Kitila Mkumbo: Mkataba wa Bandari unafanana kila kitu na mkataba wa ujenzi wa Mlimani City

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Ukienda pale Dar es Salaam kuna sehemu inaitwa Mlimani City, na wengine wakienda Dar es Salaam na kama hawajafika Mlimani City wanahisi hawajafika Dar es Salaam.

Wakati tunaijenga Mlimani City tuliambiwa tunakiuza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumbe tulichukua eneo dogo na kumpa mwekezaji akajenga Mlimani City na leo wana Dar es Salaam na Watanzania wanajivunia Mlimani City.

Hizi habari za kuambiwa umeuza au haujauza haijaanza leo.

Pia soma

20230720_072537.jpg
 
Kuna kipindi katika maisha huwa ni busara zaidi kwa mtu kukaa kimya na kuacha watu wawe na shaka juu ya aidha upo timamu ama kuna walakini katika uelewa wako (mpumbavu) kuliko kufungua kinywa chako na kuondoa shaka yeyote juu ya upumbavu wako.

Inasikitisha Profesa mzima anamithilisha bandari za nchi na square meter kadhaa za ardhi ya chuo.

Kwa mentality hii si ajabu hata tukisikia Mlima Kilimanjaro umeuzwa pia.
 
Ina maana msomi kitila hasomi taarifa za CAG pale kuna mkataba wa miaka 100 chuo kinapata 10% tu hakiruhusiwi kumfanyia ukaguzi mwekezaji uchwara cha kusikitisha zaidi mwekezaji ana maamuzi had ya kupangisha maeneo bila chuo kuwa na kauli itoshe kusema kitila na PHD yake alitakiwa kuwa shule akisaidia watoto wajikinge na mimba za mapema.
 
Kuna kipindi katika maisha huwa ni busara zaidi kwa mtu kukaa kimya na kuacha watu wawe na shaka juu ya aidha upo timamu ama kuna walakini katika uelewa wako (mpumbavu) kuliko kufungia kinywa chako na kuondoa shaka yeyote juu ya upumbavu wako.

Inasikitisha Profesa mzima anamathilisha bandari za nchi na square meter kadhaa za ardhi ya chuo.

Kwa mentality hii si ajabu hata tukisikia ikulu imeuzwa pia.
Ameshakula nyama ya punda kaanza usumbufu.
 
Kuna kipindi katika maisha huwa ni busara zaidi kwa mtu kukaa kimya na kuacha watu wawe na shaka juu ya aidha upo timamu ama kuna walakini katika uelewa wako (mpumbavu) kuliko kufungia kinywa chako na kuondoa shaka yeyote juu ya upumbavu wako.

Inasikitisha Profesa mzima anamathilisha bandari za nchi na square meter kadhaa za ardhi ya chuo.

Kwa mentality hii si ajabu hata tukisikia Mlima Kilimanjaro umeuzwa pia.
Watu wanatetea ugali wao
 
Kitila anathibitisha wametoa bandari kwa DP WORKD miaka 100? Mkataba Mlimani Holding Limited (MHL) na UDSM (kujenga/kumiliki Mlimani City) ni wa miaka 99 (bado miaka 80). UDSM wanapata 10% ya mapato kwa mwaka. Miaka 99 baadae tutarithishwa maghala (warehouse)

Kwa kiferu zaidi tafuta taarifa ya CAG ujue huyu mwenye PHD fake alivyopotea
Du hatari 10% Kwa Miaka 100 crazy. Afu MTU anausifia mktaba
 
Ina maana msomi kitila hasomi taarifa za CAG pale kuna mkataba wa miaka 100 chuo kinapata 10% tu hakiruhusiwi kumfanyia ukaguzi mwekezaji uchwara cha kusikitisha zaidi mwekezaji ana maamuzi had ya kupangisha maeneo bila chuo kuwa na kauli itoshe kusema kitila na PHD yake alitakiwa kuwa shule akisaidia watoto wajikinge na mimba za mapema.
...itoshe kusema kitila na PHD yake alitakiwa kuwa shule akisaidia watoto wajikinge na mimba za mapema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkataba wa Mlimani City ndio Case Study ya Mkataba Bora ? Au ndio ungetumika kama funzo of what not to do ?!!!!

Hakuna mtu hajui kwamba kula ni lazima na usipokula utakufa..., ila haimaanishi ule junk foods wakati vyakula bora vipo....
 
Kuna kipindi katika maisha huwa ni busara zaidi kwa mtu kukaa kimya na kuacha watu wawe na shaka juu ya aidha upo timamu ama kuna walakini katika uelewa wako (mpumbavu) kuliko kufungia kinywa chako na kuondoa shaka yeyote juu ya upumbavu wako.

Inasikitisha Profesa mzima anamathilisha bandari za nchi na square meter kadhaa za ardhi ya chuo.

Kwa mentality hii si ajabu hata tukisikia Mlima Kilimanjaro umeuzwa pia.
Wapinzani wengi ni wasaka vyeo
 
Inawezekana pia hujamuelewa mkuu..maana mkataba wa mlimani city na wenyewe ni hovyo.

Jamaa alikuja na briefcase tu na dola mia basi. Kwa sasa ni bilionea.

Aliwaingiza chaka maprof.
 
Ina maana msomi kitila hasomi taarifa za CAG pale kuna mkataba wa miaka 100 chuo kinapata 10% tu hakiruhusiwi kumfanyia ukaguzi mwekezaji uchwara cha kusikitisha zaidi mwekezaji ana maamuzi had ya kupangisha maeneo bila chuo kuwa na kauli itoshe kusema kitila na PHD yake alitakiwa kuwa shule akisaidia watoto wajikinge na mimba za mapema.
Inawezekana yupo sahihi mkuu na hiki ndicho alichomaanisha. Katumia mlango wa nyuma ila inawezekana kuna wakubwa wenzie wamemuelewa.
 
Bahati nzuri sana nilihudhuria mhadhara mojawapo wa Late Professor Seth Chachage, kipindi kile Chachage alikua "very 🔥" na alituambia kuwa mojawapo ya vitu vilivyomo kwenye mkataba wa mlimani city ni Kwamba
1. Maduka yatakua yakiuza bidhaa mbali mbali ambazo zitawasaidia wanafunzi kwenda hapo kufanya shopping
2. Watajenga low cost houses ambazo zitasadia kusuala la malazi Kwa wanafunzi, kama mnakumbuka Adha ya accomodation UDSM ilikua issue kubwa sana,
3. Kuwa watajenga permanent structures hata baada ya mkataba wao kuisha

Sasa Kwa wenye wako na akili, wanaona yanayoendelea Leo hii, zile apartments za mlimani city ndio ambazo wanafunzi walijengewa eti wakae hapo, zile nguo za laki kadhaa ndio hizo wanafunzi wa UDSM wamewekewa wakavae.

Siku chache wakati joto likiwa juu sana Kuhusu mlimani city investment, Professor Seth Chachage akiwa Kibaha alidondoka baadae akatangazwa kuwa roho yake iliacha mwili
 
Back
Top Bottom