DOKEZO Huduma za Afya Hospitali ya Magunga (Korogwe Mjini – Tanga) ni mbovu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
GRACE HONDI TLUWAY ni mgonjwa ambaye alienda mchana wa Saa Saba katika Hospitali ya Magunga kwa ajili ya kupata matibabu na aliondoka bila kupatiwa dawa kwa madai ya mtandao.

Alipelekwa tena hospitali hapo Saa Tatu Usiku kwa ajili ya kupata matibabu baada ya hali kuendelea kuwa mbaya zaidi.

Walipofika walielekea pharmacy kupata dawa kwa kuwa shida yake inajulikana, nesi wa zamu Ms Mary Mkande alikataa kuwahudumia akidai kwamba hakuna mtandao lakini wakati huo akiwa anachezea YouTube na pia kadi ya bima ya Mgonjwa ikiwa imeshaingizwa na kusoma kama imetumika tangu mchana wake (Saa Saba mchana) lakini anakataa kumpa dawa mgonjwa.

Namba ya kadi ni hii #10190328….. (Grace HONDI Tluway imetumika Korogwe District Hospital (Magunga) 14/02/2024 01:16 PM Ref# 720422486207. Piga namba 199 iwapo hutambui muamala huu.)

MAONI
Hospitali hii imekuwa na changamoto kubwa sana hususani kwenye utoaji wa Huduma za Afya kwa Wananchi ikiwa ni pamoja na huduma ya upasuaji wakina mama wengi Wajawazito wamepoteza maisha kutokana na uzembe wa madaktari wakati wa upasuaji au siku tatu baada ya upasuaji mteja anavimba tumbo na mwisho wa siku anapoteza maisha hapa hospitali pafanyiwe uchunguzi wa haraka ili kuokoa wajawazito walio wengi.
 
Uzembe wa watumishi wa afya.

Kufanya kazi kwa mazoea.

Huo ni uhuni
 
Ulichoeleza mtoa mda kina ukweli kwa 💯%. Huduma kwenye hospitali ya Magunga ni mbovu kupitiliza. Hapo mhonjwa akirnda kupata matibabu, hata panadol tu ataambiwa akanunue duka la dawa.

Wahudumu wana majibu ya jeuri! Sijui ni kwa sababu Wasambaa ni wapole, ndiyo maana wanatuletea za kuleta!! Na ubovu wa hizo huduma, upo miaka nenda.

Wagonjwa wengi wanaona bora waende hispitali ya Majengo! Na siyo Magunga. Na wale wenye pesa huwa wanaenda kituo cha afya cha Kwa Mndolwa kinachomilikiwa na Masister wa Katoliki.
 
Back
Top Bottom