwa Sh milioni 700. Katika kuhakikisha umeme wake unaingia kwenye gridi ya taifa, Tabaro alisema watajenga njia ya umeme ya 220kv kutoka Kiwira hadi Mbeya umbali wa kilometa 100.