Kiwanda cha Mazava Morogoro Chasisitizwa Kuzingatia Utunzaji wa Mazingira na Usalama wa Mahali pa Kazi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
945

MBUNGE NORAH MZERU ASISITIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA USALAMA MAHALI PA KAZI KIWANDA CHA NGUO CHA MAZAVA MOROGORO

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru mnamo tarehe 05 Machi, 2023 amefanya ziara na kutembelea Kiwanda cha Uzalishaji Nguo cha Mazava kilichopo katika Manispaa ya Morogoro na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinavyofanyika Kiwandani.

Kiwanda cha Mazava (Mazava Fabrics & Production E.A.Ltd) ni miongoni mwa Viwanda vikubwa mkoani Morogoro kinachozalisha Nguo za Michezo ambapo kwa Mwezi kinafanya uzalishaji mpaka Nguo 1,300,000 na kina wafanyakazi takribani 2600.

Lengo la ziara ya Mhe. Norah Waziri Mzeru ilikuwa ni kusikiliza kero Kiwandani hapo kwa wafanyakazi lakini pia kutafuta njia nzuri ya kuweka mazingira bora ya mwekezaji kutokana na utoaji wa fursa za ajira kwa vijana wa Morogoro

Mhe. Norah Waziri Mzeru amesema katika swali aliloliuliza Bungeni lililenga Kiwanda cha Mazava kwa kutaka kujua ni lini Viwanda ambavyo wawekezaji wamewekeza hususani hapa Mazava watatengewa maeneo maalum ya akiba ya ardhi na uwekezaji ili watoke kwenye kulipa kodi ya pango wawe na maeneo yao kwani wamekuwa wakichangia sana ajira kwa Vijana wetu.

Aidha, Mhe. Norah Waziri Mzeru ameeleza kuwa ujio wake katika Kiwanda cha Mazava ni kuoana namna ya kuwatetea wawekezaji kupatiwa maeneo ya uwekezaji, ambapo Mazava wamekuwa wakizalisha ajira nyingi za Vijana, na yeye kama Mbunge wao wa Morogoro ameona hili alisemee Bungeni ili Serikali ione namna ya kuwasaidia wawekezaji.

Katika hatua nyingine Mhe. Mzeru amewaomba wawekezaji wa Kiwanda cha Mazava Kuboresha masilahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi, asilimia kubwa ya Vijana wanaofanya kazi katika Kiwanda cha Mazava wanatoka katika maisha duni yenye vipato vya chini, maslahi yao yakiwa mazuri wataweza kusaidia familia zao kwa ufanisi.

"Mbali na maslahi ya wafanyakazi lakini hakikisheni usalama mahala pa kazi unazingatiwa, sheria ya kazi inatutaka hivyo kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi wetu kuwa salama kazini." - Mhe. Norah Waziri Mzeru

"Sanjari na hapo, kikubwa kingine wawekezaji mzingatie usafi wa mazingira, nchi yetu imekuwa ikikabiriwa na mabadiliko ya tabianchi, hivyo kuna kila sababu ya Viwanda vyetu kutusaidia kuweka mazingira safi na salama." - Mhe. Norah Waziri Mzeru

Aidha, Mhe. Norah Waziri Mzeru ameelekeza shukrani za kipekee na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea watanzania maendeleo kwani amekuwa akihangaika kuhakikisha anatimiza malengo ya Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Mwisho, Mhe. Mzeru ameupongeza uongozi wa Kiwanda cha Mazava kwa kazi nzuri wanayoifanya ya uzalishaji wa bidhaa zenye ubora na kuwaomba waongeze ubora zaidi kwenye masoko kwani uzalishaji unapoongezeka na masoko yanatakiwa yaongezeke ili wafanayakazi waendelee kufanya kazi kuliko kuwa na uzalishaji mkubwa na hakuna masoko ambayo inaweza kupelekea tena Vijana wetu kupunguzwa kukaa mtaani bila kazi kutokana na kukosa masoko ya bidhaa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.14(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.14(2).jpeg
    80.8 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.14(3).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.14(3).jpeg
    59.4 KB · Views: 14
  • WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.14(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.14(1).jpeg
    97.4 KB · Views: 19
  • WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.14.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.14.jpeg
    109.7 KB · Views: 13
  • WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.13(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.13(2).jpeg
    100.9 KB · Views: 16
  • WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.11(3).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.11(3).jpeg
    47.7 KB · Views: 10
  • WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.10(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-06 at 08.31.10(2).jpeg
    73.1 KB · Views: 12
Back
Top Bottom