Kuntakinte
JF-Expert Member
- May 26, 2007
- 701
- 37
Kwani huu Mgodi wa Kiwira ni wa Serikali? Nauliza tuu jamani...?
Nafkiri kuna ulazima wa kuweka lengo la kutimua atleast 90% ya civil servants hasa wa Makao Makuu ya wizara na kuajiri upya... Ndio, bora kuanza upya kuisuka serikali!... Watu na elimu zao huko serikalini hawana uchungu kabisa na nchi inavyoonekana.
Tatizo ni USIRI, sio civil servants per se. Civil Servants wenyewe wanasema hawakuona mkataba. Bunge halikuona, wala haliruhusiwi kuona mkataba. Hata kamati za bunge haziruhusiwi kuona na kuidhinisha mikataba. Wanaoona na kuruhusu hii mikataba ni mawaziri tu! Wanaisaini mahotelini, wakati mwingine hata nje ya nchi.
Wenye uzoefu wa magari wanajua inafika mahali linaharibika sehemu nyingi kiasi kwamba halifai kutengeneza tena, ni la kubadilisha. Hii serikali imefika mahali kama hapo. Kila unaposhika unakuta pameoza. Si ya kukarabati, ni ya kubadilisha.
Tuige Ghana. Chama kinachoingia madarakani huko Ghana sasa kilikuwa chama tawala siku za nyuma, kikawekwa benji, na sasa kimeahidi hakitafanya makosa makubwa kwani kilijifunza mengi wakati kikiwa benji.
Kama Watanzania hawataiweka CCM upinzani mwaka kesho, basi wakubali kuendalea na hivi viini macho vya kila siku.
Wizi mtupu!
Nadhani ukisema Watanazania ni watulivu tunakosea. Viongozi wetu wana-define kwamba Watanzania ni WAJINGA, MAMBUMBU! MABOZA, YAMELALA KUFAAA n.k ndiyo maana hata Wakenya wanataka Muungano wa EAT AFRICA Ukamilishwe haraka ili waje wamalizie vilivyomo. Maana sijui tujilinganishe na viumbe gani waiishio huu ulimwengu. AIBU TUPUUU! Viongozi hawa wemetokea wapi?? Huenda siyo Watanzania?? Mbona wana-act utadhani hawana roho, moyo, wala damu. Hivi ni binadamu wa kawaida kama sisi??? Huenda wameingia kwenye system kutoka familia ya Mugabe??? Maana sipati pichaa!!!