Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 3,564
- 3,472
Katika mahojiano kati ya Profesa Kitila Mkumbo na Mwandishi wa habari nimeweza kuelewa mambo yafuatayo:
Mosi, suala hili la mkataba wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Emirati ya Dubai linapitia katika hatua kadhaa na hatua iliyopo ni hatua ya makubaliano kati ya Serikali na Serikali "Intergovernmental agreement" hatua hii haijaonesha makubaliano mahususi juu ya maeneo mahususi.
Pili, Ipo hatua fuatizi ambayo ni makubaliano mahususi "consessional agreement" hatua hii ndiyo itakayobainisha makubaliano juu ya maeneo mahususi na ndiyo itakayoonesha kwa mawanda Serikali ya Tanzania itapata nini na Kampuni husika itapata nini.
Juu ya nukta hizo mbili kulingana na majibu ya Profesa alipokuwa akihojiwa ni kama upande wa upinzani unakimbilia kupinga kabla ya kukamilika kwa hatua zote muhimu za makubaliano.