DOKEZO Kituo cha Afya Zamzam (Bukoba) kuna huduma mbovu, Watumishi wanatengeneza mazingira ya Rushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kituo cha Afya Zamzam kilichopo Manispaa ya Bukoba huku Mkoani Kagera kinatoa huduma mbovu sana upande wa afya, hasa kwa Wanawake Wajawazito.

Haijalishi kama una kadi ya Bima au la, bado huduma zao ni mbovu hasa upande wa Wodi ya Wajawazito.

Watumishi wa Kituo hicho cha Serikali ambacho pia kinalaza wagonjwa kipo Bukoba Mjini, Kata Bilele wamekuwa na kawaida ya kutengeneza mazingira ya rushwa na kutojali wateja ambao hawaoneshi kuwapa ushirikiano katika kile wanachokitaka.

Nayasema haya nikiwa na uzoefu kwa kuwa awali nilikuwa nasikilia tu kuhusu hizo taarifa nikaenda mwenyewe kumpeleka mke wangu, nikakutana na mazingira ya delay ambazo hazikuwa na sababu.

Ninatumia Bima ya NHIF lakini bado unaambiwa hiki hakuna kile hakuna wakati ni vitu vidogo, wanakutaka uende nje ukanunue kwa gharama zako mwenyewe bila kutaka kusikiliza maelezo yako.

Jinsi wanavyowahudumia wagonjwa ni kama watu ambao wana ugomvi nao, ilibidi niombe transfer kupelekwa Hospitali ya Rufaa baada ya kuona tunapoelekea nitampoteza mke wangu.

Kituo hiki kimekuwa kama lango la kifo kutokana na huduma mbaya zinazotolewa na wahudumu husika.

Kama hatua hazitachukuliwa basi ni wazi inawezekana tukaendelea kushuhudia maisha ya watu wanaoenda kituoni hapo kutibiwa ama wakipoteza maisha au kuzidi kupata madhara zaidi ya ugonjwa uliosababisha wakaenda kituoni hapo.
 
Inasikitisha Sana na sio hapo tu zipo hospital nyingi tu za serikali zenye huduma mbovu hata hapa dar na shida ni kwamba wenye mamlaka hawafuatilii
 
Pole sana kwa kadhia. Lakini nashauri ili mamlaka ziweze kushughulikia vizuri pia ungewapa muongozo ikiwemo tarehe uliyohudhuria pale kituoni ili iwe rahisi kushughulikia.

Na hii itasaidia kutowajumuisha kila mmoja, sio kwamba wahudumu wote wana shida hivyo tusiwakatishe tamaa kwa kugeneralize tuhuma. Wengine ni wananchi wa Bukoba na hatujawahi kukutana na changamoto kama hizi na kwa kuwa kwako limetokea basi tunashauri mamlaka zichukue hatua lakini wasaidie sasa ni lini tukio hilo limetokea na hayo mazingira ya rushwa yaelezwe kwa kina.
 
Back
Top Bottom