DOKEZO Maafisa wa Maji Lemara - Arusha (AUWSA) wana huduma mbovu, wanatengeneza mazingira ya rushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mkazi wa Arusha, nina kero kuhusu Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA), hapa Lemara kuhusu suala la kuunganishiwa maji.

Awali, tulivyofanya maombi ya kuunganishiwa maji ilikuwa Oktoba 2023, tukazungushwa weee, baadaye AUWSA wakasema kuna mtu au watu wa ‘survey’ watakuja kwa ajili ya kuangalia mazingira.

Picha linaanza Maafisa hao wakija wanakwambia utoe Shilingi 10,000 ya nauli ya Bajaj au Tax au kama wamekuja na usafiri wao unaambiwa utoe hela ya mafuta.

Hilo likapita, wakafanya kazi yao na kuondoka tukasubiri hadi Desemba 2023 wapo kimya kienda kuulizia wanakupa majibu ya hovyo.

Mwishoni mwa Desemba wakatuita kwenda kuchukua vifaa baada ya kuwa tumeshakamilisha malipo mengine yanayotakiwa kwa njia ya mfumo wa electronic.

Kuanzia wakati huo tumekuwa tukipigwa kalenda kuja kuunganishiwa licha ya kuwa vifaa tunavyo, ambacho wanacho wao na wanatakiwa kuja nacho ni Mita.

Ukiwapigia simu wanajibu kwa jeuri au wanakupa namba ya mtu wa kuja kukuunganishia maji, naye anakwambia andaa Shilingi 20,000 kwa kuwa akifunga maji atachafuka.

Hivyo, hiyo imekuwa ni kero kubwa, kwanza wanatulipisha hela ambazo hazipo kwenye utaratibu, maana yake hiyo ni rushwa, pili hata unapoonesha nia ya kutaka kutoa wanakuzungusha wanavyotaka wao.

Kinachouma ni jinsi wanavyotuletea pozi licha ya kuwa tumelipa karibia Shilingi 200,000 lakini huduma ni mbovu.
 
Back
Top Bottom