Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Kituo cha Afya Ugala kilichopo Kata ya Ugala, Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi kipo katika hali ambayo si rafiki kwa Wagonjwa kwani kimezungukwa na vichaka virefu vya nyasi licha ya kituo hicho tayari kimeshaanza kutoa huduma za afya kwa Watanzania walio karibu na kituo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amefanya ziara ya kutembelea kituo hicho cha afya Ugala na kukuta kimezungukwa na nyasi nyingi ambapo ameuliza baadhi ya Watendaji wa Serikali katika Halmashauri ya Nsimbo ili kujua sababu ya kuwepo kichaka hicho lakini hakupewa majibu ya kuridhisha.
Afisa Tarafa, Ndurumo Pesambili Semuyemba na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mohamed Ramadhani wamesema hali hiyo imefanywa na baadhi ya Watendaji wa eneo hilo ambapo wamedai mradi huo ulisimama kwa takribani mwaka mzima ikidaiwa pesa zilikwisha na Kituo cha Afya hakijakamilika huku Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf licha ya kutembelea kituo hicho mwezi uliopita amesikitishwa kukuta hali hiyo na kuomba kupewa muda ili kuweza kuwashughulikia baadhi ya wazembe ambao wameshindwa kufanya usafi.
Mkuu wa Mkoa Mwanamvua Mrindoko amesema amekerwa na kusikitishwa licha ya pesa kuisha za kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha Afya na pesa zimeshakwisha.
Aidha, Mrindoko amewasimamisha baadhi ya Watumishi ili wapishe uchinguzi akiwemo mganga mkuu wa halimashauri ya Nsimbo, afisa tarafa tarafa ya Ndurumo, mtendaji wa kata, mtendaji wa kijiji na wengine watakaoonekana wanahusika.